miaka mitatu, nachokumbuka ni kuna dada wa kazi alikua akikaa chumba cha pili kutoka tulipokuwa tuna kaa alikunywa sumu, nakumbuka neno la kwanza kujua kusoma nilikua na miaka mitatu pia lilikua 'takataka' mama alifurahi sana baada ya kulisoma.
.
.
nakumbuka pia niliwahi kumwandikia baba barua nikiwa na miaka minne, alimwagiza kijana mmoja nyumbani kufuata markerpen nikamwandikia barua ya kumpa pole na kazi, na kumwambia siioni je ameiweka wapi? baba alifurahi sana na kumwambia mama ninywe nae chai ya maziwa.
.
.
nakumbuka majina ya niliosoma nao vidudu mpaka chuo kikuu, mpaka na space zao, naona bado kuna space, sema kwa sasa hua nikiwaza kidogo tuu kichwa kinauma sana, hapa tuu nimemeza vivian