Tengeneza mtandao wa kifamilia/ukoo

Tengeneza mtandao wa kifamilia/ukoo

Kwetu ndugu ni sisi wa tumbo moja tu, mabwege wengine tulishavurugana nao tangu enzi......Africa hakuna undugu bali unafiki, uchawi, fitina, roho ya kwa nini na majungu
Kabisaa,..ndugu ni wanafiki sanaaa hasa ukionyesha kufanikiwa kidogo tu yani ni kufunga vioo tu tutakutana msibani
 
Hii inawezekana tena kirahisi sana unakuta mtu anaitwa Justine John mwingine Imelda Robinson mwingine Rashidi A Rashidi. Kwa nini msitumie majina ya ukoo? Wazee wa zamani walikuwa na akili sana. Siye wapenda uzungu tunaacha vya kwetu tunakumbatia vya watu majanga kama haya hayatapita mbali.

TODAYS nina mfano hai wa mate wangu ambaye aliingia kwenye mahusiano mpaka mimba huku dar , siku wanaamua kwenda kujitambulisha kwa dada mkubwa wakajikuta wote wanaelekea nyumba moja (mambo ya kukutana kwa kificho gesti hausi mabaya sana)Kumbe yule ni dada yao wote
 
Mkuu upo correct kabisa sometimes watu baki uliokutana nao kwenye mihangaiko ya maisha wanakuwa zaidi hata ya ndugu wa damu. Sijui kwanini tupo hivi? hata ukifanya juhudi ya kuweka familia pamoja litaibuka jambo tuu. Watu wengi wameumizwa na familia zao waliozaliwa nao, wengine wanatoana hadi roho. Bora kutengeza mitandao mingine na watu baki ila hiki suala la familia lipo complex kuliko tunavyodhani na pia ukiwa mtu mzuri watakulalia mpaka utashindwa kununua suruali. Tatizo hatujui kutofautisha MAJUKUMU na MSAADA
 
a5723c24284a4e0e5a53570371e2dd0d.jpg

Ni lazima ujue kwamba yake yanayotokea sasa kwenye familia/ukoo wako ni matokeo ya kile kilichofanyika jana na juzi....na yatakayoleta mwendelezo wa kesho na keshokutwa.

Jitafakari utengeneze mtandao upya mtandao usio na ubaguzi wala tabaka... mtandao wenye kulenga kuleta ushirikiano upendo na mshikamano.

Asitokee au isitokee familia moja ndani ya ukoo ikajiona ni bora zaidi kuliko nyingine, ina mafanikio zaidi kuliko nyingine ina bahati zaidi kuliko nyingine... Huku ni kupandikiza mbegu ya chuki na utengano!mbegu ambayo ikimea na kukomaa itasumbua sana wanandugu.

Panga ziara za ki familia ndugu wajuane wafahamiane watoto wenu wakue wakifahamiana vema, wazoeze kutembeleana kucheza pamoja na kujenga uaminifu na upendo wa kweli kati yao.

Tofauti zenu wakubwa jitahidini kuzimaliza wenyewe bila kuwashirikisha watoto wenu, na hata kama kuna tatizo kati yenu liwe lenu tuu na watoto waachwe wasihusishwe na yasiyowahusu katika umri wao huo

Mafundisho mema kwa watoto ni msingi bora wa kesho yao na mafanikio yao hutegemea sana mahusiano ya kifamilia na hata ndugu.

Mtandao ulenge kuepusha migogoro na mifarakano kwa kiwango kikubwa kabisa....na kila jambo bila kujali udogo wake shirikishaneni na kusaidiana kwa hali na mali.

Kuna tofauti ya vipato elimu ujuzi na maarifa, kuna kupata na kukosa kuna kupanda na kushuka, ila kama mtakuwa mmeshikamana na kubebana mtaishi maisha ya furaha amani upendo na mafanikio huku mkiheshimiana sana.

Bado hujachelewa jaribu kujiangalia kama kwenye familia zenu mna kitu cha namna hii...! Kama bado anza sasa.

NAKUOMBEA [emoji122] [emoji122] [emoji122]
Umenikumbusha miaka ilee bado sisi wadogo tulikuwa tukitembeleana na ndugu wa mbaali likizo mnaenda ama wao wanakuja familia yoootee yaani nyumba inafurika wageni tu nalala sebuleni tunabanana lakini ilikua ni furahaa saana hutamani hata likizo iishee yaani siku zotee ni rahaa mnakutana na watoto wenzenu mnafurahia mnajisoma na madhaifu. Kwa kweli ilikua inatujenga saana mshikamano na upendo vilitawala. Siku hizii upendo umejaa wa maandishi hasa kwa mitandao ya kijamii, nawaambieni hawa wanaoonesha upendo mtandaoni hawainjoi kama enzi zetu banaa.
 
tetee hiki ndio hasa nililenga kwenye hii mada mnajikuta kinachowaunganisha ni upendo tu na sio mali, kila likizo mnabadili kiwanja...watoto wa mjomba binamu baba mdogo nk wote mnakutana sehemu moja
 
tetee hiki ndio hasa nililenga kwenye hii mada mnajikuta kinachowaunganisha ni upendo tu na sio mali, kila likizo mnabadili kiwanja...watoto wa mjomba binamu baba mdogo nk wote mnakutana sehemu moja
Kuna wakati mkienda kuwatembelea ndugu wengine basi alfajiri mnajumuika nao mashambani hata kama hujui kulima mnaenda tuu utang'oa ng'oa hata majani mradi umejumuika, ni booonge la adventure aisee, hapo mmetoka mjini hahaha mnajiunga kwenda kusenya kuni njiani mnapitia matunda pori mjini hayapo.... Those sweet days daah.
 
Yah ni kweli mr. mshana ubinafsi unafanya koo nyingi kutengana na kupotezana, swala la kuwakutanisha wana ndugu pamoja ni jema sana kwani itawasaidia ndugu kujuana, kushikamana na kusaidiana katika vipindi vyote vya shida na raha.
 
Kuna wakati mkienda kuwatembelea ndugu wengine basi alfajiri mnajumuika nao mashambani hata kama hujui kulima mnaenda tuu utang'oa ng'oa hata majani mradi umejumuika, ni booonge la adventure aisee, hapo mmetoka mjini hahaha mnajiunga kwenda kusenya kuni njiani mnapitia matunda pori mjini hayapo.... Those sweet days daah.
Those sweet days [emoji25] [emoji25] [emoji25] golden days . mnavuka mto na kunywa maji yake masafii wala hamuugui au mnaenda kuoga mtoni watoto wa kike wana sehemu yao na wa kiume pia...there was such a unity n trully loving kindness
 
Hakukuaa na status hata mmoja wa mzazi ana pesa nyiingi. [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] kuoga sisi ilikua ziwani wanaume wanasehemu yao na sisi wanawake tunayo yetu walaa hakuna kuchunguliana japo unawaona[emoji1] [emoji1]. Enzi hizo hakuna cha selfie wala nn.....na pia kutwanga udaga au mpunga huku mkisindikizwa na nyimbo za kukutia nguvu daaaah... Mwishowe nilie mieee
 
[emoji23] [emoji23] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Kabisaa,..ndugu ni wanafiki sanaaa hasa ukionyesha kufanikiwa kidogo tu yani ni kufunga vioo tu tutakutana msibani

Hii ni tofauti na kwetu, ukifanikiwa kidogo tu ndio unapendwa sana ili wakutumie tu.
 
hii mada ni nzuri sana, hongera kaka yangu mshana kwa kuweka bandiko hili. Makovu ni mengi sana yanayotokana na undugu, lakini wote tunakubaliana umuhimu wa koo kuwa pamoja. Nafikiri ingekua vizuri kama tungeweka mbinu mbadala za kufanya ili kuunganisha undugu na kuunganisha koo. mfano mimi nashuari njia mbili zinaweza kutumika, wengine wanaweza kujazia mbinu nyingine
1. Kuwe na siku ya kufagilia au kuzuru makaburi kwa mwaka yaani ndugu mnakutana mnasafiri kwenda kufagilia makaburi hii itawapa fursa ka kukutana na kubadilishana mawazo. Mfano wenzetu wachina wana sikukuu yao inaitwa Qingming hii ni siku maalamu kwa watu wa ukoo kwenda kuzuru makaburi. Wenzetu wachaga pia wanayo siku ya kwenda moshi kuhesabiwa. Tunaweza kuanza na hili.
2. Kuanza na kuunganisha watoto, kwa vile watoto ni very innocent wao hawana hizo chuki na magomvi yenu. Mnaweza kuanzisha get together ya watoto kwenye ukoo. Kuanzia hapo mnaweza kujikuta mnaunganisha mpaka familia.
N.B
Ni kweli hili jambo ni gumu sana na changamoto ni kubwa lakini lina faida kubwa. kwa hiyo haitakua rahisi inahitaji uvumilivu na kujitoa.
 
Ukiona mtu anahangaika sana kutafuta ukoo, ujuwe hapo kuna walakin.

Jee, hamuelewi kuwa zaidi ya 40% ya Watanzania hubambikiwa baba zao?

Sasa mnaona haitoshi mnataka kuwabambikia familia nzima.

Si hasha Tanzania hii unakuta ndugu watano wa baba mmoja na mama mmoja lakini wote hawafanani. Tulikuwa tunadanganyana "kafanana na babu yule mzaa mama" na huyu "kafanana na bibi yake", wanasayansi tena Wakitanzania wanasema hapana, hao mnabambikiana.

Ni mawili, amma ulibambikiwa baba na umepata fununu yu wapi ndiyo unaanza kuhangaika kujibadilisha na kujinasibisha au ulizaliwa nje ya ndoa na baba'ko hajulikani ndiyo utaanza kuitafuta koo yake au na visababu vingine vidogo vidogo vinavyohusiana na hayo hayo.

Jadi na jadi ya asili za huku kwetu tunaishi ki extended family, inaniwia vigumu leo hii kuamini mtu anatafuta ukoo wake kama hakuna walakini.
 
[emoji16][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Back
Top Bottom