Shemeji yangu amegushi muhtasari wa ukoo wa mirathi

Shemeji yangu amegushi muhtasari wa ukoo wa mirathi

Choosen85

JF-Expert Member
Joined
Jun 22, 2022
Posts
2,336
Reaction score
5,667
Wakuu kwema huko wale town na wale wa bush mko sawa wapambanaji...wahaini, magaidi wa serikali mpo pia...🤔
Wakuu ndugu yangu alifariki baada ya maziko ukoo ulikaa kikao cha kujadili mali za marehemu na kuteua msimamizi wa mirathi. Tuliamua kwa kauli 1 kwamba mke wa marehemu ndo awe msimamizi wa mirathi na mali zingine zote tulimkabidhi yeye na hakuna aliyechukua hata kikombe cha marehemu.

Marehemu aliacha watoto wawili. Sasa tuliandika muhtasari wa ukoo wa uteuzi wa msimamizi wa mirathi na tukamkabidhi mke wa marehemu aendelee na taratibu alipofika mahakamani akaambiwa muhtasari huo ufanyiwe baadhi ya marekebisho aurudishe kwenye ukoo afanyiwe marekebisho hayo.

Yeye sjui alikaa na akina nani wakajiandikia muhtasari wakapachika majina ya mwenyekiti na katibu wake walewale wa uko na kusaini saini zao za kughushi kisha akarejesha mahamakani. Sasa alipokwama ni mahakama kumwambia waje mashahidi wawili wa ukoo kuja kuthibitisha muhtasari huo.

Alipolileta hilo ndo hapo katibu akamuomba huo muhtasari aliopeleka mahakamani ndo akatuma muhtasari tofauti wenye sahihi bandia na umefanyiwa marekebisho mvutano ukaanza hapo sasa kwanini kaandika muhtasari mwingine ambao ukoo hauujui na kwann kafoji sahihi za watu.

Siku kesi ilipotajwa ili ndugu wawili wakathibitishe niliagizwa nikashughulikie ikiwemo kuandika barua ya pingamizi kwamba muhtasari huo ulioko mahakamani hautambuliki na ukoo kwani kuna sahihi za watu wa familia zimefojiwa na muhtasari huo ni fake, pia kuna vipengele vimeondolewa bila taarifa kwa ukoo.

Sasa nimelifikisha hilo japo ni kama hakimu alitaka kunibabaisha fulani kwamba muhtasari huo hata usipokuwepo mahakama inaweza kuteua msimamizi wa mirathi mi nikamwambia hakimu kama ndivyo wanikabidhi huo muhtasari niondoke nao leo niupeleke kwenye ukoo kwamba mahakama imesema muhtasari hauhitajiki tena wao watateua msimamizi bila muhtasari 😀

Hakimu akanywea kidogo akasema basi uamuzi ni kwamba muhtasari urudi kwa ukoo wamsaidie msimamizi kufanya marekebisho na urudishwe mahakamani au isipofanyika hivyo basi kesi hii ya msimamizi wa mirathi itafutwa na itafunguliwa kesi nyingine ya pingamizi 😀

Mi nikwambia hakimu we mkabidhi huo muhtasari mhusika arudi kwenye ukoo wamsaidie sasa shida anarudi vipi huko wakati ameshagombana na raia wengi akiwemo katibu aliyeandika muhutasari ngoma nzito.

Lakini pia asiposaidiwa hilo kesi inafutwa na inafunguliwa ya pingamizi sasa huko ndo kutakuwa na shughuli kwani mhusika amedanganya mahakama kwa kughushi muhtasari na sahihi ya mwenyekiti na katibu wake 😀

Je wakuu mnanishauri nn mpaka hapo hasa kesi ikifunguliwa ya pingamizi kulingana na barua niliyoandika na kile amefanya shemeji yangu?
Pili je anaonewa? 🤔​
 
FB_IMG_1788276570111.jpg
 
Roho mbaya inawasumbua upande wa marehemu,mlivyoamua kujitoa kwa kutotaka kukodolea macho mali za mama mjane fanyeni hivyo hivyo,msaidie mhitasari mumuache peke yake huyo mama apambane na Hali yake.

Kuna ka harufu ka kutamani mali za marehemu ili Khali mumiliki wake yupo
 
Huo ni mtazamo wako mkuu kwani we hujaelewa nilichoandka hapo, kosa alilofanya ni kuambiwa arudishw muhtasari ufanyiwe marekebisho yeye akaandka mwingne mpya na akabandika majina ya watu na akasaini kwamba wao ndo wamesaini we mpumbavu nn yaani unataka watu watumike kwenye kitu cha uwongo siyo 🤔 kwani angeleta hilo swala kwenye family nani angekataa kumrekebjshia ikiwa tyr ameshakabiziwa kila kitu sa kuna shida gani hapo...
WE UTAKUBALI MTU ATUMIE JINA LAKO NA KUWEKA SAINI FAKE ASEME WW NDO UMEFANYA KWENYE KITU USCHOKIJUA kumany.oko ww unadhan watu huku wana njaa na mirathi ya mtu nipe ushahidi hata 1 hapo unaoonyeshe kuna tamaa za watu kutaka mirathi 🖕
 
Asa kama marehemu kaacha mke na watoto wawili nyie mnataka nini hapo?
We huoni shida iko wp hapo au huelewi nilichosema hapo, yeye kaandika muhtasari mwngne bila taarifa na katumia majina ya watu na kaweka na sahihi za watu hao za uwongo we ungekubali kutumika kwa mtu kujihalalishia kitu kwa kughushi sahihi yako wakati mtu huyo alikuwa na uwezo wa kukutaarifu na ukamsaidia kihalali
 
Marekebisho yaliyotakiwa na mahakama yalihusu nini hadi saini zihitajike upya na mtu aghushi? Si ange-attach tu nakala ya mwanzo yenye saini kwenye hayo marekebisho!!

