Test Your Earliest Memory: How Long Can You Remember?!.

Nilikuwa na miaka mitatu kuelekea minne hivi, nilikuwa nalia nataka nimuogeshe mdogo wangu na mimi. Binamu aliyekuwepo nyumbani alikuwa ananiambia njoo nikuoshe mdogo wangu kwa hiyo nilipopata mdogo na mimi nkataka nimuoshe.
 
Mnavyohadithia stori za chekechea mnanikumbusha huzuni yangu kuu kipindi hicho nina miaka 4mpaka 5 sijui niite bahati mbaya au nzuri
mimi sikusoma elimu ya awali mama yangu alikuwa ananifundisha mwenyewe nyumbani kusoma na kuandika kipindi hicho nina miaka 4 mpaka 5
nilikuwa natamani mnooo shule lakini mama alipinga akisema yeye ni mwalimu tosha atanifundisha mwenyewe nyumbani na
ilikuwa kila siku asubuhi lazima niwahi kuamka kuangalia watoto wanaokwenda shule hasa wale wa chekechea baada ya hapo nalia kutaka niende shule msimamo wa mama haukubadilika baada ya chai anaanza kunifundisha
nilipokuja kuanza la kwanza pindi nina miaka 7 hakuna siku niliyofurahi kama hiyo
 
Ni kweli memory ya binadamu ina uwezo mkubwa sana wa kuhifadhi vitu kwani kuna millions of neurones ambazo kwa mujibu wa Neuro Surgeons ni kwamba only 1% tu ndiyo imeshatumika pamoja na ugunduzi mkubwa wa kisayansi uliokwishafanyika!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums

Dah, umenipa changamoto hapo mkuu, hivi kila mtu anaweza kufikiri ameshatumia % ngapi kufanya cha maana katika maisha yake tangu azaliwe? Kuna mmoja amelinganisha huu uwezo sawa na MB,GB,TB- Hivi tunaweza kuwachambua viongozi wetu kwa kutumia hivi vigezo?
 
Kila mtu anaweza kukumbuka cd yake ilipokuwa empty
Mimi nakumbuka mwaka 1964 nikiwa mdogo sana naenda chekechea na sister
Nikichoka kutembea alikuwa ananibeba alikuwa mkubwa kwangu kwa miaka miwili
Mpaka mwalimu wangu namkumbuka sana
Ila sasa kumbuka uliofanya nao kazi miaka 10 iliyopita kama ulibadili kazi
Hapo ndio utajua kumbukumbu ni utotoni tu

Saa hizi ukiniambia jina lako leo
Kesho nimelisahau
 
Nakumbuka nkiwa mdogo sana na miaka 3, nilimng'ania kaka yangu niende nae Shamba, nikiwa shamba nkabanwa na Haja akanichimbia shimo karibu na shina la maindi nkakata gogo pale akafukia akaniambia ile ni mbolea hivyo indi litastawi sana basi ikawa kila safari ya shamba nataka niende kuliangalia indi langu, kabla Ya mavuno nikatenganishwa nae kwa Miaka minne ila lile indi lilinikaa sana kichwan na nilipoonana nae nikamkumbusha....
 
Ahhaaaahahahahaha
 
Ahsante kwa mada nzuri mzee pasco @@pascal mayala mayala japo ni ya kitambo kiasi.
Naweza recall kumbukumbu za muda mrefu kupitia MUZIKI.
Kwa mfano enzi za utoto wetu, familia yetu ilikuwa ni ya kidini sana. Baba alikuwa na cassette aliinunua 1992 so me nimezaliwa nimeikuta. So alikuwa ananunua kanda za wanamuziki mbalimbali hasa kwaya za kikatoliki, kilutherani, na nyimbo za dansi kama za kina mzee rojer, mwinjuma muumini nk katapila, na za kusifia juhudi za Nyerere.
So kila nikisikia hata leo baadhi ya hizo nyimbo basi hunikumbusha Family memories kibao.

Kuna kanda fulani hivi imeitwa na mateeneger wa south africa alinunua mzee dah ilikuwa kwa kizulu mixer kiingereza basi nilikuwa naipenda mpka leo. Niihangaika mtandaoni nipate nyimbo zake in digital format nikafanikiwa kupata chache lkn hunipeleka so far kimawazo.
 
Nakumbuka nikiwa na 4yrs, nilitumia mabox na takataka nyingine nikajenga kitu nilichoita nyumba!, Cha ajabu nikaingiza kiwili wili huku miguu ikiwa nje nikauchapa usingizi wa kutosha! Mama na ndg wengine walihangaika kunitafuta lkn walikuja kuniona baada ya masaa mengi kupita nikiwa bado nauchapa usingizi!
 
