Tetesi: Mabalozi wakubali DOWANS kulipwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tetesi: Mabalozi wakubali DOWANS kulipwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by GeniusBrain, Jan 21, 2011.

 1. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #1
  Jan 21, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini wakiwamo wa Jumuiya ya Ulaya (EU) wametoa maoni yao na kuafiki kuwa DOWANS walipwe, kwani hukumu hiyo imetolewa na mahakama ambayo wao wanaiheshimu ya ICC.

  Kutokana na hivyo basi, wameitaka Tanzania kuheshimu mikataba ya kimataifa ambayo wameiridhia, ili kuimarisha utiifu wa sheria za kimataifa na kuwajibika nazo. Wametoa madhara ya kutofuata sheria za kimataifa ni pamoja na nchi wahisani kukosa imani na serikali na hivyo kupunguza au kuondoa misaada yao ili kuishinikiza serikali kufuata misingi ya utawala bora ya kimataifa.
   
 2. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #2
  Jan 21, 2011
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,007
  Trophy Points: 280
  Hao mabalozi wanataka kumwingiza JK mkenge, akilipa hizo pesa na misaada yote kwisney, hao jamaa wana intelejensia kali sana na wanajua mchezo mzima ulivyofanyika
   
 3. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #3
  Jan 21, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  CCM tukutane njia panda katika hili!
   
 4. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #4
  Jan 21, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  As usual, habari kutoka hewani hewani! Kwa hiyo wakisema mabalozi na sisi watanzania tuone ni halali tu si ndio? As if hao mabalozi wanatuwakilisha watanzania.
   
 5. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #5
  Jan 21, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Wao wanavyo sema tuheshimu sheria za kimataifa tulizo ziridhia. Sasa waweza kuacha hizo bilioni 94 , na ukanyimwa misaada ya trillion 1, kipi bora ? mie naona tulipe tu nakubaliana nao
   
 6. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #6
  Jan 21, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Lazima tufuate sheria za kimataifa. Hii mahakama iliyo toa hukumu ina heshimika dunia nzima
   
 7. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #7
  Jan 21, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Februari, habari za siku nyingi??
   
 8. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #8
  Jan 21, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  ndio madhara ya kutegemea wajomba! Jamani tutaheshimu mikataba ya kimataifa isiyo na hila! Mbona mkataba wa 1929 kuhusu maji ya mto Nile tumeukataa na hatujaathirika chochote wandugu? Umefika wakati wa kuacha kutegemea misaada!
   
 9. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #9
  Jan 21, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Source Please
   
 10. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #10
  Jan 21, 2011
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  SOURCE YA HABARI YAKO NI IPI? NA NI BALOZI NGAPI ZIMESEMA HIVYO.
  NCHI HAINGOZWI NA MABALOZI INAONGOZWA NA WENYE NCHI.
  Na hawa mabalozi hawatakiwi kuingilia mambo ya ndani ya nchi.
   
 11. Naloli

  Naloli JF-Expert Member

  #11
  Jan 21, 2011
  Joined: Aug 26, 2010
  Messages: 416
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Tanzania ni nchi uhuru, na moja ya msingi wa uhuru ni kujiamulia mambo yenu wenyewe hivyo hatuwezi kuamuriwa na mabalozi wa nchi wahisani nani tumlipe na nani tusimlipe. kama wao ni waungwana wangeshinikiza au wangetutaka tuwalipe wazee wa iliyokuwa jumuia ya East Africa fedha zao na si kuzungumzia suala la DOWANS, eti kisa wanaiheshimu ICC. Mikataba ya kimataifa sharti iheshimiwe lakini pale tu haki inapotendeka pande zote mbili kwa swala la DOWANS sisi tumeumizwa(kama watz) maana serikali inaonekana kabisa iko upande wa DOWANS sasa ilitegemewa vp kesi hiyo itoe haki kwa watz wakati serikali na DOWANS ni kitu kimoja na wamepeleka kesi ICC ili kujustify malipo ya DOWANS ionekane ni mahakam ya kimataifa ndio imeamua na si serikali.
  kama watanzania ni lazima tuipiganie haki yetu, hata kama tutaikosa lakini DUNIA ijue SERIKALI yetu na MAFISADI wanatuumiza yaani bado tupo ktk ukoloni chini ya wakoloni wa afrika na wahindi/waarabu (MAFISADI)
  Kuli hiyo ingetolewa na mabalozi wa nyumba kumi ingenistua lakini mabalozi wa nchi zilizo na ubalozi tanzania ainistui maana sakata la DOWANS linaonyesha wazi UPUMBAVU WETU WATANZANIA sasa nani atusaidie ili tusilipe malipo ya UPUMBAVU wetu. Mabalozi wanahaki ya kusema tulipe maana wanajua mchawi tunamjua na tuanmlea hivyo acha atutafunie watoto wetu.
   
 12. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #12
  Jan 21, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Lakini tatizo ni kwamba hamkuwapa TAARIFA ZOTE MUHIMU hivyo wakafanya maamuzi based on Taarifa ambazo Balozi Maajar wa Rex Attorney aliwapa ilhali Watanzania tunajua ukweli wote.

  Isitoshe, kitendo cha nyinyi kukibeba Mahakama hiyo ICC mkakileta CHUMBANI KWENU kabisa pale Movenpick na kuwajulia vema mitumbo yao, haki isingeweza kutendeka.

  Mwisho, tumlipe Dowans tunamkabidhi hasa NANI CHEKI mbona mnageuka bubu hata Mzee kule CCM makao makuu kweli hana taarifa hizi??
   
 13. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #13
  Jan 21, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Nimefurahi mabalozi wamekubali Dowans ilipwe. Kwa vile wanaonekana kujali sana sheria ya kimataifa kuliko maadili ya malipo haya naomba watulipie deni lote hili. Please.
   
 14. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #14
  Jan 21, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  source please otherwise UDAKU
   
 15. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #15
  Jan 21, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  MM Una source ya tamko la mabalozi? naona unakubali kirahisi
   
 16. bluetooth

  bluetooth JF-Expert Member

  #16
  Jan 21, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 3,936
  Likes Received: 673
  Trophy Points: 280
  source please please
   
 17. m

  mapambano JF-Expert Member

  #17
  Jan 21, 2011
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 535
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndio matatizo ya kutembeza bakuli
   
 18. 3D.

  3D. JF-Expert Member

  #18
  Jan 21, 2011
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 1,022
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kutokana na misimamo unayoionesha hapa (inaweza kuwa sahihi), inatufanya wengine tujiulize source ya information yako ni ipi kwa kuwa wewe ndiye uliyeweka post hii, isije ikawa umetunnga tu halafu unaanza ku-engage watu into arguments. Hili ni tatizo sana hapa JF.
   
 19. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #19
  Jan 21, 2011
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Kwani hawa ni akina nani katika hili? na wakikubali wao ndio kwamba Tanzania inacheza ngoma za mabalozi.

  Si dhani kama ndivyo! Hapo kale mwalimu aliwafukuza ubalozi wa ujerumani na makarai yao wakati wanajenga Nkruma hall kwa kutaka kuingilia mambo yasiyo wahusu.
  Watupishe kule !
   
 20. Sita Sita

  Sita Sita JF-Expert Member

  #20
  Jan 21, 2011
  Joined: Aug 25, 2008
  Messages: 1,196
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  I wish ungesema source ya Habari yako;

  Mabalozi wanatupima uwezo wetu wa kifedha,
  We will be questioned kama tunaweza kulipa DOWANS alafu hatuwezi kujenga shule na zahanati kwa ajili ya wananchi

  Last week nimeona kwenye Blogu Mhe. WM akipokea mkopo wa US $ 92M kwa ajili ya kusupport KILIMO KWANZA
  Sasa kama hiyo ya KILIMO KWANZA tunaenda kukopa, ya DOWANS tunatoa wapi????

  Hapo tunatakiwa tusilipe (Offcourse ni hela za kila Mtanzania)
  WOTE KWA PAMOJA TUSIUNGE MKONO HOJA YA KULIPA DOWANS
   
Loading...