TEC na Jumuiya ya Kikristu daini mapumziko siku ya mwaka mpya wa Kikristu

Asante CCM

JF-Expert Member
Jun 22, 2023
346
1,301
Upande mmoja wa Tanzania sasa ni rasmi mwaka mpya wa Dini fulani itakuwa ni siku ya mapumziko.

Sasa basi, kama imeweza kuwa hivyo ndani ya Tanzania, kwa nini TEC na Jumuiya ya Kikristu wasidai mapumziko nao siku ya mwaka mpya wa Kikristu?!

Kanisa la Roma kwa mfano, linao mwaka mpya wa Kanisa na ni muhimu sasa nanyi mdai mapumziko siku lile.

Bwana Yesu Asifiwe!
Mwanakondoo ameshinda!
Tumsifu Yesu Kristu!

Nawasilisha.
 
?matope ya tundulissu?
 
Haya mapumziko wanaoyapenda ni wavivu tu, siku zote waliojiajiri hawana mapumziko ya hovyo, hebu tusishindanie tuzo za uvivu, wacha maisha yaendelee tufanye kazi.
 
Tulikubaliana kuwa serikali haina dini lakini watu wameanza kuingiza mambo ya dini yao serikalini kwa kasi ya ajabu. Sasa huu mtindo itabidi kila dini iingize mambo ya dini yake serikalini. Mara mitihani ya dini mara upuuzi fulani uingizwe kwenye mitaala ya taifa. Itatusaidia nini sisi wengine tusiamini na kuabudu dini hiyo? Ndio maana kuna serikali duniani zenyewe zimeamua kujitenga mbali na dini zimewaachia wananchi wake huru kujiamulia waamini na waabudu kitu gani bila kuwabughudhi
 
Tuwe na mapumziko mwaka mzima maana hii kasi ya watu kushawishiana kudai mapumziko ni kama imeshika kasi sana kwenye hii jamhuri ya watu wenye amani
 
Back
Top Bottom