Tetesi: Mabalozi wakubali DOWANS kulipwa

Hebu tuzibe masikio na macho Hizo zote ni disinfomation toka mafisadi ili kuhalalisha ufisadi huo!
kwa nini walipwe kwa kazi ipi walioifanya
Au siku hizi utapeli na ufisadi ni kazi yenye kustahili malipo.
 
...Alberto,

Unatuangusha ndugu kwa kudandia gari kwa mbele! Unauhakika gani hayo hapo juu ni maoni ya mabalozi? waliyatoa wapi na kwa nani? mtoa mada kakurupuka tu na kulibwaga thread hapa, huko anakusema ni chanzo cha hii habari hakuna chochote cha aina hii!

BWT: Habari za miaka mingi......! nice to see you here man!

Kaka, inawezekana habari hii imepotoshwa na mimi nikamuamini aliyeileta. Kama si kweli kipengele cha 'mabalozi wako sahihi' nakifuta. Lakini bado hayo mengine jaribu kuyatafakari.

My no. 0785533433 or 0767
 
Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini wakiwamo wa Jumuiya ya Ulaya (EU) wametoa maoni yao na kuafiki kuwa DOWANS walipwe, kwani hukumu hiyo imetolewa na mahakama ambayo wao wanaiheshimu ya ICC.

Kutokana na hivyo basi, wameitaka Tanzania kuheshimu mikataba ya kimataifa ambayo wameiridhia, ili kuimarisha utiifu wa sheria za kimataifa na kuwajibika nazo. Wametoa madhara ya kutofuata sheria za kimataifa ni pamoja na nchi wahisani kukosa imani na serikali na hivyo kupunguza au kuondoa misaada yao ili kuishinikiza serikali kufuata misingi ya utawala bora ya kimataifa.

April fool!
 
..Hapo Mhe. tupo pamoja!

Nitakucheki kwenye simu!
 
Mabalozi wanajua wanachokitaka. Wao wanasubiri hiyo cheque atapewa nani????????????????Hapo ndio ngoma ya kiduku itakavyonoga!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
He, mimi nilifikiri mabalozi wetu huku nje kumbe mabalozi wa nje humu ndani, wala sishangai kwa sababu sidhani kama wanauchungu na Mtanzania au wameahidi kuchangia kiasi fulani.
 
Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini wakiwamo wa Jumuiya ya Ulaya (EU) wametoa maoni yao na kuafiki kuwa DOWANS walipwe, kwani hukumu hiyo imetolewa na mahakama ambayo wao wanaiheshimu ya ICC.

Kutokana na hivyo basi, wameitaka Tanzania kuheshimu mikataba ya kimataifa ambayo wameiridhia, ili kuimarisha utiifu wa sheria za kimataifa na kuwajibika nazo. Wametoa madhara ya kutofuata sheria za kimataifa ni pamoja na nchi wahisani kukosa imani na serikali na hivyo kupunguza au kuondoa misaada yao ili kuishinikiza serikali kufuata misingi ya utawala bora ya kimataifa.

NDUGU NI GAZETI GANI LA Udaku ULIPOZISOMA HABARI HIZI????????????
 
Wengi wa mabalozi wanapewa hivi vyeo kwa uswahiba tu wala sio wenye ujuzi wa kuelewa mambo na mara nyingi sana wanavutia kwao kwa sababu wanafahamu nini kitafuata baada ya hapo , maslahi yao. Hata SA walipokuwa wanaonewa na makaburu walisema ni haki ya weupe wachache kule SA kuendelea kufaidi pesa za waafrika na rasilimali zao. Who are they to determine the distination of this country? The can go to hell and when they come back we will be in a better position.
 
Wao wanavyo sema tuheshimu sheria za kimataifa tulizo ziridhia. Sasa waweza kuacha hizo bilioni 94 , na ukanyimwa misaada ya trillion 1, kipi bora ? mie naona tulipe tu nakubaliana nao

There z typical circumstance where 1 worthy more than 1000000
 
Tunaweza kudurufu kutoka Kenya, turuhusu Bunge letu lipige kura kujitoa kwenye hiyo sheria tuliyoridhia, kisha tuingia uwanjani tuishughulikie hiyo Dowans humu humu ndani. Siyo kila linalosemwa na hawa wajomba (wafadhili) ni lazima tulitekeleze hata kama lina uendawazimu ndani. NO PLEASE
 
Rubbish Brain go and ask those humps to pay on behalf of all Tanzanians- yaani always unakuja na kichefucheku manina zako huoni kama we ni full mgese? so kama wamekubali hao mabalozi ndo iwe nini?
hatulipi nenda kaseme Easymutant amesema hatulipi Dowans
 
Mabalozi wanatuamulia kama nani. Tanzania ni nchi yetu hawakubaliani na wananchi waanze kwani lazima kupewa hiyo misaada. Misaada yenyewe inaishia kwenye mifuko binafsi kwa hivi hakuna tofauti hata kama wataacha kutupa hiyo misaada. Wasituzingue bana.Balozi balozi my ting ting
 
Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini wakiwamo wa Jumuiya ya Ulaya (EU) wametoa maoni yao na kuafiki kuwa DOWANS walipwe, kwani hukumu hiyo imetolewa na mahakama ambayo wao wanaiheshimu ya ICC.

Kutokana na hivyo basi, wameitaka Tanzania kuheshimu mikataba ya kimataifa ambayo wameiridhia, ili kuimarisha utiifu wa sheria za kimataifa na kuwajibika nazo. Wametoa madhara ya kutofuata sheria za kimataifa ni pamoja na nchi wahisani kukosa imani na serikali na hivyo kupunguza au kuondoa misaada yao ili kuishinikiza serikali kufuata misingi ya utawala bora ya kimataifa.

Hawa Mabalozi ina maana hawaoni hatari iliyopo baada ya dowans kulipwa? Au ndio wanataka yaliyo tokea huko tunisia ya tupate? Hivi baada ya serikali kulipa Dowans itawezaje kwa mfano kuwaambia wafanyakazi wake kuwa haina uwezo wa kuwaongeza mishahara, nk. Sio kila kitu wanachoshauri hawa mabwana ni chakututakia mema inawezekana kabisa wana agenda yao ya siri. Katika mambo yanayo weza kulipua nchi hii ni kulipwa hawa dowans ngoja tusubiri na tutaona.
 
Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini wakiwamo wa Jumuiya ya Ulaya (EU) wametoa maoni yao na kuafiki kuwa DOWANS walipwe, kwani hukumu hiyo imetolewa na mahakama ambayo wao wanaiheshimu ya ICC.

Kutokana na hivyo basi, wameitaka Tanzania kuheshimu mikataba ya kimataifa ambayo wameiridhia, ili kuimarisha utiifu wa sheria za kimataifa na kuwajibika nazo. Wametoa madhara ya kutofuata sheria za kimataifa ni pamoja na nchi wahisani kukosa imani na serikali na hivyo kupunguza au kuondoa misaada yao ili kuishinikiza serikali kufuata misingi ya utawala bora ya kimataifa.

Source please!!
 
Kwahiyo kumbe nchi hisani kukosa imani kwa serikali ni muhimu kuliko wenye nchi kukosa imani na serikali??Hii nchi ikiwaka moto leo kwa wananchi kukosa imani na serikali yao ndo wataona raha ehh?Na kuihisani juu!Embu wachape mwendo huko...na wewe -Geniusbrain acha kuandika pumba!Tanzania ni ya Watanzania na sio ya wahisani...!
 
Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini wakiwamo wa Jumuiya ya Ulaya (EU) wametoa maoni yao na kuafiki kuwa DOWANS walipwe, kwani hukumu hiyo imetolewa na mahakama ambayo wao wanaiheshimu ya ICC.

Kutokana na hivyo basi, wameitaka Tanzania kuheshimu mikataba ya kimataifa ambayo wameiridhia, ili kuimarisha utiifu wa sheria za kimataifa na kuwajibika nazo. Wametoa madhara ya kutofuata sheria za kimataifa ni pamoja na nchi wahisani kukosa imani na serikali na hivyo kupunguza au kuondoa misaada yao ili kuishinikiza serikali kufuata misingi ya utawala bora ya kimataifa.

Source of this information please? Hii post ingeletwa na mtu mwingine labda nisingeuliza lakini GeniusBrain? Tupe chanzo cha hii habari!!!

Tiba
 
Ama kweli wahenga walisema: Wajinga ndio waliwao. Huyu GeniusBrain ameleta hii mada kama tetesi alafu hapo hapo anasema imechapishwa euronet ambako mpaka sasa hakuna ambae ameiona. Dah!
 
Back
Top Bottom