Tetemeko la ardhi latokea Dodoma, Singida

HIMARS

JF-Expert Member
Jan 23, 2012
69,369
94,554
Taarifa
20230217_165811.jpg

View attachment 2520526


GST inapenda kuutangazia umma kwamba kumekuwa na matukio ya matetemeko ya ardhi katika maeneo ya wilaya ya Manyoni kwenye mpaka kati ya Mkoa wa Singida na Dodoma yakiwa na ukubwa wa 4.3 na 4.9 katika kipimo cha Richter kama yalivyoainishwa kwenye jedwali hapa chini:

Tarehe ya tukioMuda wa tukio
ukubwa​
Mahali lilipotokea
Latitudo​
Longitudo​
Eneo
16/2/202312:13 Jioni
4.9​
-50 25' 47"340 57' 35"Makuru
17/2/20231:45 Asubuhi
4.3​
-50 27' 35"340 57' 35"Makuru
17/2/20236:26 Mchana
4.9​
-50 37 7.4"350 13' 156"Zuboru
Matukio hayo yalisikika katika maeneo ya mkoa wa Dodoma na Singida. Hata hivyo, pamoja na matetemeko hayo kusababsha taharuki kubwa kwa wakazi wa Jiji la Dodoma na maeneo ya jirani, GST haijapata taarifa zozote za kutokea kwa madhara kutokana na matetemeko hayo.

Ikumbukwe kwamba mikoa ya Dodoma na Singida imepitiwa na ukanda wa bonde la ufa la Afrika Mashariki mkondo wa mashariki. Mikoa mingine katika mkondo wa mashariki ni Manyara, Arusha, Mara, Iringa na Njombe ambapo mkondo wa magharibi una mikoa ya Kagera, Kigoma, Katavi Rukwa, Songwe, Mbeya na Ruvuma. Maeneo ya ukanda wa bonde la ufa kwa kawaida ni maeneo tete ya mabadilko ya kijiolojia ambayo hukumbwa na matetemeko ya ardhi na milipuko ya volkano.

Mateteneko ya adhi hutokana na nguvu za asili ambazo husababisha rngandamizo katika ya miamba. Hadi hivi sasa hakujagunduliwa teknolojia ya kuweza kutabiri kutokea kwa tetemeko la ardhi, hivyo GST inatoa wito kwa wananchi kuendelea kuchukua tahadhari muda Wote kama ambavyo imekuwa ikishauri ili kuepuka madhara Yanayoweza kusababishwa na majanga asili ya Jiolojia ikiwemo matetemeko ya ardhi. Mojawapo ya hatua za tahadhari dhidi ya tetemeko la ardhi ni kama zifuatazo:

Kabla ya tukio; Kujenga nyumba bora na imara kwa kuzingatia viwango halisi vya ujenzi, kupata ushauri wa kitaalamu wa aina ya majengo yanayofaa kujengwa kulingana na jiolojla ya eneo husika, kuepuka ujenzi wa nyumba katika miinuko yenye kuambatana na mawe/miamba na mipasuko ya miamba.

Wakati wa tukio; Kama uko nje ya Jengo unashauriwa kubaki nje. simama mahali pa wazi mbali na majengo marefu, mti mirefu, nguzo na nyaya za na ujikinge kichwani kadri inavyowezekana; endapo litatokea ukiwa ndani ya nyumba unashauriwa kubaki ndani na ukae sehemu salama kama vile chini ya uvungu wa meza imara, kitanda, ama simama kwenye makutano ya na makabati ya vitabu, vyombo au fenicha ili kuepuka kuangukiwa na vitu hivyo; usitangetange muda mrefu kutafuta mahali salama kwa sababu tetemeko la ardhi hutokea ghafla na huchukua muda mfupi Sana; jihadhari na moto kwakuwa tetemeko la ardhi linaweza kusababisha matukio ya moto kwa kutokea hitilafu ya umeme au kupasuka kwa rnabomba ya gesi; usiendeshe chombo cha moto wakati wa tukio tetemeko; toa taarifa kwa uongozi wa husika au kwa vyombo vya uokoaji ili kupata msaada zaidi;

Baada ya tukio: kagua ili kuhakikisha kama hayakupata madhara na kama ikilazimu unashauriwa kuwaita wataalamu wa kufanya ukaguzi kuona kanu ni salama wa majengo hayo kuendelea kutumika.
 
Nilihisi Mayele anamfundisha Musonda kutetema kumbe ni tetemeko

Limenikuta juu ya kifuacha li jimama, kwanini lisinikumbatie hadi nikamwaga.
Jua na joto lote hili mzee, au jimama lilikupiga tozo la maana?

Maana papara na kisirani cha kufanya mapenzi saazingine husababishwa na kuhonga pakubwa.
 
Back
Top Bottom