TEGETA, DAR: Meja Jenerali Mstaafu wa JWTZ, Vicent Mritaba apigwa risasi 5 na majambazi

Meja General mstaafu wa JWTZ, Vincent Mritaba amepigwa risasi 5 na watu wasiojulikana akiwa anaingia nyumbani kwake, yupo Lugalo hospital kwa matibabu.
Je Wamepora Mali yeyote au wamemshuti tu na kutokomea ??

Mungu amponye mstaafu wetu
 
Utawala uliofitinika hauoni ndani maana sasa usalama wa wananchi haupo kabisa jeshi la polisi TISS na kwa karibu TPDF na mahakama bunge wameingia kwenye siasa its pity tunaingiza nchi kwenye umwagaji wa damu kwa tamaa ya bashite na baba yake eeh Mungu tuone na jibu sala zetu hawa watu hawafai kabisa
 
Hata kama ni ujambazi tu, kuna uhusiano kati ya ugumu wa maisha na ujambazi.

Kama mbunge na Jenerali mstaafu wa jeshi wanaweza kupugwa risasi, hakuna raia aliye salama.

Sent from my Kimulimuli
 
Ukishakuwa na hicho cheo nachojua unalindwa hadi kifo...hata ukistaafu
Na ulinzi wake ni wa MP na si mmoja...

Sasa nini kimetokea jameni...
Mungu Ibariki Tanzania
 
Wote lao ni moja tu alafu ujue Utawala huu haulipendi Jeshi ( JWTZ) na Mtukufu yy kaamua kuwapenda Polisi kuliko taasisi zote, ni tofauti na Kikwete yy aliwapenda jwtz akawapa huduma na heshima kubwa na wengi wanamkumbuka mpaka leo, Mtukufu yy anawapenda polisi na sasa anajiandaa kumweka makonda awe Mbunge wa kuteuliwa na waziri wa mambo ya ndani na mwigulu nchemba atachukua wizara ya Simbachawene, huku Mrisho gambo akihamishiwa Dsm kuwa RC kuchukua nafasi ya Bashite.
Wacha tu awapende Police nawao wajione wanathaminiwa.. Ujue jamaa wapo stressed sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
IMG-20170912-WA0049.jpg
 
Meja Jenerali mstaafu wa JWTZ, Vincent Mritaba amepigwa risasi 5 na watu wasiojulikana akiwa anaingia nyumbani kwake, Tegeta Dar es Salaam ambapo watu wanaodhaniwa kuwa majambazi wamemshambulia kwa risasi Meja Jenerali huyo

Tukio hilo limetokea jioni ya September 11, 2017 wakati Meja Jenerali Mritaba akiwa anaingia getini nyumbani kwake Tegeta ambapo alivamiwa na watu wasiojulikana na kupigwa risasi tumboni, begani na mguuni.

Hadi usiku wa jana Madaktari walikua wanaendelea na upasuaji kutoa risasi tatu tumboni na kushughulikia majeraha mengine katika hospital ya Lugalo.
Sasa hii ni Cinema ili tuamini kua kuna majambazi tu.
Risasi zile zile tano kama zilivyompata lissu, halafu maeneo yale yale, Tumboni, mkononi na miguuni
 
Back
Top Bottom