Mkuu nafikili unaelewa kinacho endelea kati ya mataifa ya Magharibi na Uchina - vita hii ndio inaendelea katika mradi huu, wanaweza kusema chochote cha kuwazulia Wachina as if na wenyewe hawahusiki na vices wanazo watuhumu Wachina!! Ingechukuwa muda gani kupata mkopo kutoka nchi za magharibi ambazo hali yao ya kifedha si nzuri, wangetoa mashariti gani; je kampuni ya magharibi inayohusika kusafirisha GESI kwa njia ya bomba kutoka Kilwa unataka kunieleza hiko clean sio kwamba ilikuwa inachezea TAIFA letu kwa kubadilisha badilisha tariff za GESI wakati mwingine kuifunga kabisa kwa visingizio vya kila aina, Je TANESCO ilikuwa inalipa kiasi gani cha fedha kwa mwezi kwa kampuni hii ya kinyonyaji ambayo ilikuwa imepania kuzima ushindani wa kibiashara katika usafirishaji wa gesi nchini, walikuwa wanataka wabaki wao tu! - hilo mbona amlisemi, mnawashambulia Wachina tu.We unafikili kwa nini Serikali iliwashtukia kampuni hii kutokana na umangameza wao, Serikali ilikata shauri la kaomba msaada kutoka kwa Wachina ili wasaidie kujenga a parallel bomba kumaliza ukiritimba huu ambao ulikuwa umekubuhu! Nini kijili walipo pata habari kwamba Wachina wanakuja kujenga Bomba mbadala, walilalamika sana si hilo tu walishirikisha World Bank ili wakwamishe Wachina kwa kutoa visingizio vya kubuni tu - hata wafadhili wanao changia bajeti ya TAIFA letu waka jump kwenye bandwagon la kuwasema vibaya Wachina - wote hao i.e World Bank, Wafadhili lao moja i.e kupiga vita Wachina.Mwanzo nilifikili malumbano haya labda yanasukumwa na mambo ya partisian lakini baada ya kulichunguza kwa umakini naona si kweli. Kwa nini tuone ajabu Wachina kufanya kila kitu, kwani ujenzi wa TAZARA walishirikisha mataifa gani? Hapa nimeuliza mbona Projects karibu zote zanazo husu Japan nchini mwetu, Wajapan ndio ufanya kila kitu na sijawahi kusikia malalamiko kuhusu hilo - why pick on Chinese!