Tenda ya Bomba la gesi ya Mtwara

mkuu asante kwa kuleta hii hoja. Kuna bandiko hapa kutoka Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu juu ya mpango wa 2010 wa ujenzi wa hili bomba. Umeeleza vizuri sana na gharama halisi lakini katika vitu ambavyo wahenge walitufundisha ni kuwa "ukitaka kusema uongo basi kuwa na kumbukumbu". Serikali hii hii imesahau iliyoyasema na kufanya wizi wa mchana. Wengi wanasema na hili litapita lakini wasisahau kuwa suala la Richmond lilikuwa rahisi hata zaidi ya hili na halikupita japo DOWANS wananyemelea $$$$$$ zao pale hazina!
 

Thanks Bro,kumbe wakati mwingine unawaza vizuri,heshima inaanza kurudi taratibu
 
Wazushi ni wengi sana humu jamvini

Heshima yako mkuu, sisi tumekwisha timiza wajibu wetu kama wazalendo, uzuri Watanzania wengi ni wepesi ku-grasp mambo wakielimishwa vizuri, watakaa chini wa-digest tahadhali zote tulizo hanika humu. At the end of the DAY watapata picha kamili ni kitu gani kinajili behind the scene. God bless U mkuu.
 

Mkuu I can't disagree with you kwenye dunia ya leo ni vigumu kuibiwa bila kujijua ni Chief Mangungo tu na wenzake wa enzi hizo ndo waliibiwa hivyo otherwise kila wizi unaofanyika humu nchini lazima ufanywe kwa ridhaa ya viongozi wetu wasiokua na uzalendo hapo wanaotuibia sio wachina bali ni viongozi wetu na ndio maana ukiongelea swala la huu mradi wanakua wakali kama simba kwa mradi wa Pakistan kwa mfano utaona tofauti kubwa sana ya bei kule bei ni wastani wa 1.2M usd per mile na bomba lao ni la kipenyo kikubwa na linapitia kwenye maeneo magumu kijiografria wakati sisi huku linapita mchangani tu na ni almost 3M usd per mile huu ni wizi wa wazi kabisa na unaweza kuta wachina walitoa genuine estimates lakini wakubwa hapa wakaweka cha juu kama kwenye mradi wa upanuzi wa bandari
 


Nyinyi ndiyo mmevunja utaratibu ambao ungetoa hayo majibu. Kwa hiyo unathibitisha mradi huu ni wa mfukoni ndiyo maana ni siri, ndiyo maana kuna maswali yasiyo na majibu. Nchi hii chini ya utawala wa CCM ni hovyo kabisa.
 

miKATABA YA PAKISTANI haiwezi kuwa sawa na yetu inayo fichwa kana kwmba imeandikwa kwenye nyeti za mkuu fulani,na Pakistani itakuwa bomba linakotoka wanachi pale wana mrahaba wao wa kuwanufaisha na si POROJO kama za kina MUHOGO,laa yawezekana nao wamefanya ujinga pia lakini hayo ni yao na ujinga ni wao kama wamefanya hivyo sisi lazima tuangalie maslahi ya wahusika.
 
Naomba kutumia model ya ile Tenda ya Bandari
Sasa ni zamu ya TPDC.

Pasco.

Ahsante kwa majibu ya Ukweli

Nina imani Pasco utanijibu swali langu moja tu.

Baada ya hayo yote kujibiwa kama ulivyojibu Je TAKUKURU hawana uwezo wa kuhoji ukiukwaji mkubwa wa taratibu za manunuzi kama kama huu ulivyofanywa?
 

Amen Mkuu
 
mkuu sasa naona unafika mbali, yaani unaanza kuingilia 10% za watu eeee. haya mzee endelea...
 


Mkuu najua waswahili ndio walio bobea katika nyanja za ku-doctor figures na kuongeza vitu chungu mzima vya uongo na kweli katika miradi ya kitaifa. Wachina wakishugulikia mradi huu wa GESI basi kwetu hiyo itakuwa a golden chance ya kuwakamata with their pants down culprits wote walio kubuhu katika mchezo huu wa ufisadi na wizi wa mchana; kama kutakuwepo ushahidi wa kweli wa ufujaji wa fedha zilizo tolewa na Serikali ya Kichina kusaidia ujenzi wa mabomba ya gesi - nakwambia nchi haitakalika.


Kwa nini nasema hivyo:
(a) Wachina hawana utani na wala RUSHWA kama wakipata taarifa ya kuaminika kuhusu wizi watachukua hatua mara moja bila ya kujali cheo/ushikaji na undugu, watapokea kwa mikono miwili taarifa yoyote bila ya kujali mtoa taarifa anatoka Serikalini au ni raia wa kawaida kutoka Taifa lolote lenye miradi inayo gharimiwa na Wachina.


(b) Wachina wanagharimia mradi wote kwa pesa yao waliotoa kama mkopo, hivyo hawawezi kuvumilia watu wajanja kutafuna hela zao bila ya kujali kama wezi ni Waswahili wa hapa hapa au Wachina wenzao.


(c) Kama ubadhilifu wa funds za mradi wa Kichina ukiwa proven - basi wahusika wa pande zote watatiwa mbaroni, upande wa China watapigwa risasi kwa upande wa Tanzania Serikali yetu italazimishwa kuwachukulia hatua kali na kutangaza majina ya wahisika adhalani, Wachina hawawezi ku-treat kwa SIRI swala la ufisadi/wizi wa funds zao.


Sasa nini cha kufanya: Tuwaache Wachina watujengee mradi huu muhimu Kitaifa mpaka mwisho, wakisha maliza na kwa bahati nzuri wametupa a long grace period kabla ya kuhanza kurudisha mkopo wao, basi muda huo utatupatia nafasi ya kuwahoji Wachina waeleze kwa nini gharama za mradi unaofanana na hule wa Paskistani lakini kwetu unaonekana gharama zimekuwa kubwa wakati kipenyo cha bomba ni kidogo ukilinganisha na bomba zilizo pelekwa Pakistan, gharama za kutandaza bomba per kilometer kwetu zinaonekana zimezidi wakati geological formation ya Pakistani na Pwani ya Tanzania kuna tofauti kubwa kwa hiyo kwa akili za kawaida gharama za utandikaji wa mabomba unatakiwa huwe chini zaidi hapa kwetu and not the other way around. Serikali ya Kichina ikipewa maswali kama haya basi watalazimika kufatalia what WENT WRONG na ku-apprehend wahusika wakuu kirahisi na bila huruma.
 
Nadhani mkataba ulisainiwa chumbani somewhere huko China kwenye lijihoteli.
Sasa sijui wanaume wazima wasaini mikataba kwa usiri vyumbani huko ugenini!
Makalio yao yalisalimika kweli????[wamefanyiwa mchezo mbaya hao hawakusalimika wameliwa utamu
 
Ahsante kwa majibu ya Ukweli

Nina imani Pasco utanijibu swali langu moja tu.

Baada ya hayo yote kujibiwa kama ulivyojibu Je TAKUKURU hawana uwezo wa kuhoji ukiukwaji mkubwa wa taratibu za manunuzi kama kama huu ulivyofanywa?
.
Kwani kwenye Richmond, TAKUKURU walisema nini?, vivyo hivyo kwa Gulf Stream, BAE radar na sasa bombo la gesi!.
Kama umebahatia kuwajua the real people behind Richmond, they are the same, "big fish", hicho
Kitakukuru ni nini, ni kama ukucha tuu kwenye kidole!.
Pasco.
 
Nadhani hapa lawama msiwape wachina,mbona hatuoni wachina wakileta ujinga Zimbambwe? tujilaumu wenyewe,sisi watanzania kwa kupenda njia za mikato ktk kufanya mambo yetu.
na kuhusu pesa za mikopo hususani hii mikopo kutoka nchi mbalimbali,wao huja na masharti yao na kwa mfano moja ya sharti waliloliweka kuhusu mradi wetu wa gesi ilikuwa ni kuuza gesi nje ya Tanzania,serikali ililikataa hili,kwa hiyo si kila masharti wanayotuwekea tunayakubari hapana,yapo yanayokubalika na yapo yasiyokubalika,kwa mfano kuhusu wakandarasi ni kawaida kuwatumia wakandarasi wa nchi husika maana hii itasaidia mradi kufanywa kwa kiwango na ubora unaotakiwa na tukumbuke kuwa Tanzania bado hatuna wakandarasi wenye uwezo wa kufanya miradi mikubwa kama hiyo,mfano mnzuri ni hizi shule za kata,wamatumika wakandarasi wa ndani kufanya kazi hiyo,nandeni mashuleni na mtajionea nyufa kwa madarasa yaliyojengwa ndani ya miezi 6 iliyopita.
hata kama serikali ingeongozwa na chama chochote kile pinzani,isnge kubali miradi iliyokopewa pesa nyingi zitakazolipwa na kodi ya wananchi kuharibiwa kwa kupewa mkandarasi aliyeshindwa kujenga shule zetu za kata.ila nacho kielewa mimi kuna kazi wakandarasi wetu wa ndani hupewa kupitia miradi mikubwa kama hii ya gesi na barabara.
 
Tenda ya Bomba la gesi ya Mtwara
1. Ilitangazwa lini
2. Consultant alikuwa nani?
3. Estimates zake zinasemaje?
4. Tenda ilitangazwa na idara zipi za
serikali?
5. Kampuni ngapi ziliomba hiyo
tenda?
6. Majina ya hizo kampuni
zilizoomba yako wapi?
7. Evaluation team ya hiyo tender
ilihusisha akina nani?
8. Pre qualification stage zilipita
kampuni ngapi?
9. Zilizoshindwa zilitolewa kwa
vigezo vipi?
10. Technical specs za huu mradi ni
zipi?
11. Financial specs za huu mradi
mbona siri kubwa?
12. Je kampuni ngapi za wana
Mtwara zilihusishwa hata kwenye
sub contracting?
13. Je, Mtwara Development Agency
WALIHUSISHWAJE KWENYE HUU
MPANGO?
14. Hizi TUHUMA za watu kula pesa
China ni kweli?
 
Very essential questions, on a serious note, unafaa kuwa mbunge!!!
 
maswali mazuri ila sasa yapo sehemu ambayo sidhani kama kuna atakae kuwa anamajibu ya kuridhisha........
 
Kwa ufupi kama mnakumbuka ilikuwa tugawane na mwekezaji 50% to 50% cha ajabu baada ya mtoto wa mfalme kukamatwa condition zimebadilika ni Wadanganyika tutapata 20% na mchina anapata 80% na ndivyo Jk alivyosainishana kumwokoa Prince
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…