Ahsante kwa mada nzuri mzee pasco @@pascal mayala mayala japo ni ya kitambo kiasi.
Naweza recall kumbukumbu za muda mrefu kupitia MUZIKI.
Kwa mfano enzi za utoto wetu, familia yetu ilikuwa ni ya kidini sana. Baba alikuwa na cassette aliinunua 1992 so me nimezaliwa nimeikuta. So alikuwa ananunua kanda za wanamuziki mbalimbali hasa kwaya za kikatoliki, kilutherani, na nyimbo za dansi kama za kina mzee rojer, mwinjuma muumini nk katapila, na za kusifia juhudi za Nyerere.
So kila nikisikia hata leo baadhi ya hizo nyimbo basi hunikumbusha Family memories kibao.

Kuna kanda fulani hivi imeitwa na mateeneger wa south africa alinunua mzee dah ilikuwa kwa kizulu mixer kiingereza basi nilikuwa naipenda mpka leo. Niihangaika mtandaoni nipate nyimbo zake in digital format nikafanikiwa kupata chache lkn hunipeleka so far kimawazo.
Mkuu nazitafuta sana hizo nyimbo za hao Wasouth,kama utaweza naomba uorodheshe majina ya hizo nyimbo hapa nizitafute

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanabodi.

Kumbukumbu ni moja ya vitu ambavyo binadamu anaishi navyo milele hadi kufa navyo!. Ubongo ni kama computer hard disc, na uwezo wa kuhifadhi ni kama computer memory, kadri unavyohifadhi memory nyingi, ndivyo unavyoongeza space ya hard disc yako, wengine ni KB, wengine, MB, wengine ni GB na hata TB, jee wewe unaweza kujijua uko kundi gani?.

Naomba ujikumbushe the earliest thing kilichokutokea udogoni, mpaka leo unakikumbuka, ulipokuja kuhadithiwa ulikuwa na umri gani wakati huo unaweza kushangaa!.

Mimi wakati nikiwa mdogo kabisa, nikiwa naishi Arusha, mbio za mwenge zilipita nje kwetu!. By that time nilikuwa urefu wa buti ya jeshi, kwa sababu hapo barabarani nilipo simama, buti ilikuwa ndio usawa wa macho yangu!. Tukaja kuhama Arusha na kuhamia Tanga, nikiwa mkubwa naonyeshwa picha zangu tukiwa Arusha, naambia tulihama nikiwa 3 years, na wakati tunahama, mwenge ulikuwa haujapita, hivyo nilipoziona mbio za mwenge I was two years na mpaka leo nakumbuka!.

Nilianza Nursery shule ya St. Peters Kindergarten ya Tanga nikiwa 4 years. Mpaka leo, more than 30 years back, nakumbuka baadhi ya majina ya wanafunzi wa darasani kwangu na miongoni mwao ni Alex Shaba, David Naburi, Allen Semu, Irene Minja, Jane Mutayoba, Robert Kilala na Ana Kilala!. Jee wewe unaweza kuwakumbuka baadhi ya wanafunzi mliosoma nao vidudu?.

Nikiwa nursery ndio mara yangu ya kwanza kuvaa shati jeupe, suruali nyeusi, soksi nyeupe na viatu vyeusi!, kabla ya hapo ni raba na ndala tuu. Nilinunuliwa nguo hizi ili kucheza mchezo wa kuigiza mimi nikiwa ndio mfalme!.

Kitu cha ajabu, nimemaliza Chuo juzi juzi, kuna watu nakutana nao mtaani tunasalimiana vizuri, namuomba anikumbushe, ananiambia tulikuwa class moja Chuo!. Yaani wale wazamani ninawakumbuka, hawa wa sasa siwakumbuki!. Nilipojiuliza nikakuta hard dis itakuwa imejaa hivyo it can take no more!. Huyo Robert Kilala na Jene Kilala, baba yao alikuwa ana pikipiki, anawaleta wote wawili wamepakizwa mbele kwenye pikipiki, hivyo nikawa naishangalia sana pikipiki nikitamani na mimi kupandishwa!. Watoto wengine wakiletwa na magari, mimi kwetu hatukuwa na gari, napelekwa shule na dada akiitwa Marrita (Martha), sometimes nikifika shule, siingii kwanza darasani ili kuona pikipiki, kumbe siku ingine wanakuwa wamewahi zaidi na mimi nikiwakuta, I feel sorry, I've missed the fun!. Baadae nilipokuja kuwa mtu mzima I was mad about bikes!.

Jee wewe unakumbuka nini enzi za udogoni kabisa?!.

Remembering those good old days, makes you feel good!.

Feel Good!.

Pasco
Kwa upande wangu, nilikuwa mkutubi nilipokuwa shule ya msingi na wanafunzi wenzangu wakija kuazima vitabu maktaba nilikuwa siandiki majina yao, lakini nilijua nani kaazima kitabu gani na anatakiwa arudishe lini. Pia darasani mwalimu akifundisha nilikuwa nasoma biblia chini ya dawati (maana yalikuwa yale yenye nafasi ya kuweka madaftari au vitabu chini) au rozari, lakini tukifanya mtihani nilikuwa nakuwa wa pili. Kwa uzoefu wangu, kadiri muda unavyoenda ndivyo ninavyokumbuka vizuri mambo ya zamani na kwa kawaida nikifahamu jambo huwa nakuwa na kumbukumbu nzuri almost ku'reproduce' kilichoandikwa. Enzi hizo kulikuwa na kitabu cha Kiingereza chenye simulizi la 'Mkisi crosses lake Nyasa' hii hadithi niliijua yote 'verbatim' pamoja na ile ya Ziwa Victoria 'Omusoke twahwelela'. Ni ajabu sana!
 
