Nimekuwa nikiambiwa na jamaa zangu kuwa nikienda benki sasa hivi niwe na tabia ya kuhesabu pesa zangu kabla ya kuondoka pale dirishani kwani wale 'Tellers' wamekuwa na mtindo wa kuchomoa pesa hususan kwenye bundle za 1m.
Nilikuwa siamini lakini leo yamenikuta Equity Bank,pale Golden Jubelee branch. Yule Dada alikuwa anahesabu pesa kwa ile mashine ambayo anayo ndani na wakati anahesabu kwa machine wala sikutia mashaka kwa hiyo sikuona hata namba za kwenye mashine inavyohesabu na akimaliza anazifunga kwa 'rubber band'.
Alinipa pesa zangu na akaniaga vizuri tu.Nimefika nyumbani nimehesabu Bundle moja limefungwa kama milioni moja lina Tsh 930,000 tu na lingine kama hilo lina Tsh. 800,000 tu. Nimesikitika kwa kweli kwani sikutegemea ushenzi kama huu kufanywa waziwazi na mfanyakazi aliyeaminiwa na Benki.
Sasa mimi najiuliza kama ingetokea nimehesabu palepale nikagundua upungufu huo yule Dada angekuwa na hatma gani kwani nisingekubali yaishie hqpo.Ni Mungu tu ameamua kumuhifadhi. Lakini pamoja na Mungu kumuhifadhi inabidi uongozi wa Benki ulitizane jambo hili la aibu.
Vilevile hata kwa Mabenki mengine kama kuna mambo kama haya yamulikwe na yasipate nafasi kwani yanaharibu sifa za Kibenki ,nkiamini kuwa wizi huu ni wa mfanyakazi mmoja mmoja na sio wa mtandao ndani ya Benki.
Nduguzanguni tuwe makini zaidi pale tunapokwenda benki kuchukua pesa.Hali ya sasa siyo.