Tendwa sasa atishia kukifuta CHADEMA

Tendwa sasa atishia kukifuta CHADEMA

Tendwa hajui wajibu wake wa kazi. Yeye ni msajili wa vyama nchini, kwa lugha nyingine yeye ni mlezi na baba wa vyama vyote vya kisiasa. Baba badala ya kuwatetea watoto wanaponyanyaswa unakaa kimya.kucheza ni sehemu ya makuzi ya mtoto, kazi ya Baba ni kuhakikisha mtoto anacheza kwa usalama huku ukimpa ulinzi wote na wala si kumzuia kucheza.Vyama vya siasa ni watoto wako Tendwa. kujitafutia wanachama ni sehemu ya michezo ya Vyama vyote katika makuzi yao. Wajibu wako ni kuhakikisha wanacheza kwa usalama, yaani wasibugudhiwe. Ukiwazuia kucheza(kutafuta wanachama) watadumaa. Kipindi cha kutafuta wanachama ni muda wote kabla ya kampeni kuanza na mara tu baada ya uchaguzi kuisha

Sasa wewe Tendwa Msajili gani hujui hata kutofautisha kati ya Kampeni za uchaguzi na Ushawishi kwa wananchi ili wajiunge na chama. Kampeni zinaenda na kusema mchague fulani na sio fulani. Chadema hawapigi kampeni bali wanawashawishi wananchi wahamie Chadema.

Umesahau sharti mojawapo kwa chama chochote ili kisajiliwe lazima kipate wanachama wasiopungua 200 kila mkoa? hiyo ni kianzio tu ili kupata usjili. Baada ya usjili lazima chama kirudi kwa wananchi kujinadi ili kujiongezea wafuasi.

Tendwa unatakiwa uvihamasishe vyama vilivyobweteka mjini kuiga mfano wa CDM wa kujitafutia wafuasi zaidi, au unapenda kuwa na vyama dhaifu kama mtoto mwenye utapiamlo?

None sense, Ndio maana nikasema hujui wajibu wako. Wewe unatakiwa kuwamtetezi No. 1 wa chadema wanapozuiwa kutekeleaza haki yao ya michezo ya makuzi. Umekaa kimya kipindi chote hicho unakuja kubata-bata dakika za mwisho
 
makada wa sisiem bana wata matatizo sana......ngoja tuone na huyu mwisho wake ni upi,,,,,,,,
 
Hilo ndilo tatizo la kupeana kazi kiushikaji, Tendwa amepewa handout na akaisoma pasipo kubadili kitu.
Inaelekea ukweli anaujua japokua kwa makusudi kabisa hataki hanajifanya kipofu aoni wala hasikii ujinsi upepo unavyovuma anadhani kwa hali ilivyo sasa ni rahisi kuifuta Chadema kama ambavyo mwalimu anavyofuta maandishi kweye ubao.
Kinyume na mawazo yake leo hii ni rahisi kuifuta CCM kwa sasa na ukapata uungwaji mkono wa watu wengi kitaifa na kimataifa kuliko CDM.
 
This is victim blaming. It is supporters of CHADEMA that are being killed. But we know what the plot is. Slaa fingered it before implementation began. He clearly elucidated that there was a plan for CCM to arm its cadres, cause mayhem and blame it on CHADEMA.

CCM cadres are walking around with handguns, and I suppose they are not limiting themselves to pointing them at each other.CCM has come to the conclusion that it cannot compete with CHADEMA. It is hoping to do away with CHADEMA by using surrogates in positions of power.

CHADEMA does not exist at the pleasure of the Registrar of Political Parties. It is not at his mercy. I would advise CHADEMA to go to court and seek an injunction against the Registrar. It must be possible to obtain an order that restrains him from abusing his power.

It is critical for CHADEMA to show Tendwa that it is a mass movement that cannot be stopped by him. He must be confronted once and for all.
 
Kwa hiyo hapo hakuna sheria tena....ni suala la yeye kuchoka tu basi! Walsa hahitaji kujua wanaofanya hizo vurugu ni akina nani, wala wanaua na kuuawa ni akina? Ni suala la yeye tu kuchoka then anachagua upande wa kuazibu bila kuzingatia niliyoyataja hapo juu.
Wakati anakiri hakuna sheria inayokataza mikutano nje ya kampeni, lakini anashauri vyama vifanye mikutano kwa wakati ule umpendazo yeye.....
This is Tendwa ,anahubiri asiyoyaamini na kujaribu kutufundisha asiyoyakubali...
 
Msajili wa vyama vya siasa nchini John Tendwa amesema sasa amechoka kusikia mauaji kwenye mikutano ya kisiasa ya CDM na atatumia rungu lake kufutia usajili chama chochote kitakachoshindwa kutunza amani ya nchi.Tendwa amewaambia waandishi wa habari hatishiki na chama chochote kuwa na wabunge kwani sheria inamruhusu kufuta chama hata kama kina wabunge 100.

Katika hali ya kushangaza Tendwa ameshauri vyama visubiri nyakati za uchaguzi ndipo vifanye mikutano ya kisiasa.Hata hivyo amekiri sheria inaruhusu vyama kufanya mikutano na maandamano wakati wowote.

Source:Habari Radio Tumaini.
Humu JF wakuu kuna manabii, issue zikisemwa zinatimia. Hii nayo ilishasemwa. Nchi hii kuna mambo.
 
hizi ndizo shortcomings za viongozi wa Tanzania.Stereotypes, wanatumia akili kwa kiasi kidogo sana kwa manufaa ya taifa na sehemu kubwa wanazihamishia sehemu nyingine.haiwezekani wakaenda katik obvious kiasi hicho yet wakajiita ni viongozi wa taasisi inayotakiwa kuwa Neutral.

Nimesikia hotuba ya huyu jamaa ila kajiumauma na kujirudiarudia kuhimiza karipio lake liende kwa vyama.Huku akigusa polisi kama zuga.Seems that viongozi wengi wameamua chagua political suicide kama default option yao.

Hotuba yake ya kwanza haikutakiwa ongea hizi junk kama za leo.Leo alitakiwa akiwa kama patron wa political parties, alitakiwa exclusively akomae na polisi huku akitoa pole kwa Tasnia ya habari.Then andae seminar na kuelezea dukuduku zake.

Sasa huyu mzee anajifich aktika kichaka dhaifu namna hii.Yaani kutumia wingi ndio kutatoa target?mbona tukio alilokuwa kiongelea ni wazi kuwa limekuja katik mazingira ambayo CDM ndio chama pekee cha kisiasa.Na udhaifu tayari hukumu ya raia imepita.Kama ni kubalance angelisema kuwa na polisi nao atawapeleka mahakamani.Leo huyu mzee wa town kapotea mjini.Anatumia kauli ipo uchi kuongelea mambo ya sirini?

Kinaniuma sana kuona watu wenye wajibu mkubwa wakiwa so predictable .Yaani suala linalohusu CDm unaweza tegemea nini kinafuata wakiwa polisi, wakiwa viongozi wa CCM, wakiwa viongozi wa upinzani wanaoitwa mamluki, msajili wa vyama, na hata wapiga domo wa media.

CCM wanaanza poteza control kwa kiasi kinachoogopesha,kila anayeibuka anasema lake.Kwa vile hawana wa kuwapa onyo,basi mwingine naye anaona kuwa hiyo ndio njia na wote wanaanza shindana katika mambo hatari sana.Sijaona wanachama wa CCM wakijfunza hata kidogo,kuwa kuingia katik malumbano na CDM ni kujiua kisiasa kabla hata effect hazijafika CCM.
 
Anazidi kuhalalisha kile nilichosema ktk ule uzi wangu wa sababu 3 zilizoko nyuma ya vifo ktk mikutano ya Chadema. Vifo hivyo, vinataka kuhalalisha jambo. Kama si kuchafua chadema, basi ni kuifuta chadema. Exactly, kama alivyosema rafiki yangu. Nijuavyo na niaminivyo, hilo halitawezekana.
Pili, kwa kuwa mjadala wote sasa umeelemea polisi kwa kubebeshwa lawama zote, Tendwa anataka kubadili mjadala uwe Chadema na vifo. Watz wa leo siyo wa miaka 50. Hawatafanikiwa.
Wewe ndie yule nabii ajaye, au tutazamie mwingine!
 

IMEBAINIKA kuwa mwenendo wa mauaji yanayofanywa na Jeshi la Polisi katika mikutano na maandamano ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ni mkakati wa makusudi uliosukwa na watawala ili kukivuruga chama hicho, na kuwatisha wananchi kwamba ni chama cha fujo.

Hii si mara ya kwanza kwa watawala kufanya njama hizi dhidi ya wapinzani. Mara ya mwisho, waliofanyiwa hivyo ni Chama cha Wananchi (CUF), kilipokuwa chama kikuu cha upinzani.

Njama hizo zilikiangusha chama hicho, hadi kikajisalimisha kwa kufunga ndoa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, huku kikipoteza mvuto Tanzania Bara.

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wameliambia gazeti hili kuwa, CHADEMA inapaswa kuwa macho na njama hizi, kwani CCM imegundua kwamba inazidi kudhoofika na CHADEMA kinazidi kuimarika katika jamii; hivyo walio madarakani wanafanya kila njama kuua wapinzani ili wabaki madarakani.

Siku chache zilizopita, polisi walimuua kijana Ally Zona wakati wakitawanya waandamanaji wa CHADEMA mjini Morogoro. Jumapili iliyopita wameua mwandishi wa habari wa kituo cha Channel Ten, Daud Mwangosi, mkoani Iringa na kuleta sokomoko la kitaifa, ambalo limelichafua mno Jeshi la Polisi na Tanzania mbele ya jumuiya ya kimataifa.

Utetezi wa polisi na jitihada zake kuwasingizia CHADEMA, waandishi na wananchi wengine kuwa ndio walifanya mauaji hayo, umegonga mwamba kwa sababu katika matukio yote haya, wapo mashahidi walikuwepo pale pale.

Matukio haya yanatokea wakati ambapo vita ya kisiasa baina ya chama kilichoko madarakani na CHADEMA ikizidi kuongezeka kutokana na uungwaji mkono mkubwa unaopata chama hicho cha upinzani kwa sasa kuliko historia ya wakati mwingine wowote.

Kasi ya kukua kwa CHADEMA katika miaka ya karibuni inatishia madaraka ya watawala ambao wamekuwa madarakani kwa miaka ipatayo 50, na ambao chama chao, CCM, kimepoteza mvuto kwa umma, na hakiaminiki kutokana na kuzongwa na tuhuma nyingi za ufisadi, na kukumbatia makundi hasimu yanayotafuta madaraka na masilahi mengine, huku yakiendelea kudhoofisha uongozi wa CCM uliokwisha nyong'onyea.

Wakati CHADEMA kikipambana kukumbatia mapenzi ya umma unaokiunga mkono, huku kikifungua misingi na matawi vijijini, CCM inahaha kukidhibiti kwa propaganda na nguvu za polisi.

Kwa muda mrefu, CCM imejaribu kukipaka CHADEMA matope ya ukanda, ukabila na udini, kama ilivyofanya kwa CUF miaka ya nyuma; lakini baada ya kuona mbinu hizo zimeshindikana, sasa imeamua kutumia jeshi kutisha viongozi wake na wananchi kwa visingizo mbalimbali.

Hata hivyo, CHADEMA kinasema kimejiandaa vema kukabililiana na propaganda zote na vitisho vya watawala; na kwamba kimejifunza kwa makosa waliyofanya wengine katika NCCR-Mageuzi na CUF.

Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lissu, anazo tafsiri tatu za matukio ya mauaji yanayofanywa na polisi katika mikutano ya CHADEMA.

Anasema: "Hawana majibu na matatizo ya wananchi, hawana majibu na tatizo la maji, elimu, matibabu ya uhakika na kero kadha wa kadha zinazowakabili wananchi. Kwa sababu hawana jibu, wanatumia nguvu. Sasa hawatumii vitisho tu, wanatumia nguvu.
"Hii ni taswira ya ‘system' (mfumo) inayojua inaondoka. System imara haitumii nguvu, inatumia vitisho, kama kupeleka watu mahakamani. Sasa huko tumekwishapita, tumeingia katika hatua ya kuuawa."

Tafsiri ya pili ya Lissu, ambayo ina uhusiano na ile ya kwanza, ni kwamba kwa vile watawala wanaona wako hatarini kuondoka, wanatafuta namna ya kuwachafua CHADEMA kwa wananchi ili wawaogope.

"Ikishindikana kutuchafua kwa propaganda wanaua. Wanaua watu kwenye mikutano na hadharani. Maana yake ni nini? Ni kwamba wanatuma ujumbe kwa jamii kwamba ukienda kwenye maandamano ya CHADEMA utakufa. Tafsiri yake ni kwamba watu waogope," anasema Lissu.

Tafsiri yake ya tatu ni kwamba, watawala wanatengeneza mazingira ya kisiasa ili CHADEMA kionekane chama cha vurugu, ili utafutwe msingi wa kukifutia usajili.

"Ukishafanya mauaji kwenye mkutano unajenga mazingira ya kusema hiki chama hakina sifa, unamtengenezea mazingira msajili wa vyama vya siasa akiondoe…ukikiondoa CHADEMA maana yake umeondoa mgogoro na bungeni…utawaondoa akina Lissu, akina nani kule… Hivyo, nasema wanatafuta sababu ya kuendelea kutawala kupitia kuua raia," anasema Lissu.

Anasisitiza kwamba kwa mantiki hiyo, Jeshi la Polisi limeacha kazi yao ya msingi ya kulinda raia na mali zao, na sasa limegeuka jeshi la kulinda walio madarakani ili waendelee kutawala.

"Jeshi limegeuzwa chombo cha ulinzi wa watawala. Hilo la kusema kwamba kazi ya Jeshi la Polisi ni kulinda raia na mali zao ni siasa, lakini the primary function (kazi yao ya msingi) ambayo hawaisemi ni hii ya kulinda watawala ili waendee kuwepo," anasema Lissu.

Aidha, wachambuzi wanasema kinachotokea sasa ni kwamba watawala wanaanza kuhamanika, na wanaweza kutumia polisi kutenda mambo ambayo hatima yake itakuwa mbaya kwao, kama ilivyokuwa kwa watawala wa mataifa mengine waliofikishwa kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu dhidi ya binadamu, The Hague, Uholanzi.

Taratibu, kwa sababu ya matumizi mabaya ya Jeshi la Polisi, hata sifa ya Tanzania katika jamii ya kimataifa inaanza kuchafuka.

[TD="bgcolor: #FFFFFF"]
Njama za kummaliza Dk. Slaa, CHADEMA zabainika

na Mwandishi wetu
Tanzania Daima

[/TD]
[TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF"][/TD]
 
shida ya tendwa ni kada anaota ili kuwafurahisha watalawa masikini ajui ni chadema au polisi ndio wauwaji,unaifuta chadema au mwamko wa watanzania?
 
...Hili la kufuwa CDM linaweza kabisa kutokea kwa sababu propaganda zote za magamba kuhusu CDM kwamba ni chama cha Wachagga na Wakristo zimeshindikana na sasa wanataka kukipaka matope kuonyesha kama kina uhusiano na haya mauaji yanayotokea, kitu ambacho hakina ukweli wowote.

Msajili wa vyama vya siasa, kitengo kingine cha magamba, awe makini sana kutokurupuka na kuifuta CDM. Uamuzi huu wa kuifuta CDM unaweza kuleta vurugu kubwa sehemu nyingi nchini ambazo zinaweza kabisa kusababisha maafa makubwa.

Huu si wakati wa kuweka mbele maslahi ya magamba ili waweze kutimiza ndoto yao ya kutawala milele bali ni wakati wa kuweka mbele maslahi ya nchi ili kuepuka maafa makubwa yanayoweza kusababishwa na maamuzi ya kukurupuka ambayo yanaweza kabisa kutuachia majuto makubwa kwa miaka mingi ijayo. Mungu ibariki Tanzania.
 
Watambue kuwa wanaweza kuuwa chama (CHADEMA) wana weza kuuwa watu, lakini kamwe hawawezi kuuwa mawazo ya kimapinduzi yaliyoko katika akiliza Watanzania hivisasa!
 
Msajili wa vyama vya siasa nchini John Tendwa amesema sasa amechoka kusikia mauaji kwenye mikutano ya kisiasa ya CDM na atatumia rungu lake kufutia usajili chama chochote kitakachoshindwa kutunza amani ya nchi.Tendwa amewaambia waandishi wa habari hatishiki na chama chochote kuwa na wabunge kwani sheria inamruhusu kufuta chama hata kama kina wabunge 100.

Katika hali ya kushangaza Tendwa ameshauri vyama visubiri nyakati za uchaguzi ndipo vifanye mikutano ya kisiasa.Hata hivyo amekiri sheria inaruhusu vyama kufanya mikutano na maandamano wakati wowote.

Source:Habari Radio Tumaini.
Yeye aendelee kutishia maana kutishia si kufanya hata yeye anajua hana uwezo huo,wakati anatishia makamanda wao wanachapa kazi.

Akili yake imechoka na anaongea kile ambacho yeye mwenyewe hakiamini.
 
Mbwa koko nyie mtaishia kutukana hapa tu lakini hamna ubavu wa kupigana na sisi. Na ndio maana mnaanzisha ugomvi halafu mnakuja kulialia hapa kwa machangudua wenzenu.

Nakumbuka ndio hata kipindi cha mkapa askari walivyoingia na viatu pale mwembe chaina walivyoua watu kule visiwani. Vyie mnajua sana na ni kweli hatuwawezi
 
Back
Top Bottom