Wa shule ya msingi niliowasahau majina yao watu kumi tu kwenye darasa lililoķuwa na wanafunzi sabini na tisa ila sec wa O na A level niwakumbukao hawazidi watu kumi!
Nalog off
 
Ilikuwa na miaka 3.nilimuona bibi jirani yangu ana mguu wa mtu chumbani kwake... ... Mpaka leo sisahau hiyo kitu...
 
Kumbukumbu ninazo nyingi kiasi nadhani toka nikiwa na miaka 2 hadi mi 3 hivi...siku moja tunacheza na mwenzangu kwenye sebule hivi,ni kama tulitaka kuchukua kitu fulani kwenye gunia lililojaa mkaa kama nusu hivi,kabla ya kulifikia tukamuona nyoka mkubwa kama mweusi hivi,akainua kichwa,tukakimbia kumuita mama mdogo,akamtoa kumvutia nje na akamuua.Yule mama mdogo alikuwa haogopagi nyoka kabisa,mazingira yale yalikuwa na nyoka wengi na matukio machache ninayokumbuka kuhusu nyoka yeye ndo alikua akiwashughulikia.Nadhani matukio yale yalinijengea kuwaogopa nyoka sana mpaka karibuni woga umepungua kiasi kikubwa.
 
Wanabodi.

Kumbukumbu ni moja ya vitu ambavyo binadamu anaishi navyo milele hadi kufa navyo!. Ubongo ni kama computer hard disc, na uwezo wa kuhifadhi ni kama computer memory, kadri unavyohifadhi memory nyingi, ndivyo unavyoongeza space ya hard disc yako, wengine ni KB, wengine, MB, wengine ni GB na hata TB, jee wewe unaweza kujijua uko kundi gani?.

Naomba ujikumbushe the earliest thing kilichokutokea udogoni, mpaka leo unakikumbuka, ulipokuja kuhadithiwa ulikuwa na umri gani wakati huo unaweza kushangaa!.

Mimi wakati nikiwa mdogo kabisa, nikiwa naishi Arusha, mbio za mwenge zilipita nje kwetu!. By that time nilikuwa urefu wa buti ya jeshi, kwa sababu hapo barabarani nilipo simama, buti ilikuwa ndio usawa wa macho yangu!. Tukaja kuhama Arusha na kuhamia Tanga, nikiwa mkubwa naonyeshwa picha zangu tukiwa Arusha, naambia tulihama nikiwa 3 years, na wakati tunahama, mwenge ulikuwa haujapita, hivyo nilipoziona mbio za mwenge I was two years na mpaka leo nakumbuka!.

Nilianza Nursery shule ya St. Peters Kindergarten ya Tanga nikiwa 4 years. Mpaka leo, more than 30 years back, nakumbuka baadhi ya majina ya wanafunzi wa darasani kwangu na miongoni mwao ni Alex Shaba, David Naburi, Allen Semu, Irene Minja, Jane Mutayoba, Robert Kilala na Ana Kilala!. Jee wewe unaweza kuwakumbuka baadhi ya wanafunzi mliosoma nao vidudu?.

Nikiwa nursery ndio mara yangu ya kwanza kuvaa shati jeupe, suruali nyeusi, soksi nyeupe na viatu vyeusi!, kabla ya hapo ni raba na ndala tuu. Nilinunuliwa nguo hizi ili kucheza mchezo wa kuigiza mimi nikiwa ndio mfalme!.

Kitu cha ajabu, nimemaliza Chuo juzi juzi, kuna watu nakutana nao mtaani tunasalimiana vizuri, namuomba anikumbushe, ananiambia tulikuwa class moja Chuo!. Yaani wale wazamani ninawakumbuka, hawa wa sasa siwakumbuki!. Nilipojiuliza nikakuta hard dis itakuwa imejaa hivyo it can take no more!. Huyo Robert Kilala na Jene Kilala, baba yao alikuwa ana pikipiki, anawaleta wote wawili wamepakizwa mbele kwenye pikipiki, hivyo nikawa naishangalia sana pikipiki nikitamani na mimi kupandishwa!. Watoto wengine wakiletwa na magari, mimi kwetu hatukuwa na gari, napelekwa shule na dada akiitwa Marrita (Martha), sometimes nikifika shule, siingii kwanza darasani ili kuona pikipiki, kumbe siku ingine wanakuwa wamewahi zaidi na mimi nikiwakuta, I feel sorry, I've missed the fun!. Baadae nilipokuja kuwa mtu mzima I was mad about bikes!.

Jee wewe unakumbuka nini enzi za udogoni kabisa?!.

Remembering those good old days, makes you feel good!.

Feel Good!.

Pasco

Kweli disc imejaa; hivi ni Anna Kilala au Jane Kilala 🤣
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom