Tendwa sasa atishia kukifuta CHADEMA

Tendwa sasa atishia kukifuta CHADEMA

Msajili wa vyama vya siasa nchini John Tendwa amesema sasa amechoka kusikia mauaji kwenye mikutano ya kisiasa ya CDM na atatumia rungu lake kufutia usajili chama chochote kitakachoshindwa kutunza amani ya nchi.Tendwa amewaambia waandishi wa habari hatishiki na chama chochote kuwa na wabunge kwani sheria inamruhusu kufuta chama hata kama kina wabunge 100.

Katika hali ya kushangaza Tendwa ameshauri vyama visubiri nyakati za uchaguzi ndipo vifanye mikutano ya kisiasa.Hata hivyo amekiri sheria inaruhusu vyama kufanya mikutano na maandamano wakati wowote.

Source:Habari Radio Tumaini.
Ndivyo alivyotumwa na wakuu wake wa kazi?aache kutumika vibaya kama condom,mzee mzima eli mradi aendelee kupanda magari mazuri na maisha safi basi kila analoambiwa anakurupuka tu,mzee vinamwisho hivyo utaviacha tu ukumbuke hilo halafu sijui utajificha wapi?ccm haitatawala milele hata ufute leo itatokea chadema nyingine aache ujinga asifikiri tupo zama za mawe tulishatoka huko
 
anaacha kuwaambia wauwaji ambao ni police anakiambia chama,chama kinaweza ua mtu,yeye alisikia wapi m4c imeua mtu kama si ujinga na makamasi yaliyojaa kwenye kichwa,aibu sana kwa zee kama lile,hawa ndo wakudili nao siku ccm ikipigwa chini
 
Wana jf, nimemsikia msajili wa vyama vya siasa John Tendwa akitishia kufuta chama cha siasa kitakachosababisha mauaji,lkn sote tunajua wanaosababisha vurugu na mauaji ni polisi,hakuna mahali vurugu au mauaji yametokea bila polisi kuhusika,mikutano au maandamano yanayofanyika bila polisi kuingilia huisha salama. Tunaona kwamba wanaoharibu amani yetu ni polisi badala ya kutulinda wanatuua,Hivyo Tendwa angetakiwa kutafuta chanzo cha tatizo na kutolea ufumbuzi wa kina.Ili kuondokana na machafuko Tendwa atangaze kufuta jeshi la polisi(kama ana mamlaka),kauli za vitisho hazijengi-polisi wasiingilie mikutano ya vyama vya siasa hakutatokea mauaji tena. Nawasilisha kwenu wana jf
 
HIVI TANZANIA HAKUNA WACHAWI WANAOWEZA KUWALOGA HAWA WASHE*^&+ZI WAAMKE MATUMBO NJE KAMA MWENZETU ALIVYOFANYIWA NA polisi??????

maneno ya hasira tu haya
 
Msajili wa vyama vya siasa nchini John Tendwa amesema sasa amechoka kusikia mauaji kwenye mikutano ya kisiasa ya CDM na atatumia rungu lake kufutia usajili chama chochote kitakachoshindwa kutunza amani ya nchi.Tendwa amewaambia waandishi wa habari hatishiki na chama chochote kuwa na wabunge kwani sheria inamruhusu kufuta chama hata kama kina wabunge 100.

Katika hali ya kushangaza Tendwa ameshauri vyama visubiri nyakati za uchaguzi ndipo vifanye mikutano ya kisiasa.Hata hivyo amekiri sheria inaruhusu vyama kufanya mikutano na maandamano wakati wowote.

Source:Habari Radio Tumaini.

Yaani akijaribu kukifuta CDM hapo ndipo atakapojua Watanzania wakoje hakuna rangi ambayo hataacha kuiona. Huyo anaye mdanganya mwache aendelee kumdanganya tu... Ya Misri na kwingineko yatatokea hapa kwetu!
 
Mmemsahau huyu babu ndiye aliyemruhusu JK afanye kampeni mpaka usiku na kuleta mgogoro na tume ya uchaguzi? anaipenda CCM kwa moyo wake wote na kwa akili zake zote hivyo akiona inachakazwa na CDM hofu humjaa. Nadhani dhamira yetu ya ukombozi na mabadiliko haipo ktk jina CHADEMA au ktk ile bendera bali tunayo ndani ya mioyo yetu na kwene akili zetu tunalala nayo,tunatembea nayo, kila mahali tunayo.

Tusitishwe na vitisho vyenye utapiamlo kama hivi, ana uwezo wa kufuta nguvu ya mabadiliko ktk karatasi tu lkn kwenye akili na mioyo yetu imepigwa chapa na muhuri wa moto mpaka siku ya kufa CCM na hata baada ya hapo kama haki haitatawala.

Lazima wanamageuzi wote tuwe na ngozi ngumu ya kumudu mishale butu inayorushwa na CCM iliyokosa shabaha kutokana na kuongozwa na watu wenye makengeza ya akili.Tusitegemee itatoka kirahisi lakini cha kufurahisha ni lazima itatoka kwa hiari ama kwa shari. Aluta Continua!
 
Haya sasa CDM endeleeni kujitoa fahamu muone mziki wa Tendwa.
 
Karudia tena kushabu alilovuta kipindi kile kule kwenye msiba wa mbunge wa zamani arumeru mashariki. Hizi bange za uzeeni ukichanganya na stress za kuamrishwa na ccm kinachokuja mdomoni unaachia tu. Kuna kiongozi wa cdm alishapewa hizo taarifa kabla.
 
Nashindwa kumuelewa Tendwa, kwamba chama ambacho kitasababisha mauji atakifuta, hapa ndipo ananichanganya sasa, Je, Polisi na cho ni chama, maana hawa ndi wanao fanya mauaji na ushahidi wa kutosha upo. Nitashukuru sana na nitafurahi sana kama watakifuta hiki chama maana kila kukicha kinaua wananchi wasio na hatia.
 
Mimi bado imani yangu inasimamia kuwa; mikutano au hata maandamano ya chadema yanawezekana 100% bila uwepo hata wa mgambo. Tension wanazoleta kwenye mikutano ya chadema wakiwa na mabomu, risasi, mabomu na sare mpya wangepeleka kwa wezi na majambazi.
 
mnitafte niwapeleke kwake. Jirani yangu. Tukamwoneshe nguvu ya uma ilivo.
 
Si walisema ni vyama vya msimu tu! Mbona sasa wanaweweseka na mikutano ya CDM?

Tendwa anataka tuamini kuwa CDM wanafanya 'kampeni' bila kutuambia wanamnadi mgombea gani! Kama ni kampeni za kunadi sera na kutafuta wanachama na kuungwa mkono hiyo si ni sehemu ya kazi ya chama cha siasa?
 
Kwa hiyo ccm nao watasitisha mikutano yao!!
Msajili wa vyama vya siasa nchini John Tendwa amesema sasa amechoka kusikia mauaji kwenye mikutano ya kisiasa ya CHADEMA na atatumia rungu lake kufutia usajili chama chochote kitakachoshindwa kutunza amani ya nchi.

Tendwa amewaambia waandishi wa habari hatishiki na chama chochote kuwa na wabunge kwani sheria inamruhusu kufuta chama hata kama kina wabunge 100.

Katika hali ya kushangaza Tendwa ameshauri vyama visubiri nyakati za uchaguzi ndipo vifanye mikutano ya kisiasa.

Hata hivyo amekiri sheria inaruhusu vyama kufanya mikutano na maandamano wakati wowote.

Source: Habari - Radio Tumaini
 
Huyu mzee haeleweki, asema ataifuta cdm, kwa lipi? Polisi wameua ndani ya ofisi ya chama, unafuta chama? Ama kweli ana macho lakini haoni
 
Hata kama anamamlaka ya kufuta vyama vya siasa, Je ni hoja gani ataitumia kukifuta chadema? mauaji yote yamefanywa na Polisi na silaha zote wanazo polisi, iweje CDM walaumie? .Huwezi weka chumvi kwenye asali halafu lawama umpe nyuki. lawama ziwafikie nyinyi ccm wenye jeshi na silaha.
 
Its true umuri umekwenda sana hana jipya anatakiwe apumzike YUPO KWA SABABU YA PETE ZA MAJINI
Ushirikina una mwsho 2015 wachawi wote mtatupisha
Tendwa1.jpg

Tendwa na pete ya majini

Hii nchi yet wakati mwingine kutofautisha kiadto cha nne asiyejua kusoma na wenye digree zao ni ngumu mno, tunahitaji mitaala ya kipekee naddhani, au jinga wake unapitia kwnye huo mwanya!!!!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom