Hili chaweza kuwa kitu kigeni mno masikioni mwa wengi lakini ni kitu kilichopo Katika Ulimwengu huu
Telekinesis ni hali ya kuwa na uwezo na nguvu za kiasili za kuweza kunyanyua na kusogeza vitu kwa viungo vya mwili hasa mikono bila kuvigusa
View attachment 299478
Telekinesis ni tendo la psychic ambalo ambalo uwezo wake ni uleule wa kusogeza vitu na kuvihamisha bila kuvigusa-psychokinesis
Sasa hiajalishi kama ni telekinesis au psychokinesis lakini matendo yote haya mawili ni sehemu mojawapo ambayo kisayansi bado yanaacha maswali mengi huku baadhi ya watu Katika tafiti na mabandiko yao wakizihusisha a nguvu za giza
Lakini ukweli ni kwamba mind/ufahamu wa binadamu ni kitu chenye nguvu mno na kwakweli tunachotumia ni sehemu ndogo tu ya nguvu ya ufahamu wote tukio nao... Kidini hasa katika Biblia takatifu hii nguvu inaitwa imani, na tunaambiwa ukiwa na imani ndogo tu isiyozidi ukubwa wa chembe ya haradali utakuwa na uwezo hata wa kuhamisha milima... Hii imani katika Bible ndio telekinesis kwa upande mwingine
Sasa watu hujaribu kumiliki hizi nguvu kwa njia ya mkato au ya kujituma na kupractice, tunapoongelea mambo ya meditation, psychic powers n abilities yoga astral practice nk kimsingi Tunaongelea telekinesis katika secondary stage, baada ya kuchanganya na maarifa mengine Kama hayo
Lakini pia kuna wale ambao hupenda kumiliki nguvu za telekinesis kwa njia za mkato na hapa ndipo watu huingia mikataba na kuzimu na kufanya makafara huku wengi wakiingizwa kwenye dini ya mashetani ili tu aweze kufanya mambo kama hayo
Siku hizi tuna manabii na mitume wengi wanaofanya miujiza mingi hasa ile ya kuwapuliza tu watu na watu hao kuanguka au kunyoosha tu mkono au kidole na nguvu yake kuwaangusha watu.... Msidanganyike ile si nguvu ya kiMungu bali ni aina fulani ya nguvu za kitelekinesis na ki psychokinesis zilizochakachuliwa na mwishowe kuchomekea jina la Yesu kristo kupumbaza watu
Tuna waganga wa kienyeji pia wenye hizi nguvu, lakini huchanganya na mambo mengine ya giza na kuweza kuwapumbaza na kuwarubuni maelfu kwa maelfu
Telekinesis ya kiasili na isiyochakachuliwa haina madhara zaidi ya mtu mwenye hizi nguvu kuweza kufanya maajabu ya kusogeza vitu bila kuvigusa.... Dunia bado ina mengi na mengi bado hatuyajui... Usiunyime ufahamu wako maarifa bado kuna mengi huyajui
Telekinesia...
Ni finomena inayofungamana na maumbo -- maumbo, akili na nia. Mara nyingi mashauri ya hili huangukia uchunguzi, utafiti wa yale yanayotajwa kama 'yapitayo kawaida'; ya kikuu juu ya asili... Lakini ni vema kukumbuka 'Kikuu juu ya asili' labda bado ni asili -- tusiyoijua namna yake.
Kuna mengi yenye kujinasibu na 'akili' zetu lakini hatujui na mawezekano yaliyonasi wakati wote; labda ni baada ya kuwa katika mazingira fulani ama kupitia mafunzo fulani hayo huanza kudhahirika na kudhihirika namna zake.
Miongoni mwa jamii ambazo kumekuwa na jamii na mapokeo ya vitendo vya kiimani -- kujinasibu na 'kujitambua nafsi' ama kuwa 'masiha/avatara/bodhisatva' ama 'kutaamulika kibuddha'; mengi hufahamika juu ya mapitio katika 'safari ya kiroho'... Ishara na uweza zaidi, ujao na mtu mwenye kudumu katika jitihada za kufikia 'sifa' na 'hadhi' mpya za 'kuwa' na 'kufanyika' -- Uzaliwa Upya...
Yoga kwa mfano, si dini -- ni mfumo wa mfululizo wa vitendo vyenye kusaidia na kuwezesha mtu afanyike 'kamili'... Kamili ki'aje? Kwa mujibu wa Yoga, mtu ni daraja la chini -- ama la msingi kwa huyo kuwezekana 'kuzinduka' zaidi. Vitendo vya Yoga ni njia mahsusi kulingana kusudi lake la 'kumzindua' mtu kwa sura moja hadi ingine -- lakini kilele cha yote ni 'Mtu kujijua Nafsi yake Kuu'...
Nafsi ya mtu ipo ndani ya 'nafsi ingine'; kuzinduka kiyoga ni kuamka hadi ngazi ya nafsi ingine -- ile yenye 'kusitiri' ya mwanzo. Kadri mtu azindukapo, yapo mambo kadhaa zaidi yanayoweza kujitokeza katika yule mwenye kudumu katika nidhamu ya Kiyoga. Sasa, kupitia Yoga mtu huzinduka na kuanza kuwa ni 'mmoja' na zile nguvu ambazo awali hakudhani ama kushtukia kuwepo -- kuwa ni zenye 'kutia' nguvu nasibu ya maisha yake ya kimwili, kihisia na uweza zaidi -- kile tunachoweza kusema kuwa uzima zaidi wa kiroho...
Kusudi la Yoga ni kufikia 'fahari' ya kiroho ili kuwa kwamba mtu 'amekombolewa' -- amekombolewa kutoka katika ile nafsi isiyozidi kheri za kimwili tu na milango yake ya fahamu. Kwa hivyo kilele cha Yoga ni Ufunuo kamili juu na 'nafsi' na 'akili'... Kwa kuwa nafsi ya msingi ya mtu ni zao la mwili na milango ya fahamu, Yoga huanza na mazoezi ya mwili wenyewe, katika kuingiliana na akili... Milango ya fahamu ikianza kunasibishwa na jambo tunaloweza kulibatiza kwa kiswahili ni tendo la 'miditisha'...
Miditisha kulingana na Yoga huja kwa jitihada na nidhamu mbalimbali -- yaweza kuwa baada ya mwili kuweza kumudu kutulia kabisa, namna isivyosumbuna na akili -- basi akili kubaki huru kufanyikia mafunzo mahsusi yenye kufungamana na nguvu yenyewe hasa -- ile yenye kuhuisha na kuhaisha yote : Nuru ya Ufahamu.... Kwa hivyo kwa namna za Yoga, kuna za namna mbalimbali kama vile vitendo vya kukazia fahamu kwenye 'kitu', 'jambo', 'alama' ama 'neno' -- kulingana na ufundi wa 'kuifua akili' ili kuja kuwa 'daraja' -- kwa mambo zaidi ya kazi yake hii ya kawaida ya kuchakata fikra, mawazo na hisia.
Yoga ni mbinu, kadri ya ufundi wake, njia zake huja na mambo tofauti na matunda tofauti ; lakini la juu zaidi ni Kuamka katika nafsi ya kweli kuishia kujua na kuziishi kudra na kheri zenye kudumu zaidi kuliko mapana ya hata uhai wa mwili. Na basi vivyo hivyo Matunda ya Yoga yanaweza 'kumfuata' mtu hata baada ya yeye kufa kimwili... Mtu kuzaliwa na vipawa 'visivyo vya kawaida' ; ambapo ni vigumu asiyefahamu mambo ya 'kiroho' kubaini ukweli wake...
Yoga ya mtu huzaa matunda hata kwa mapana ya kuishi zaidi ya 'isho' moja... Safari ya mtu kuamka kiroho si jambo muda mfupi, kulingana na namna za Yoga na mambo yake -- safari ya mtu yaweza kukamilika kwa 'isho' na 'isho' katika jitihada za kujinasibu kuamka... Na basi Yoga ni sehemu ya muktadha wa watu kuzaliwa na wito zaidi wa 'kiroho' na kiimani mara nyingi zaidi kuliko kawaida. Lakini kila mtu ni msafiri wa kiroho, kwa kujua hata kutokujua -- Yoga huharakisha safari ya mtu katika kuamka kiroho; na basi kuwa ni 'kitovu' na 'chachu' ya umma mwingine wa wale waelekeao 'ukombozi' kamili... Kwa walimu wa Yoga husema safari ya mtu, kwa hatua kawaida, yaweza kupata 'mamilioni' ya miaka ya hapa duniani... Na hivyo hatma ya sisi viumbe kama watu ni 'ukombozi' -- kuja kufanyika 'kiumbe kipya' siku moja mbele ya wakati... Japo kwa namna isiyo ya kawaida kimafikra na mantiki, linalowezekana 'kesho', lawezekana 'leo' na hata 'jana' lilikuwa ni lenye kuwezekana; Yoga ni siri ya kufumbuka na jaala ya viumbe vyote kiwakati na nasibu zake zote za kufanyika na kuendelea... Yoga ni kutaniko ama unganiko la mtu na ile 'Nafsi' yenye kudumu zaidi -- yenye kuwa pamoja na nafsi nyingine zote za namna zote za viumbe -- mimea, wanyama, sayari, majua, falaki na ulimwengu wote mzima... kadri ya vyote vyenye kuonekana na vile visivyonekana. Yote ni Moja.
Telekinesia ni moja ya mawezekano yaliyokatika madaraja ya chini kabisa ya safari ya kiroho, kujifunua kwa mtu anayejinasibu na mwingiliano wa akili na maumbo... Hili lidhihirikapo katika mtu ni hakika ya kwamba kudhani kwako kama vile kusema : labda akili yako na vingine vinavyokuzunguka ni utengano ni si kweli hasa... Basi akili yako si kwamba yafanya kazi ndani yako tu -- ya fanya kazi hata nje yako...
Yapo mengi tukianza kuvutika kuyajua na kuyafuatilia, tutakoma kujichukulia ukweli wa nafsi zetu kwa kufungamanisha na ukomo wa uweza. Katika Yoga kumekuwa ni miiko ya kutojifurahisha na mambo yajayo ukomavu wa mazoezi ya Kiyoga yenyewe; kwa nini? sababu ni rahisi -- mtu yeyote ambaye 'atajifurahisha na haya' safari yake yaweza kukoma mahala; na halafu anaweza kujifunga na kile kinachokinza safari ya mtu kuelekwa 'wokovu' wa nafsi -- Karma... Kwa hiyo, ni vema mtu kujichunguza 'matamanio' yake na haja zake zinazoweza kumletea mkingamo.
Kwa wale ambao wamepata kusoma na kusikia habari za Yesu, kulikuwa na vitatu vikuu vya majaribu ya yeye katika kumamiliza safari yake ya kiroho na 'kuamua kutumikia' -- na basi Yoga ni vivyo hivyo kwa Yoga yenyewe hasa. Wote, Wasafiri Kiroho, hufika mahala, tunajaribika kwa 'matatu'...
Mimi kama mtu ninapenda na niko tayari kuzungumza sura za hayo ya njiani, lakini ninajiasa nafsi yangu na ya ninyi ndugu ndugu zangu -- msijekubabaika ama kuhadaika na ya katikati ya safari ama ukingoni... Kadri inavyofaa, nitakuwa ninajinasibu kueleza ni namna gani 'uwezekano usio wa kawaida' katika safari yako ya kiroho yaweza kuzaa Karma mbaya; na kwa namna gani ya kufanania... Tukumbuke, tukiwa safarini twatazamia kufika na si kuikatisha safari. Kama hili ni uhakika kabisa katika mtu, basi upo uhuru hata kufunua kwa mtu muktadha wa mambo ambayo yanaweza kumpeleka yeye katika mawezekano hayo, kwa imani kwamba hayataishia kuwa ni 'mtego' kwake...
Hmmm...
++++++
....
Labda ni India tu ambapo utamaduni wa mapokeo ya 'kinadharia' daima yamechuana sambamba na mapokeo ya moja kwa moja ya kutoka kwa wale walioitambua na kuiishi kweli wakati hata wakati. Ni katika hili ndio Vedanta ilikuja kujitokeza kama ukamilisho wa veda kulingana na jitihada za wale waliobaini kweli fulani na toka kwenye ile kweli kujaribu kuzungumzia veda kwa sura bora na yenye msingi imara siyo mapokeo tu ya mdomo ama maandishi. Pia ndiyo kuendeleza utamaduni wa
Upanishad... Yale ambayo watu walijifunza miguuni pa waliotaamulika ama kufunguka kiakili. Ndiyo hivi waliopata kutokea kwenye hata jamii za Kihindu kama Gautama Buddha aliyefahamika awali kama Siddhartha Mshakya; waliweza kufundisha mafundisho mapya yaliyotegemeana na kufunguka kwa fahamu zao na ufahamu wa yote. Tokea kwake yalikuja mapokeo ya U-Buddha yaliyojikita katika mtindo wenye kufahamika toka siku zake kama njia ya Buddha-dhammapada. Hii ni kuweka alama juu ya tofauti ya mapokeo ya kifikra yanayoridhiwa kama habari tupu; kuyatofautisha na yale mapokeo yanayolenga kumletea mtu mwongozo katika njia ya mabadiliko halisi ili kweli aishuhudiayo mtu kuwa ni moja na kweli aliyofanyikia upya mtu mwenyewe. Si Buddha pekee yake aliyefundisha mafunzo ya mabadiliko ya moja kwa moja ya kiutu; wapo wengine wengi walifanya hivyo hivyo kwa namna zao za kipekee na huku wengine wakikumbukwa na wengine kuwa kana wameshahaulika. Wapo walimu na wanasayansi wa zamani kama yule mwalimu mkuu wa
Yoga Hatha, Patanjali, aliyefundisha mbinu za mikao, utulivu na ukimya wa kiakili na kimwili vinavyoweza kuleta utangamano wenye kutaamulisha akili ya mtu hata kuinukia na kufika katika ufahamu wa 'Kweli' na 'Nguvu' iliyofanyikia ulimwengu wote... Yupo Krishna aliyefundisha
Yoga Bhakti-Yoga ya wanaojitoa moyo wote kwa Kweli ya Krishna iliyo ni Kweli ya ulimwengu wote mzima katika fahari yake iliyofichika mbele za macho ya watu waliokosa mwongozo ili kuona; na hivi kupitia
Yoga Bhakti wanaweza kufunguka na kuwa moja na hiyo... Japo mafundisho ya Buddha ndiyo yamekuja kutawala sehemu mbali mbali za India na nje ya mipaka yake na huku yakionekana kuchepuka kutoka kwenye mapokeo ya awali ya kihindu na utamaduni mzima wa kiveda. Na haya pia kuwa mahususi kwa wale wenye kupenda na kutaka kuongoka hadi katika 'Kweli' iliyo ni muktadha wa Ufahamu mkuu wa Hekima na Huruma juu ya masumbuko ya mwanadamu katika zama zote anazoishi na ujinga wa kutotambua asili ya 'Buddha' ndani yao wenyewe...
