MwanaHaki
R I P
- Oct 17, 2006
- 2,401
- 705
Takriban saa 9:05 alfajiri, tarehe 9 Aprili 2010, nikiwa ndani ya hoteli ya Aquiline iliyopo eneo la stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani, ghorofa ya 5, nimeshuhudia tetemeko dogo la ardhi, ambalo lilidumu kwa takriban sekunde 10.
Kwa makisio yangu yasiyo ya kitaalam, tetemeko hilo lilikuwa kwenye kipimo cha chini ya 1, kwenye kipimo cha Richter, hata hivyo lilikuwa la kutisha,
Wakati nikiwa ninafanya shughuli kwenye laptop yangu huku nikijiandaa kulala ili kujipumzisha, ghafla kitanda kilianza kucheza, kwenda kushoto na kulia, mara tatu hadi nne, kwa muda wa takriban sekunde 10.
Kwanza nilidhani ninaota, lakini nikatazama kando yangu, kwenye glasi kulikuwa na kinywaji changu - Red Bull - nikaona glasi inayo inatetemeka huku kimiminika nacho kikionekana kutikisika.
Kutazama mezani ambako kuna chupa ya after shave, nayo nikaona hali ni ile ile.
Nilipatwa na mstuko almanusura nianguke chini, haraka nichachukua handset zangu na ufunguo, nikaacha kila kitu kitandani, nikavaa viatu bila soksi, huku nikipatwa na kiwewe.
Mbio nikashuka hadi chini, kumbe kuna baadhi ya wageni hapa hotelini, wengine wakiwa ni wenzangu tuliokuja pamoja kwenye mkutano, nao walikuwa hawajalala.
Baada ya kupoa kidogo - BADO NINA WASIWASI - tukaamua kurudi vyumbani kila mmoja kwa wakati wake, HATUKUPANDA LIFT!
Hii imetokea kweli. Inatisha!
SWALI: Majengo ya ghorofa yanayojengwa hapa nchini yana viwango vinavyozingatia uimara dhidi ya matetemeko ya ardhi, kiasi kwamba, MUNGU EPUSHA MBALI, tetemeko likitokea, maafa yasiwe makubwa?
Asanteni.
./Mwana wa Haki - Jijini Arusha