Test Your Earliest Memory: How Long Can You Remember?!.

Test Your Earliest Memory: How Long Can You Remember?!.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
57,152
Reaction score
128,807
Wanabodi.

Kumbukumbu ni moja ya vitu ambavyo binadamu anaishi navyo milele hadi kufa navyo!. Ubongo ni kama computer hard disc, na uwezo wa kuhifadhi ni kama computer memory, kadri unavyohifadhi memory nyingi, ndivyo unavyoongeza space ya hard disc yako, wengine ni KB, wengine, MB, wengine ni GB na hata TB, jee wewe unaweza kujijua uko kundi gani?.

Naomba ujikumbushe the earliest thing kilichokutokea udogoni, mpaka leo unakikumbuka, ulipokuja kuhadithiwa ulikuwa na umri gani wakati huo unaweza kushangaa!.

Mimi wakati nikiwa mdogo kabisa, nikiwa naishi Arusha, mbio za mwenge zilipita nje kwetu!. By that time nilikuwa urefu wa buti ya jeshi, kwa sababu hapo barabarani nilipo simama, buti ilikuwa ndio usawa wa macho yangu!. Tukaja kuhama Arusha na kuhamia Tanga, nikiwa mkubwa naonyeshwa picha zangu tukiwa Arusha, naambia tulihama nikiwa 3 years, na wakati tunahama, mwenge ulikuwa haujapita, hivyo nilipoziona mbio za mwenge I was two years na mpaka leo nakumbuka!.

Nilianza Nursery shule ya St. Peters Kindergarten ya Tanga nikiwa 4 years. Mpaka leo, more than 30 years back, nakumbuka baadhi ya majina ya wanafunzi wa darasani kwangu na miongoni mwao ni Alex Shaba, David Naburi, Allen Semu, Irene Minja, Jane Mutayoba, Robert Kilala na Ana Kilala!. Jee wewe unaweza kuwakumbuka baadhi ya wanafunzi mliosoma nao vidudu?.

Nikiwa nursery ndio mara yangu ya kwanza kuvaa shati jeupe, suruali nyeusi, soksi nyeupe na viatu vyeusi!, kabla ya hapo ni raba na ndala tuu. Nilinunuliwa nguo hizi ili kucheza mchezo wa kuigiza mimi nikiwa ndio mfalme!.

Kitu cha ajabu, nimemaliza Chuo juzi juzi, kuna watu nakutana nao mtaani tunasalimiana vizuri, namuomba anikumbushe, ananiambia tulikuwa class moja Chuo!. Yaani wale wazamani ninawakumbuka, hawa wa sasa siwakumbuki!. Nilipojiuliza nikakuta hard dis itakuwa imejaa hivyo it can take no more!. Huyo Robert Kilala na Jene Kilala, baba yao alikuwa ana pikipiki, anawaleta wote wawili wamepakizwa mbele kwenye pikipiki, hivyo nikawa naishangalia sana pikipiki nikitamani na mimi kupandishwa!. Watoto wengine wakiletwa na magari, mimi kwetu hatukuwa na gari, napelekwa shule na dada akiitwa Marrita (Martha), sometimes nikifika shule, siingii kwanza darasani ili kuona pikipiki, kumbe siku ingine wanakuwa wamewahi zaidi na mimi nikiwakuta, I feel sorry, I've missed the fun!. Baadae nilipokuja kuwa mtu mzima I was mad about bikes!.

Jee wewe unakumbuka nini enzi za udogoni kabisa?!.

Remembering those good old days, makes you feel good!.

Feel Good!.