Haya yote ni mwaliko wa kuingia katika kutambua kuwa daima kumekuwa na misimamo ya aina mbili katika kushika nia juu ya mtu kufuata mkondo wa 'mafundisho' matupu ama mafundisho yaliyo ni taa yenye kumuongoza mtu katika hata ile kweli itakayommeza yeye mzima mzima na kumwezesha yeye kuzaliwa mara ya pili katika 'Kweli'. Ni sehemu ya hili la pili ambapo Plato na baadhi ya wanafilosofia wakiyunani walikuwa wakilitambua lakini walijua hakuna 'lugha' hasa ya kueleza ufasaha wa yote yanayodhahirika. Ilikuwa ni jitihada yao kujaribu kudadavua mashauri ya watu na ustaarabu wao katika kuingiliana na lile 'lisiloelezeka'. Kwa hilo ambalo halielezeki wao walijaribu kutambua kanuni na taratibu zinazoongoza yote yafanyikayo; japo wapo ambao walianza kutotea kwa ujumla katika mashauri ya kueleza 'siri' za ulimwengu wa maumbo na 'asili' yake. Ndivyo falsafa ilivyozaliwa japo hata kwa wayunani si kuwa ndiko pekee jitihada kama hizo zimepata kufanyika... Kutoka Bara Hindi kumepata kuwa na jitihada kama za wayunani hata kipindi kirefu kabla ya siku za akina Plato na Aristotle.
Tutaendelea kuchambua mengine katika kisomo rasmi cha utatu na wawezekano ya kuupangilia upya ustawi na tamaduni za watu ili kuendana na visomo vya leo na mawezekano ya neema zaidi.
https://www.facebook.com/notes/10150299968989421/
+++++
Mawasiliano angani ni jiwe la msingi katika hatua za ustawi na maendeleo ya mwanadamu. Ni ishara ya mengine mengi yatakayofuatia na hata kubadilisha sura ya jamii yote na mustakhabari wake. Si tu kimawasiliano na uchukuzi peke yake bali pia katika muktadha wa unyambuliko wa kiutu.
Maendeleo makubwa ya ulimwengu wa leo wa habari ni matunda ya '
uelektronishi wa kimawasiliano'; na katika huu tunashuhudia mwanzo wa mwanadamu 'kuvuna' mawezekano yaliyo katika uwazi wa nafasi na mbingu. Kutuma ujumbe/habari hata mahala pa mbali na hivi pia kuletewa 'habari' yoyote yenye mapenzi mema ndiyo mwanadamu--hata kabla ya huu uwezekano alipatwa na njozi na maono ya mfano wa 'malaika'. Yeye aliliona hili kwa jinsi ya mtu mwenye mbawa, arukaye hata mbawa na hivi mwenye kuzidi kadiri za umbali na kasi ilikutokea. Na yeye alilichukulia hili kama mfadhiliko kwa ujumbe kati ya mtu na Mungu na kwa nia njema. Lakini hii pia ni akitipu muhimu kuelewa jinsi ilivyojichimbia ndani sana ya
fahamu mbalali iliyozama kwa kiasi chake ndani ya
utofahamu kumbaizi. Kutoka katika
utofahamu kumbaizi,
fahamu mbalali ya mwanadamu ilipitisha 'ujumbe' kwa '
fahamu jua' ya mtu iliyowakilishwa kwa sura ya 'mtokezo wa malaika'. Malaika ni daraja ambalo binadamu vile vile amepata ufunuo wa hata yale yasiyokuwepo katika jamii yake kufahamika.
Binadamu hana uwezo wa kumaizi ukweli ulio ni dhahania mno; na hivi ufunguko wake hufanyika kuja kwa muktadha wa namna ya kipekee. Wakati mwingine huo huhitaji daraja lenye kumaizika sura ya upokezi wa 'taarifa/ujumbe/maaria' kuufaa '
ufahamu jua' wake. Ni kama vile kusema binadamu hawezi kuielewa lugha ngeni mpaka pale yale maneno ya lugha ngeni yamekuwa ndani ya fahamu yake kawaida ambayo ndiyo
ufahamu jua. Ili kung'amua habari/ujumbe wowote kwa wakati binadamu hushughulika na upande wake wa ufahamu ulio ni
ufahamu jua.
Uwezo wowote ambao unaweza kupitiliza
ufahamu jua ili kung'amua habari; huo unaleta mashauri ya '
Paranomo' ya utambuzi kwa mwanadamu; huu pia ni uwezekano lakini usio wa kawaida sana miongoni mwa watu wengi; mara nyingine kujitokeza katika kulingana na mazingira fulani.
Paranomo ndiyo yaweza kuhusisha hisia za kiakili zijitokezazo zaidi ya zile za milango ya kawaida ya fahamu kwa mtu na tena zenye kiasi chake cha usahihi kiutambuzi.
Ufahamu jua katika hali ya kawaida hukamilisha kitendo cha utambuzi kwa kukutanisha hisia pokezi za kimwili, kumbukumbu na fikra/mashauri ya akilini.
Paranomo hutanua hisia pokezi kutoka zile zilizomwilini mwa mtu na hata zaidi ya hizo-hali pia isivyo ni moja kwa moja.