Au muhtasari wa mwanzo haukuwa na saini za kikao cha ukoo?

Ni kama mna nongwa hivi,sioni sababu ya kuitisha kikao cha ukoo tena kwa ajili ya marekebisho kama hakukuwa na pande zinazovutana kwenye huo muhtasari.
 
Hao watoto wawili wote huyo ndiyo mama yao?..kama ndiyo kipi kilimfanya afoji?,au familia ilimega baadhi ya mali ya marehemu?.
Hakuna kilichomegwa hata kikombe cha marehemu vyote kapewa mkewe hata mirathi kakabidhiwa yeye afatilie 😀 marehemu kaacha vitu vya ndani tu hakuna anayetaka chochote vyote anavyo mke, watoto wanasoma na wameshalipiwa ada na ukoo na hakuna anayemendea mirathi shida ni kujiandikia muhtasari na kubandika majina ya watu na kuweka sahihi zao za uwongo ww ungekubali
 
Dah poleni. Mambo ya ndoa na mali ayo
Bt hakuna mwenye shida na mali na mali zenyewe zpi sasa vitu vya ndani au maana hakuna kingne shida tu alipopeleka muhtasari akaambiwa aurudishe kwenye ukoo ufanyiwe marekebisho kisha aurejeshe mahakamani yeye hakusema ila alikaa akajiandikia na akabandka majina ya mwenyekt na katibu walioandka muhtasari na akasaini kwa sahihi fake ww ungekubali kutumika ivo
 
Huo ni mtazamo wako mkuu kwani we hujaelewa nilichoandka hapo, kosa alilofanya ni kuambiwa arudishw muhtasari ufanyiwe marekebisho yeye akaandka mwingne mpya na akabandika majina ya watu na akasaini kwamba wao ndo wamesaini we mpumbavu nn yaani unataka watu watumike kwenye kitu cha uwongo siyo 🤔 kwani angeleta hilo swala kwenye family nani angekataa kumrekebjshia ikiwa tyr ameshakabiziwa kila kitu sa kuna shida gani hapo...
WE UTAKUBALI MTU ATUMIE JINA LAKO NA KUWEKA SAINI FAKE ASEME WW NDO UMEFANYA KWENYE KITU USCHOKIJUA kumany.oko ww unadhan watu huku wana njaa na mirathi ya mtu nipe ushahidi hata 1 hapo unaoonyeshe kuna tamaa za watu kutaka mirathi 🖕
Ukiona hivyo ujue hili swala lina makandokando. Mpeni haki yake mali za marehemu ni za familia yake ni Haki yao!
 
Bt hakuna mwenye shida na mali na mali zenyewe zpi sasa vitu vya ndani au maana hakuna kingne shida tu alipopeleka muhtasari akaambiwa aurudishe kwenye ukoo ufanyiwe marekebisho kisha aurejeshe mahakamani yeye hakusema ila alikaa akajiandikia na akabandka majina ya mwenyekt na katibu walioandka muhtasari na akasaini kwa sahihi fake ww ungekubali kutumika ivo
Mkuu Acha Roho mbaya halafu unatamaa na mali za watu
 
Ukiona hivyo ujue hili swala lina makandokando. Mpeni haki yake mali za marehemu ni za familia yake ni Haki yao!
Makando kando yapi sasa 🤔 hapo kama kila kitu kipo mikononi mwake watu hawataki kutumika kwa kitu waschokijua sasa yaani mtu aandike jina lako na kuweka sahihi yako fake kwenye document inayotakiwa enda mahakamani wewe utakubali wakati document hiyo alikuwa na uwezo kukurejeshea umfanyie marekebisho na aipeleke
 
Marekebisho yaliyotakiwa na mahakama yalihusu nini hadi saini zihitajike upya na mtu aghushi? Si ange-attach tu nakala ya mwanzo yenye saini kwenye hayo marekebisho!!

Au muhtasari wa mwanzo haukuwa na saini za kikao cha ukoo?

Ni kama mna nongwa hivi,sioni sababu ya kuitisha kikao cha ukoo tena kwa ajili ya marekebisho kama hakukuwa na pande zinazovutana kwenye huo muhtasari.
Sawa mke wa marehemu 😀
 
Mkuu Acha Roho mbaya halafu unatamaa na mali za watu
Sawa mke wa marehemu 😀 mi na roho mbaya lete huo muhtasari watu wakusainie tu na ueleze kwann ulisaini sahihi fake za watu ambao ungeweza onana nao tu wakakurekebshia na kukusainia
 
Si mtumie ule wa mwanzo.. Mrekebishe au? Ila why uliandika hayo na ni kama una cheka.. Lazima kuna watu walimtisha mpe nafasi msaidie atakuwa amejuta kimya kimya
Namsaidia sn na naongea naye mi sina tatzo kbs nimemwambia tu arudi kwenye family wamrekebishie nipo tyr kumsaidia vzr tu
 
Back
Top Bottom