Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,657
- 729,764
Ni lazima ujue kwamba yake yanayotokea sasa kwenye familia/ukoo wako ni matokeo ya kile kilichofanyika jana na juzi....na yatakayoleta mwendelezo wa kesho na keshokutwa.
Jitafakari utengeneze mtandao upya mtandao usio na ubaguzi wala tabaka... mtandao wenye kulenga kuleta ushirikiano upendo na mshikamano.
Asitokee au isitokee familia moja ndani ya ukoo ikajiona ni bora zaidi kuliko nyingine, ina mafanikio zaidi kuliko nyingine ina bahati zaidi kuliko nyingine... Huku ni kupandikiza mbegu ya chuki na utengano!mbegu ambayo ikimea na kukomaa itasumbua sana wanandugu.
Panga ziara za ki familia ndugu wajuane wafahamiane watoto wenu wakue wakifahamiana vema, wazoeze kutembeleana kucheza pamoja na kujenga uaminifu na upendo wa kweli kati yao.
Tofauti zenu wakubwa jitahidini kuzimaliza wenyewe bila kuwashirikisha watoto wenu, na hata kama kuna tatizo kati yenu liwe lenu tuu na watoto waachwe wasihusishwe na yasiyowahusu katika umri wao huo
Mafundisho mema kwa watoto ni msingi bora wa kesho yao na mafanikio yao hutegemea sana mahusiano ya kifamilia na hata ndugu.
Mtandao ulenge kuepusha migogoro na mifarakano kwa kiwango kikubwa kabisa....na kila jambo bila kujali udogo wake shirikishaneni na kusaidiana kwa hali na mali.
Kuna tofauti ya vipato elimu ujuzi na maarifa, kuna kupata na kukosa kuna kupanda na kushuka, ila kama mtakuwa mmeshikamana na kubebana mtaishi maisha ya furaha amani upendo na mafanikio huku mkiheshimiana sana.
Bado hujachelewa jaribu kujiangalia kama kwenye familia zenu mna kitu cha namna hii...! Kama bado anza sasa.
NAKUOMBEA