Muktadha mintarafu paranomo unapohusisha ile jinsi ambavyo 'vifungu' ama 'uzi wa habari' ama pia namna ya ushawishi wenye kuweza kutoka kwenye wigo wa akili ya mtu mmoja hadi mazingira yake ya nje na kinyume chake pasipo zile jitihada za kimwili, kama vile kutamka na kutenda, ila tu kwa nguvu ya nia na akili tupu ndiyo ugani hasa wa chenye kuweza kutajwa ni '
Saikia'. Na vile vile yaweza kusemwa mambo ya Paranomo ni vipawa vya
Saikia. Mawezekano ndani ya
Saikia ya mwanadamu ni pamoja na kitendo chenyewe cha ufikirivu na utambuzi uendenao na kumbukumbu ama kuzidi mipaka ya kawaida na hivi kuhusisha
ukionambali, usikiambali, uelewambali na
uisharifu. Haya ndiyo katika mashauri ya kiingereza hutajwa ni 'clairvoyance', 'clairaudience', 'clairsentience' na 'intuition'.
Saikiakwa minajili ya vipawa vya akili ndiyo hutajwa katika mashauri ya kiingereza ni 'Psychic'. Msimamo mzima wa mtu kiakili kwa wakati ni
Saikia ya mtu; 'Psyche' katika mashauri ya kiingereza.
Nuru ya Ufahamu, utambuzi na kumbukumbu ndiyo husokota nyuzi zote za msuko wa UTU na 'ujifahamuko'; ndani ya wigo wa
Ufahamu Jua wa mtu. Utambuzi ni mfungamano wa Fikra na Hisia kwa kila urajisi wa neno ama tendo ndani ya
Saikia ya mtu na kumbukumbu lake lote katika
ufahamu jua-kwa nukta ya wakati wowote. Kwa kuwa hisia zote ni jinsi ya kimiminika kama ilivyo kwa 'maji'; fikra ni kama 'barafu' katika bahari ya ufahamu kamili. Kwa jinsi ya mchanganyo wa 'joto' na 'baridi' binadamu anaweza kufanya matone ya 'barafu' za mafikara. Nayo matone ya barafu yaweza kuja kufanya mabonge juu ya uso wa 'ujifahamu' wa mtu na pia chini; katika kuelea kwenye mapana ya bahari inayowezekanisha mabonge yote. Basi kwa mfano huu, ni miale ya Nuru ya Ufahamu yenye kumjalia mwanadamu uwezo wa 'kusababisha' hali ya joto ama baridi ili kurajisi jinsi ya mafikara yote katika madhahirisho katika utumikivu wa kumbukumbu lake na 'kujiona' katika kioo chake cha utu.
Kwa kadri mtu anavyojifahamu na kwa minajili ya kumbukumbu yeye atazidi kujisokotesha nyuzi za maisha yake kwa msingi wa mafikara yake. Maisha kwa jinsi yake; huakisi kile mtu akitendacho kwa matokeo yajayo kwa mujibu wa kanuni za maumbile. Kwa jinsi ya mizunguko na majira kila fikara ama neno ambalo mwanadamu hukirimu haja ili kudhahirika--kwa kukusudia ama kutokukusudia; hilo huja kuchukua sura kwa nguvu za kimaumbile. Kuna vile vitu ambavyo mwanadamu hupanda kwa nje kwenye mazingira yake na basi pale majira sahihi yanapowadia yeye huvuna kutokana na kile alichokipanda. Kuna vile ambavyo hata pasipo kutambua jinsi atendavyo nje ndivyo vile apandapo ndani katika
ufahamu mbalali; hivi navyo hubaki kuwa ni ushawishi wa kichinichini utakaokuja kumtia mtu kwenye uwanja wa mavuno ya jinsi yake. Mawazo yote na mafikara ya mtu ni mbegu katika gurudumu la wakati. Majira sahihi yafikapo binadamu huvuna matokeo ya faida ama hasara kwa mawazo yake yote. Kwa kuwa mawazo ni vizio vya nia-utu kulingana na fikra na hisia za mtu mwenyewe; hivi ni kama vipande vya sumaku inayovuta ama kuvutika katika mazingira ya jinsi yake ili kufiti sura na maumbo.
Haba na haba hujaza kibaba ndiyo kanuni inayotawala misukumo ya mikondo midogo midogo kuweza kuunganika na kufanya msuko mmoja mkubwa na wenye nguvu ya jumla ya yote na mwelekeo mmoja uliodhahiri. Kila msukumo wa wazo ndani ya mwanadamu ni wenye kupanda hatia ama uhuru katika muktadha wa haki wa kanuni za maumbile. Wakati ndiyo huhukumu yote kwa nguvu zilizofanyikia katika maumbile yake na madhahirisho. Mkusanyiko wa mawazo ya jinsi ya uharibifu ama uharibiko yatamvuta mtu katika mazingira ya uharibifu na matunda yake. Mkusanyiko wa mawazo yenye ujenzi yatamsukuma mtu katika kiu ya kuunda na kutanua ustawi wake. Panapostahili stahili ujenzi binadamu akiwa na nia-utu iliyo ni mbegu ya mafikara mema atajaliwa kheri na maumbile na azma yake kutimizwa. Kulazimisha kujenga pale ambapo mazingira na wakati si sahihi binadamu atavuna taabu na kujihangaisha. Ujenzi hutaka werevu wa akili na utangamano wa maumbile na nyakati-siri yenyewe hasa majira na mizunguko iletwayo na 'Pumzi ya Uzima'. Binadamu akoseapo kanuni anaweza kusahihisha adha yoyote imsibuyo kwa kuendana na njia ya usikronizi wa mwendo wake na kanuni za kheri ya maumbile yote. Dosari ya makosa ya mwanadamu husahihishwa kwa nia safi na uongofu katika njia ya katikati yenye kheri kwa yote. Mwendo huu ndiyo utangamano wa nia-utu katika mtu na nia-uzima wa vyote. Dosari ya makosa kwa mwanadamu si hesabu kwa matendo yake bali ni upotofu wa nia yake kwa wakati na pia mshahara wa ubovu katika nia-utu wake kwenye mfichamo wa
ufahamu mbalali wake.
Maumbile yote yamefanyika kwa hekima ya namna yake ambapo hakuna chochote kinachoweza kukimbia athari za matendo yake. Kadri mtu asababishavyo jitahada zozote matokeo humrudia kwa kadri ya stahiki za nguvu zake katika kitendo cha mgongano wa madhahirisho yote. Kuna yatendayo na matokeo yake huonekana kuja upesi ama kadri ya kusemama hapo hapo; na yale ambayo huleta athari za matokeo katika kusonga kwa vipindi. Hii yote ni kwa kuwa ulimwengu wote tuuona kwa macho ni tumbo la uzazi kwa hata yale yasiyodhahiri kwa
ufahamu jua wetu kung'amua mara moja na hali pia tumbo hili hukirimu hata uwezekano wa mdhahiriko wa maumbo kwa mafikara yetu mabovu ndani ya
ufahamu mbalali. Yapo mambo yatokeayo katika jamii ambayo ni mavuno ya mtu mmoja mmoja na yapo ambayo ni mavuno ya kiukundi-ukijiji, ukimtaa, ukimji, uki-Jiji, utaifa. Pia yapo mambo ambayo ni mavuno kwa uanadamu wote duniani.
Hakuna mwanadamu asiye na kadri ya dosari inayomkutanisha yeye na wengine walioko katika mazingira yake ila ikiwa tu ameyatambua madeni yake katika makundi ya watu na kuweka nia ya kuyalipa na kuacha kulisha ubatili na upotofu wa kanuni zenye kheri ziongozazo madhahirisho yote.
Ndivyo '
Karma' imekuwa ikifundishwa katika mashauri ya dini nyingi kutoka mashariki. Kinachokwenda katika mzunguko hurudi; kinachopandwa huvunwa. Pia kuwa binadamu yuko kokote pale anapojikuta kuwapo kwa kuwa ana
karma katika muktadha wa deni na hapo alipo. Na pia mtu huzaliwa pale ambapo msimu ni sahihi ili karma yake kuvunwa na majira na mazingira ya yale anayoyakuta mahali. Mtu huzaliwa mahala kwa kheri ama ubaya kwa kadri ya mbegu yake iliyofichamia katika
ufahamu mbalali; ndani ya
ufahamu mbalali pia kuna kumbukumbu hata kwa yale asiyomaizi kupata kuyatenda katika muktadha wa
ufahamu jua wake. Na hivi kila nukta ya mwanadamu ni hukumu yake ikiwa hamaizi mbegu za nia-utu wake zichipukiazo kutokana na matendo aliyotenda kungine katika muktadha wa ufahamu mbalali. Mengi ya mawazo na fikra na usadikifu wa watu si 'mawazo mapya' kama wanavyoishi kujifahamu; bali ni fikra na mawazo waliyodumisha toka kungine hata nje ya wigo wa maisha yao wanaoujua. Na basi ni mpaka pale mwanadamu anavyokirimika kujua hata yale yaliyofichika ndani ya
ufahamu mbalali wake ili aweze kubatilisha ushawishi wa uchafu wa mawazo yake hawezi kumaizi yeye 'Haki' iliyofanyikia ulimwengu wote. Haki hii ni hai na endelevu; si kama vile hasa ilivyopatwa kuzungumzwa kwamba husubiri siku fulani. Kwa kuwa watu wa zamani walifaa kwa mambo ya zamani na mashauri kuwafaa visomo vyao na mapana yao. Leo hii kisomo hiki hiki kinafunua mambo makuu zaidi na binadamu hana budi kutahayari upokeo wake kwa hekima kuu kuliko kumbukumbu lolote la maneno na masimulizi.
UHURU wa mtu ni kujinasua na kamba zote zinazomfunga mtu na mtu, pia mtu na mazingira hata katika muktadha wa
ufahamu mbalali na mbegu zake za fikra-hisia kikumbukumbu. Lengo la mirengo ya kiroho kwa imani za kimashariki toka zamani ilikuwa ni kuupata huu Uhuru-Kisaikia, kimwili na kihisia; na ndivyo ilivyo hata kwa siku zote. Daima uhuru kamili huhusisha muktadha wa hata yale yaliyofichika toka kwenye upande wa nje wa ustawi wa wanadamu wote na tena jinsi ya mtu mmoja mmoja.
