Tetemeko dogo la Ardhi lashuhudiwa Arusha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tetemeko dogo la Ardhi lashuhudiwa Arusha

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MwanaHaki, Apr 9, 2010.

 1. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #1
  Apr 9, 2010
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Takriban saa 9:05 alfajiri, tarehe 9 Aprili 2010, nikiwa ndani ya hoteli ya Aquiline iliyopo eneo la stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani, ghorofa ya 5, nimeshuhudia tetemeko dogo la ardhi, ambalo lilidumu kwa takriban sekunde 10.

  Kwa makisio yangu yasiyo ya kitaalam, tetemeko hilo lilikuwa kwenye kipimo cha chini ya 1, kwenye kipimo cha Richter, hata hivyo lilikuwa la kutisha,

  Wakati nikiwa ninafanya shughuli kwenye laptop yangu huku nikijiandaa kulala ili kujipumzisha, ghafla kitanda kilianza kucheza, kwenda kushoto na kulia, mara tatu hadi nne, kwa muda wa takriban sekunde 10.

  Kwanza nilidhani ninaota, lakini nikatazama kando yangu, kwenye glasi kulikuwa na kinywaji changu - Red Bull - nikaona glasi inayo inatetemeka huku kimiminika nacho kikionekana kutikisika.

  Kutazama mezani ambako kuna chupa ya after shave, nayo nikaona hali ni ile ile.

  Nilipatwa na mstuko almanusura nianguke chini, haraka nichachukua handset zangu na ufunguo, nikaacha kila kitu kitandani, nikavaa viatu bila soksi, huku nikipatwa na kiwewe.

  Mbio nikashuka hadi chini, kumbe kuna baadhi ya wageni hapa hotelini, wengine wakiwa ni wenzangu tuliokuja pamoja kwenye mkutano, nao walikuwa hawajalala.

  Baada ya kupoa kidogo - BADO NINA WASIWASI - tukaamua kurudi vyumbani kila mmoja kwa wakati wake, HATUKUPANDA LIFT!

  Hii imetokea kweli. Inatisha!

  SWALI: Majengo ya ghorofa yanayojengwa hapa nchini yana viwango vinavyozingatia uimara dhidi ya matetemeko ya ardhi, kiasi kwamba, MUNGU EPUSHA MBALI, tetemeko likitokea, maafa yasiwe makubwa?

  Asanteni.

  ./Mwana wa Haki - Jijini Arusha
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Apr 9, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,814
  Likes Received: 83,212
  Trophy Points: 280
 3. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #3
  Apr 9, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Pole Sana Mkuu kwa hilo tetemeko lililotokea Arusha huku kwetu Ughaibuni kama litatokea tetemeko la ardhi kwa Takriban sekunde 10. basi ukae ukijuwa majumba mengi ya magorofa yataanguka na watu wengi kupoteza maisha huku huwa linatokea kwa Takriban Sekunde 4 au 5 au 6 au limezidi sana basi itakuwa Sekunde 8 na hivyo hivyo linauwa Watu kwa wengi sana pole Mkuu na watu wote wa mji wa Arusha nawapa pole zangu.
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  Apr 9, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  well.. kuna makala nimeandika "Juu ya kujiandaa na tetemeko la ardhi".. ambako ninahofia zaidi ni Rukwa...
   
 5. M

  Magezi JF-Expert Member

  #5
  Apr 9, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Swali ni je Serikali zetu tanzania toka enzi wanahimiza lolote juu ya ujenzi wa majumba yanayohimili tetemeko??
   
 6. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #6
  Apr 9, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  sijawahi kusikia hiyo mbiu ya kujenga nyumba za kuweza kuhimili tetemeko... na kwa staili ya ujenzi wetu, ma-contractor feki na chinese kila sehemu sidhani kama tunajiandaa na matetemeko
   
 7. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #7
  Apr 9, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Pole sana mkuu kwa usumbuifu. Nadhani huko kwenye maeneo ya bonde la ufa hali inaweza kuwa mbaya zaidi, zuri ni kuwa hakuna maghorofa kama hapo mjini
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Apr 9, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  mji kama wa mbeya unaweza kuwa leveled in second kama Port Au Prince.. na sijui kama watawala wenu magogoni wanampango wowote.. wa tahadhari au wanaombea tu..
   
 9. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #9
  Apr 9, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Hii ni taarifa ya jamaa wa US Geological Survey, inaelekea epicentre yake ilikuwa mbali kidogo na A town

  PRELIMINARY EARTHQUAKE REPORT ==  Region: TANZANIA
  Geographic coordinates: 4.106S, 35.305E
  Magnitude: 4.9 Mb
  Depth: 10 km
  Universal Time (UTC): 8 Apr 2010 23:57:41
  Time near the Epicenter: 9 Apr 2010 02:57:41
  Local standard time in your area: 9 Apr 2010 02:57:41

  Location with respect to nearby cities:
  171 km (106 miles) WSW (242 degrees) of Arusha, Tanzania
  233 km (145 miles) N (350 degrees) of Dodoma, Tanzania
  296 km (184 miles) ENE (70 degrees) of Tabora, Tanzania
  357 km (222 miles) SSW (208 degrees) of NAIROBI, Kenya
   
 10. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #10
  Apr 9, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  i know that feeling .................nishatikiswa sana na matetemeko na i never get used to the feeling.
  mungu aepushie mbali tetemeko kubwa Tanzania. sidhani kama kwenye miji yetu nyumba zinajengwa zikiwa earthquake conscious.
   
 11. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #11
  Apr 9, 2010
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Ni kweli, tetemeko limetokea A. town. labda wataalamu watatueleza kipimo chake, lakini lilitutisha sana. Mungu mkubwa hakukuwa na madhara.
   
 12. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #12
  Apr 9, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Mkuu Mwanakijiji, nimeishi Sumbawanga miaka ya themanini, kule ni balaa nakumbuka siku moja usiku km saa tano tulikuwa sebuleni tunapiga story nilikuwa very young wakati huo basi lilipita tetemeko la ardhi si mchezo jamani, inatisha kulikuwa na meza kubwa ya chakula, ilikuwa inaruka mpaka vitu vyote ilivyokuwa juu ya meza vikadondoka. wote tulikimbia nje ya nyumba, sasa imagine upo PPF tower pale gorofa ya 15 kule na ndo linatokea sasa
   
 13. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #13
  Apr 9, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  Hadi matetemeko yatokee na watz wafe ndo itaundwa kamati ya kuelimisha na kutunga sheria bungeni!
   
 14. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #14
  Apr 9, 2010
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145

  Kaka Mpita Njia

  Ingekuwa vizuri ukaweka link ya hiyo taarifa nzuri hapo juu ya USGS.

  Asante sana.

  Epicenter haikuwa karibu na Arusha, na Jiji zima limetikisika. Tena magnitude KUBWA. Naomba unipe link ili niandike article, niwapelekee wakatangaze, maana MEDIA za Bongo ZIMELALA DOROOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO!!

  ./Mwana wa Haki
   
Loading...