Pasco
 
Huu ni uonevu, mkuu Pasco ... Lile darasa letu kule linasuasua, topic moja kila baada ya miezi miwili .. Then, nakukuta umeanzisha somo jingine ... !!! Hii ni haki kweli ???:nimekataa
 
dah mi sikumbuki asee vingi navikumbuka nilikua kama najielewa kama miaka minne na nusu mpaka mitano mama yangu alikua anasoma basi akija likizo lazima aniletee vigali vya mbao vya kuchonga
 
Mkuu people remember extraordinary au out of ordinary things..., kama wewe kwa bahati mbaya au kukusudia uliwahi kuua mtu hata kama ulikuwa na miaka miwili utakumbuka tu..., ila vile vitu unavyofanya kila siku kama ni watu wangapi au magari mangapi uliyapita siku ya jumapili wakati unakwenda kwa rafiki yako (labda uwe na photographic memory au something different happened on that day ndio utakumbuka).

Kwa ufupi memory ya binadamu ina uwezo mkubwa wa kukumbuka vitu vingi lakini ipo underutilized
 
kichwa hakijai piga ua, connections zinabuild up more n more japo vingine vitakua mbali kukumbuka ila vimo hmohumo, hata mtu aishi miaka buku, hii mishe hujazi, ka unataka ku-erase kagongwe na gari
 
uwezo wa ubongo ni terabytes 2.5.

katika kukumbuka mimi nakumbuka siku ya kwanza kuanza chekechea ingawa nilikuwa na miaka minne, vilevile nakumbuka baadhi ya matukio yaliyotokea nilipokuwa na miaka mitatu.

niliwahi kuangalia episode moja ya natgeo kuhusiana na mmoja wa polga sisters (susan). kuna sehemu moja walikuwa wanaelezea kuhusiana kukumbuka vitu. binadamu ana uwezo wa kukumbuka vitu katika mafungu saba ndiyo maana hata namba za simu ambazo zina vary huwa ni saba mfano 075xxxxxxx, au hotelini mhudumu anaweza kukumbuka oda za watu saba kwa urahisi.
vilevile ubongo una sehemu tofauti za kuhifadhia kumbukumbu kwa jinsi kumbukumbu hizo zinavyokuwa recalled. kwa mfano maelezo kuhusiana na watu unaokutana nao mara kwa mara au njia unayopita mara kwa mara huwekwa sehemu tofauti na maelezo ambayo huyatumia mara chache.
 
Mkuu people remember extraordinary au out of ordinary things..., kama wewe kwa bahati mbaya au kukusudia uliwahi kuua mtu hata kama ulikuwa na miaka miwili utakumbuka tu..., ila vile vitu unavyofanya kila siku kama ni watu wangapi au magari mangapi uliyapita siku ya jumapili wakati unakwenda kwa rafiki yako (labda uwe na photographic memory au something different happened on that day ndio utakumbuka).

Kwa ufupi memory ya binadamu ina uwezo mkubwa wa kukumbuka vitu vingi lakini ipo underutilized

Ni kweli memory ya binadamu ina uwezo mkubwa sana wa kuhifadhi vitu kwani kuna millions of neurones ambazo kwa mujibu wa Neuro Surgeons ni kwamba only 1% tu ndiyo imeshatumika pamoja na ugunduzi mkubwa wa kisayansi uliokwishafanyika!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Mimi nakumbuka, wiki ya kwanza vidudu- kama miaka 35 iliyopita.Mmoja wa wanafunzi darasani kwetu (kwa jina Rehema)alibanwa na haja ndogo. Badala aombe ruhusa kwa mwalimu, akajisogeza kwenye kizingiti cha mlango wa darasa na kuachia bonge la kojo, huku darasa zima tunasshuhudia. Alipigwaje sasa!
 
Wanabodi.

Mimi wakati nikiwa mdogo kabisa, nikiwa naishi Arusha, mbio za mwenge zilipita nje kwetu!. By that time nilikuwa urefu wa buti ya jeshi, kwa sababu hapo barabarani nilipo simama, buti ilikuwa ndio usawa wa macho yangu!. Tukaja kuhama Arusha na kuhamia Tanga, nikiwa mkubwa naonyeshwa picha zangu tukiwa Arusha, naambia tulihama nikiwa 3 years, na wakati tunahama, mwenge ulikuwa haujapita, hivyo nilipoziona mbio za mwenge I was two years na mpaka leo nakumbuka!.

Pasco

Dah! Hapo kwenye mwenge umenikumbusha mara ya kwanza kusikia habari za mwenge, msafara wa mwenge ulipita kijijini kwetu ila haukusimama. Wakati gari lililobeba mwenge lilipokaribia, niliambulia kuona kile kibao kinachokinga upepo chenye picha ya mwenge. Lilipopita nikabaki nawashangaa watu kwamba mbwembwe nyiingi kumbe mwenge wenyewe ni picha tu.
 
Mmmh! Mi nakumbuka wakati niko mdogo, Mjomba wangu alipenda sana kunirusha juu na kunidaka!
One day alinipachika juu ya paa la kibanda, mtu mzima nikaanza kutembea na kuelekea kileleni kwa banda! Walinizungukaje!!!! Teh! Teh! Teh!
 
Me Memory yang inaanzia pale When I was about 5 year old na ni kabla cjaanza hata vdudu (nursery school) wazaz wang walikuwa na shamba la Mahind so ilipokuwa kila akitaka kuenda Shamba alikuwa akinichukua yeye pamoja na mimi na kwa vile nilikuwa Mpenz wa Vitumbua (na kwa wakat huo I remember nilikuwa naita 'Vitobato') hivyo alilazimika kunichulia vtumbua ksha ndio niweze kustahimili route za shamba japokuwa ckuwa na kaz yoyote bt nikuwa karib na my Mom.
Nakumbuka pia nikiwa na Miaka hyo hyo katka kipind hcho hcho nilivyokuwa nikichoka kukaa shamba bas mom alkuwa akinipeleka kwenye Class moja hv Kanisan ambapo enz hzo watoto wa Vdudu walikuwa wanasomea Humo nami nilijoin class japokuwa intention kubwa ya Mom ni kuniweka nitulie na wenzang mida ya uji ikifika nangalia kikombe lkn pia mimi mwenyewe nilikuwa napenda nianze masomo kwa kpnd hcho, so nilkuwa nashirik na nilkuwa nafanya poa sana,japo sikumbuk niliwezaje kujitambua kuwa niko poa lkn ninachokumbuka ni sifa alizokuwa akitoa Mwlm kwa Mom kwamba kwann nisisajiliwe rasm kwan nilikuwa very Bright! HAPO NIKIWA NINA MIAKA MINNE.

Pia nilivyoanza std one nikiwa Age ya 8 yrs (japo nilichelewa) nakumbuka nilikutana na Marafiki Wengi Ambao mpaka leo baadhi yao kwa majina nawakumbuka: Carlos John,Gerevus William,Godfrey Makoba,Ibrahim John,Mika,Anita John na Neema Asangalwise. Baada ya hapo nikiwa Std 5 nilipata nafac ya kuhamia Bush ambako pia nilipata More friends na cha kunishangaza ni kwamba leo hii list ya wale frnd ambao nilianza nao ndio hipo kwenye Memory lkn hawa wa std 5 inahitajika nguvu ya ziada kuwakumbuka.

Cha Ajabu kuna vtuko vile vya ktoto (nan Baba na nan mama) vilinishikisha kumbukumbu ya msichana mmoja hv ambaye mpaka waleo hii huwa natokea kuhisi kumtafuta japo tulipotezana mda mref lkn fikra zang znanituma nmtafute tu she still alive. Huyu yeye yuko kwenye list ya wale nilioanza nao std 1 (Neema Asangalwise) na nina mkumbuka kwa sababu ndie aliyekuwa akinipa company ya kamchezo ka 'nani Baba, nani Mama' And she was a mother yl I was a father na kilikuwa kinanipenda sana though tulikuwa watoto but we used to made a Big promise with.

Kingne ninachokumbuka Japo kuwa sina kumbukumbu ya umri husika ila nilikuwa sizd 4yrs father aliwah kuninunulia vitenes vya kudundadunda na Ndege za ktoto, siku moja nikiwa nacheza katenesi kakadunda kakapotelea uvunguni nilitafuta lkn wap, so mshuwa wang alivyokuja kugundua sina hcho kidude ahahaa! Alipiga..! Over anapiga paka aliyemchosha kwa kumkombea Samaki.