Ikiwa kwa muktadha wa mawazo na matamanio yake yeye mwenyewe mwanadamu hukirimika kuzaliwa mahala hata pasipo kumaizi kanuni zilizopelekea yeye kuzaliwa hapo; ni ishara ya kwamba yeye mtu si huru. Kila mwanadamu anawajibu wa kutafuta muktadha wa sababu za yeye kuzaliwa mahala; la sivyo yeye si mwenye kuwajibika na kweli ya ukirimiko wa uzima wake na ustawi wake pale alipo. Pia yeye hawezi kuwa huru na yale ambayo hajayashtukia kutawala majaliwa yake na hivi anakuwa 'mteja' wa usadikifu wowote usio ni hekima madhubuti ila mashauri ya mpito na ahueni. Kwa kadri anavyokirimika kutambua toka ndani, muktadha wa majaliwa yake kutokana na matendo yake yeye mwenyewe ndani ya nyakati za ndani na nje; kwa uzuri na pia ubaya yeye anao 'utashi' ambao ndiyo basi ngazi ya msingi kwa ukombozi wa mtu mwenyewe. Kwa kuwa kheri humshika mkono kumwongoza yule aliye na nia thabiti na uwajibikaji kwa jumla yote ya matokeo ya kazi zake. Mwanadamu ana kheri anapokiri makosa yake na kuyakubali kwa moyo wake wote na huku akiomba ndani ya 'roho' mwangaza wa wongofu kwa njia yake. Kwa saburi, maovu yote ya mtu husafishwa kwa moto wake wa nia safi na marekebisho ya dhamira katika mwendo wa safari yake yote mpaka pale atakapotakasika kabisa. Na hata atakasikapo mwanadamu anaweza kwa kupitia 'nia moja na Roho wa Uzima wote' kuchagua majaliwa yake kungine kokote katika msongo wa wakati na mahala-naam, hata kwa maisha mengine mbali na wigo wa maisha yake kipindi cha sasa.
Namna ya kumbukumbu inautumikivu kwa 'ukuwa' wa mtu katika muktadha wa nia na dhamira. Kumbukumbu ni kimvuli cha maarifa ya yote katika wakati wote na mawezekano yote. Ipo namna inayoweza kuleta shauri kuwa kila litendekalo katika majaliwa ya vitu vyote ndani ya nyakati ni sehemu ya uwezekano wenye kutathminika wa madhahirisho na maumbo yote hata kama ndani ya madhahirisho hayo kuna mkondo wa kuweza kuchagua baadhi ya maamuzi ndani ya viumbe vyenyewe. Kuna muktadha wa vitu kuwa kwamba vimepangwa na hali havijapangika kwa wakati huo huo -- kusema basi jumla ya yote huwa na sura dhahiri pale upana wa matukio unapotathminiwa. Hili katika ulimwengu wa fizikia ni huleta mashauri yenye nadharia za dhana ya kwamba 'haiwezekani kukadirisha mwendokasi na unafasi wa chembe zifanyazo tonadari ya maada' na hali tonadari yenyewe yaweza kutathminiwa hayo mawili katika uhalisia wake. Hili ni shauri la mfizikia Heisenberg--kwa mfano; na huitwa 'Kanuni ya Utohakika ya Heisenberg'.
Jinsi ya tabia na hadhi ya tonadari ni yenye kufanana kabisa na chembe msingi kwa utu na roho katika kufanyika kwa mwanadamu. Hivi ni vema kuyapitia mashauri yahusiyo muundiko wa chembe na chembe katika kuyafanya maumbo. Minajili ya utohakika wa kung'amua unafasi na kadiri ya mwendo kwa chembe zidhaniwazo kufanya tonadari ndiyo hiyo hiyo huweka ombwe katika utambuzi wa mwanadamu katika kudadavua 'kiini' cha uzima wake. Kwa mfano mtu aweza kusema kuwa kwake mtu ni 'hakika'; lakini je' iweje kuwa yeye ni mwenye kujimaizi ujitambuko wake na wakati mwingine asiwe hivyo? Nukta moja ya wakati mtu ni mzima na bukheri wa afya, wakati mwingine yeye yu mgonjwa na hajiwezi na tena zaidi wakti mwingine yeye ni mwenye kulala katika mauti na tena asije kumka tena... Kiini cha ujitambuo wa unafsi katika mwanadamu kitovu chake ni wapi hasa? Kwa maana ni hicho tu labda ndiyo 'hakika' yenyewe-hivyo basi mwili wenyewe usiwe ni hivyo. Ikiwa mtu huwa na 'utambuko' kwa kujimaizi nafsi yake ni nini sehemu ya kumbukumbu katika kujibainisha kwake hakika ya kuwa ni nafsi moja?
Kumbukumbu ya mambo na unafsi wake mtu japo yaweza kuwa ni 'kioo cha ujitambuo' yenyewe hiyo yaweza kabisa isiwe 'kweli' na wala 'hakika' yenyewe... Sasa kipi basi ni hakika? NI kawaida ya kuwa binadamu anayosilika ya kujibainisha 'ukuwa' wake kwa kumbukumbu la matendo yake lakini je, hili ni shauri la kweli ya utu wake kabisa kabisa? Yumkini kumbukumbu ina utumikivu wa kadri ya umuhimu kabisa katika ulimwengu wa madhahirisho lakini kumbukumbu yote ni 'usikweli'. Kadri ambavyo kumbukumbu ni usikweli lakini kubidi kukidhi haja ya 'ujitambuo wa mpito' basi hilo litakuwa wazi kuwa ni ile hali yenye kuwezeshwa na akili ya mtu mwenyewe yenye kufikiri na kuendesha mashauri ya wakati hadi wakati-- na pia iko sehemu ya akili ya mtu isiyo na sililka ya namna hiyo. Sehemu ya akili isiyo ni chombo cha mafikara ila tu sitaajabu ya 'mgundisho' wa tafsiri ya uwezekano wa mtu kujitambua; kwa minajili ya kumbukumbu lake na kwa jinsi ya 'kioo cha kujiona' tuuite ni 'akili ya juu' nayo hutenda kazi kwa mtindo tunaoweza kuuita ni 'dhahania'. Wazo tupu lililo ni mfano wa mbegu ni dhahania. Jinsi ya dhahania katika muktadha huu ni ile sura isiyo bayana ya jambo pana na hali yenyewe ni kama ule muhtasari mzima unaohifadhi ukweli wa lenye kujakufahamika vema baada ya vitendo vya kawaida vya matendo ya akili ya chini ya mtu kuchukua mkondo wa mizunguko wake wa mafikara na udadavuaji. Akili ya chini na ya juu ya mtu vyote kwa pamoja hufanya saikia ya mtu; nayo humuandama yeye kwa mapana yote ya kujitambua uzima wake.
Saikia ya mtu yeyote ni siri ya mafumbo kwa uelewa wa mtu nayo mazingira yake na hiyo huja kuzaa tathmini ya nidhamu ya mtu mwenyewe na nia yake. Upo uwezekano wa kutosheleza kusema kwamba-- Saikia ya watu wote, vitu vyote na uzima wote huwa na mahala ambapo hukutana ki 'maana na kheri' ya mienendo yote. Lakini katika muktadha wa dhahania binadamu kwa jinsi ya mtu mmoja mmoja, hukinga 'maji' kwa wakati mawezekano ya kujifafanua yeye wenyewe katika minajili ya majaliwa na mustakabari wake na hivi kuazimia mielekeo ya nia yake tokea kwenye mawezekano mapana zaidi ya dhahania ya utu na uzima wote.
Ili kutia hamasa ya 'ujitambuo' wa mtu, kumbukumbu la mtu humchochea yeye katika kuyabayanisha mapana ya kuchagua na kuamua mashauri ya 'utu' wake kulingana na mfululizo wa matendo yake na uhifadhiko wake katika maisha na mazingira aishiyo na kutokea kule atokeako. Nidhamu ya 'utu' ni kutaniko la mtu, mazingira yake na ung'amuzi wa mema ama mabaya katika kutanabahi ustawi wake yeye mwenyewe. Na hivi katika wanadamu wote kumbukumbu yaweza kuwa ni kimvuli cha kuegama na kinga kwa yale yasiyofahamika. Hapo hapo mwanadamu akusudiapo kutanua zaidi wigo wake ndivyo hata wigo wake wa kimvuli huongezeka. Mwanadamu daima yuko katika mapambano ya mazoea na yale mageni kwake. Mageni huweza kumletea hofu yeye lakini ikiwa mtu ni mwenye kushirikisha akili yake ya juu yeye aweza kushinda adha ya kumbukumbu na mashauri yenye kasumba na hivi huweza kuongozwa na dhahania katika kukabili mawazo mapya na wigo mpana zaidi wa maisha.
Akili ya chini ya mtu ni yenye kusumbuka na kumbukumbu na vina vya tafsiri dhidi ya utu wa mtu mwenyewe. Lipo daraja linalounganisha akili chini na ile ya juu ya mtu mhusika mmoja; wateosofia huita hili 'antakarana'. Uwezo wa mwanadamu kuzidi akili ya kawaida-- iliyo ni ile ya chini ni hafifu; na hivi ni katika mazingira maalum hutokea kwa mwanadamu kutumia mawezekano yaliyo katika akili ya juu. Na hivi wanadamu katika wingi wa idadi na silika ni wenye 'utambuo' mdogo wa yale yanayofanya saikia yao. Basi ndivyo hivi watu waweza kuwa watumwa wa mazoea yao duni na hafifu na hali wao wasione lolote lililopungua katika ustawi wao. Wale wote wanaoanza kuvuka daraja la antakarana daima wataonekana ni watu wa 'mashauri ya ajabu ajabu' na ufikirivu usio wa kawaida. Hawa ndiyo wale watu ambao huleta mabadiliko makubwa katika jamii zao hata kama jamii inayowazunguka haijaweza kwa wakati wake kuwatambua kwa matunda ya michanyato yao.
https://www.facebook.com/notes/10150299967634421/