Tarehe 4 April, jamaa yangu mmoja (siyo mwanafamilia), ambaye ni rafiki na alisoma na Mchimbaji aliniambia kuwa siku 3 kabla alikuwa na mazungumzo na Mchimbaji. Wakati wa mazungumzo yao, huyu jamaa yangu alimwuliza kuwa kutokana na TAL kuanza kutoa elimu kwa wananchi, na watu wengi kuonekana wanaunga mkono No REFORM no ELECTION, je watafanya reforms zozote? Mchimbaji akamjibu kuwa, haiwezekani kabisa kufanya reforms zozote, kwa sababu wakifanya reforms ambazo TAL anataka, ni sawa na kutangaza kuwa wameondoka rasmi kutawala nchi.
Yule jamaa yangu akamwuliza kuwa kwa vile wamefanya mema mengi kama ambavyo huwa wanatangaza, kwa nini kufanya reforms iwe ni ticket ya kuondoka madarakani. Mchimbaji akamjibu kuwa, 'kumbe wewe huelewi? sisi huyu wa kwetu kwanza ni mgonjwa, pili kutoka upande ule na yale mambo yaliyotokea, kama yale ya bandari, tayari ni disadvantage, lakini jingine kubwa hana uwezo mzuri wa kujieleza, sasa ukifanya na reforms, unaona kuna uwezekano wa kushindana na TAL?'.
Yule jamaa yangu akamwuliza, 'sasa kama ni hivyo, na TAL anazidi kuwafungua watu, na wengi kuonekana kumwunga mkono, mtafanyaje kupambana naye?'. Mchimbaji akamjibu, ndiyo maana naenda Songea. Kule naenda kuelekeza vyombo vya dola. Pale mjini Songea hatafanya mkutano. Tukimdhibiti yeye, na kila atakayeinuka, tukaweza kuongeza nguvu na kuwasaidia wale wanaopingana naye ndani ya chama chake, tutafanikiwa kuwafanya wakubali kushiriki uchaguzi bila mabadiliko au wasusie, lakini wasizuie. Wakisusia itakuwa vizuri zaidi.
Ile tarehe 4, yule ndugu yangu alivyonisimlia, nilipuuza. Lakini baada ya leo TAL kukamatwa kabla ya mkutano wa Songea mjini, na hivyo TAL hataweza kuhutubia huo mkutano kama Mchimbaji alivyonena, nimeanza kuamini yale niliyoambiwa, kumbe ulikuwa ndiyo ukweli wenyewe.
Mambo muhimu niliyoyapata katika conversation ya hawa wawili:
1) Mgombea mmojawapo wa nafasi ya juu ni mgonjwa, huenda asiweze kuzunguka nchi nzima.
2) TAL inajulikana kuwa kwenye mazingira huru, wagombea wengine hawaambulii chochote
3) Mbinu pekee waliyobakiza dhidi ya NO REFORM NO ELECTION ni kuwakamata viongozi.
TUOMBE:
Mungu wetu muweza wa yote, tunaomba umjalie ulinzi wa pekee mtetezi wa haki za watu wako, Tundu Lisu. Tunaomba uwashangaze wale wafuasi wa ibilisi walio kinyume cha haki wanaokesha kupanga uovu dhidi ya wanaoitafuta haki. Mungu wa Ibrahim, Mungu wa Isaka, Mungu wa Yakobo, tunaomba mkono wako wenye nguvu uwafikie na uwaangamize wote walio kinyume cha watafutao haki katika Taifa hili la Tanzania. Tunaomba, hata wakipora haki kwaajili ya tamaa ya madaraka, ukawaoneshe kuwa walikuwa wajinga, sawa na yule mkulima aliyesema kuwa sasa amefanikiwa kupata mavuno mengi, kilichobakia ni kula na kunywa, nawe ukamwambia umpumbavu wewe kwa kuwa leo naihitaji roho yako. Kwaajili ya neno hilo, tunaomba, wote wanadhulumu haki ili wajitwalia madaraka kwa kulazimisha, wakaonekane wapumbavu kwa sababu kamwe hawatayafurahia wala kuyafaidi madaraka waliyoyapata kwa dhuluma. Tunayaleta maombi yetu kwako, kwa Jina la BABA, Tunayaleta maombi yetu kwako kwa jina la Mwana, Tunayaleta maombi yetu kwako, Kwa jina la Roho Mtakatifu, AMINA.
Kila anayetaka haki katika nchi yetu, baada ya kujitakasa kwa toba, asali sala hii au inayofanana na hii katika content kwa kadiri ya imani yake, kwa siku 10 mfululizo , Mungu wetu aliye wa haki, husikia sauti za watu wake, hakika atatenda kwa kadiri ya hekima yake.