Haukupita Mda kuna Kaka ang akawa kanitapel kachukua Kandege toy kang kalikuwa still Brand new akakafanyia u-mechanics ndio anirudishie kakiwa used, ckuwa na jinc siku hyo nilishnda kwenye sweta huku nimefisha kisionekane halafu mshua akaniuliza vp nilimwambia naumwa naskia barid kal kumbe naxkep Bakora!

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Nakumbuka nikiwa Mdogo sana (sikumbuki exctly ni miaka mingapi lkn si zaid ya Mitano) nilikuwa napenda kujiombeleza kwa Watoto wenzang jambo ambalo siku moja yalinitokea ya kunitokea. Ni pale nilipokaomba pp katoto kenzang, kakanijibu;
'KAOMBE KANISANI" kuskia hvyo nikaingia church nikakuta kuna line ya watu ambao akili yang ilinituma kuwa bila shaka wako kwenye harakati za kupokea kile nilichokiomba bila kupoteza mda, katikat il niwah kutoka nikazama kwenye mstar. 'Sikumbuki ilikuwaje baadae'

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Nakumbuka mama yangu alikua mjamzito akawa anapenda sana kula udongo........mzee alikua hapendi sana hiyo tabia. Basi mama akawa anaficha udongo bafuni....akienda kuoga anakula. Wakati huo nadhani nilikua na 2years.....ilikua naingia nae bafuni ananiogesha then natoka yeye anaoga. I remember alikua ananiweka mapajani pake then ananiogesha.
My solid memory starts from there
 
I bet I was 2yrs coz hiyo mimba ilikua ya mdogo wangu anayenifuatia.....
 
Kila nikikumbuka huwa nashangaa sana...

I rembember nikiwa na 3 years my dad passed away alikuwa anakwenda Mbeya kuchukua gari yake
aliokuwa ameiacha mkoa fulani siku zote dereva alikuw anaenda ila this time naambiwa alingangania
kuwa anataka kwenda mwenyewe

Nakumbuka pic ya the last time anaondoka akiwa kavalia Koti jeusi na suruali yake ya jinzi
na alimwambia dada tuliokuwa nae "angalia sana hawa watoto" tulikuwa tumelala kitandani
ni maneno ambayo sijawahi kuyasahau pia kila nikivuta picha yake hiyo ndio picha inayonijia kwenye akili yangu

mama alikuwa hayupo alisafiri kwenda kwao nilikuwa mdogo sana lakin ile picha haijawahi kunitoka
katika akili yangu baba yangu alifariki wakati anarudi kwa ajali ya hilo hilo gari alilokuwa kaenda kulifuata..
May His soul Rest in Peace
 
Nakumbuka nikiwa about 4 years nikiwa nursery kuna jamaa alirusha mdoli juu ya kabati na mimi kwa utundu wangu nikapanda kwenye ma shelf na kabati likanifuata nilipasuka kichwani na nilizimia

Kuna dada nilikutana naye UDSM nilimkumbuka kwamba tulisoma wote nursery,mwanzoni alicheka sana alijua naleta gia za kibazazi lakini nilivyomtajia jina lake na la mdogo wake aliita rafiki zake na akanisifia sana kwa memory na ikawa kila tukionana ananiambia wewe una kipaji cha kukumbuka,lakini maajabu siku hizi nasahau matukio na majina ya watu niliofahamiana nao karibuni
 
kichwa hakijai piga ua, connections zinabuild up more n more japo vingine vitakua mbali kukumbuka ila vimo hmohumo, hata mtu aishi miaka buku, hii mishe hujazi, ka unataka ku-erase kagongwe na gari

hahaa eti ka unataka kuerase kaginge na gari............
umenikumbusha jirani yangu alipata ajali ya pikipiki sa hivi memory zote zimefutika
kaanza upya tena hata mkewe alikuwa hamtambui imagine mtoto wake ndio kaanza tena
kumfundisha a,e,i,o,u
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom