TEC: Mipasuko kwenye jamii Husababishwa na Watu fulani kujiona bora zaidi na wako juu ya Katiba na sheria

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,280
BARAZA la Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini Tanzania (TEC), limewataka Watanzania kuacha siasa za upendeleo na ubinafsi, kwa kuwa zinasababisha mfarakano katika kijamii.

Wito huo umetolewa na TEC kupitia ujumbe wake wa Kwaresma uliotolewa hivi karibuni, ukiwa na kichwa cha habari “Ingekuwa heri leo msikie sauti yake, msifanye migumu mioyo yenu…” (Zab 95:7-8).

Leo Jumatano, tarehe 17 Februari 2021, Wakristo wengi duniani wameanza ibada ya Kwaresma.

Kwenye ujumbe huo wenye kurasa 29, umehusisha maaskofu 33 akiwemo Rais wa TEC, Gervas Nyaisonga, umeelezea mambo mbalimbali ya kijamii, kisiasa na kiroho ukisema, kwa sasa dunia imeshuhudia manung’uniko na malalamiko kutoka kwa umma.

Malalamiko hayo ni juu ya baadhi ya viongozi wanaotumia mamlaka zao kufanya mambo kwa ajili yao na wanaowazunguka ama kikundi fulani, jambo linalokuza mashaka na kuondoa uaminifu.

“Licha ya hayo yote mema ambayo wenye mamlaka hususani ya kisiasa wamekabidhiwa, nyakati zetu hizi dunia, imeshuhudia manung’uniko na malalamiko kutoka kwa umma kwamba baadhi ya viongozi, wanatumia dhamana hiyo kwa ajili ya kujinufaisha wenyewe au kwa ajili ya manufaa ya kikundi fulani.”

“Siasa za namna hiyo, husababisha unyanyasaji wa baadhi ya watu au kikundi cha watu na hivyo kuondoa hali ya kuaminiana,” limeeleza baraza hilo la juu la Kanisa Katoliki.

Ujumbe huo umeeleza wazi kwamba, miongoni mwa mipasuko mikubwa ya kisiasa inayotokea katika jamii, huchagizwa na kutokana na kikundi cha watu fulani kujiona ni wa daraja la juu na bora kuliko kingine.

Na kwamba, kikundi hicho wakati mwingine kujiona kiko juu ya Katiba na Sheria mbalimbali za nchi na hivyo kuzivunja pasi na kujali.

“Matokeo ya haya yote ni kufarakana kijamii, lawama zisizoisha na hivyo kuhatarisha amani na usalama wa jamii husika,” umeeleza waraka huo.

Ujumbe huokutoka Kitabu cha Zaburi 95:7-8 ‘Ingekuwa heri leo msikie sauti yake, msifanye migumu mioyo yenu,’ umewakumbusha Watanzania kurudi kwenye misingi ya Mungu ili kuleta uongozi bora na siasa safi.

“Kati ya maeneo muhimu sana ya kipimo cha uongozi bora na siasa safi, ni namna kiongozi anavyoishi uadilifu wake wa uongozi tukitambua kwamba “Hakuna mamlaka (halali) isiyotoka kwa Mungu”(Rum 13:1). Kutokana na hilo, uongozi, madaraka au mamlaka yoyote ile inapaswa kuwa ni dhamana kutoka kwa Mungu.

“Dhamana hii anapewa kiongozi kama mwakilishi wa Mungu katika uongozi tukitambua Mungu ndiye kiongozi na mtawala pekee. Dhamana hii inapaswa kumkumbusha kiongozi kwamba, mamlaka aliyopewa si kwa ajili yake bali ni kwa ajili ya wote aliokabidhiwa,” umekumbusha waraka huo.

TEC limewataka Watanzania kusikia sauti ya Mungu kwa kufanya toba na kuilainisha mioyo yao, katika kuhakikisha haki inatendeka katika jamii.

“Ujumbe wa Kwaresima unatutaka kama jamii “tusikie sauti yake, tusifanye migumu mioyo yetu. Tutaisikia sauti ya Mungu kwa kuhakikisha kwamba haki inatendeka katika jamii.

“… na hasa haki za kikatiba za kujiendesha kisiasa zikiwemo kuheshimu uhuru wa mawazo mbadala, kama sehemu ya kudumisha demokrasia na hasa katika mfumo wa vyama vingi vya kisiasa ,” umeeleza ujumbe huo.

Chanzo: Mwanahalisionline
 
Ujumbe wa Kwaresima ulitakiwa ujikite kwenye imani zaidi mfano badala ya porojo za kisiasa ulitakiwa

1. Ueleze kipindi hiki kuwa cha maungamo kwa kila mtu kibinafsi kuacha mabaya na kutenda mema kama wafanyavyo waislamu kipindi cha mfungo wa ramadhani

2. Usisitize watu kujitoa kwa moyo wote kuhudumia wengine kama KRISTO alivyojitoa

3. Kuwahurumia wenye shida na mateso kama wagonjwa,yatima ,wahitaji wa chakula nk kama Yesu alivyosaidia wahitaji alipokuwa duniani

4. Kuomba Mungu atuepushe na janga la Corona .Yaani waraka umejaa porojo ina maana kuomba swala la Corona hawajakupa uzito!!!

5. Kuombea uchumi wa nchi na watu wake

Huo waraka umekaa kifarisayo kufunga wafunge wakatoliki halafu washambulie wanasiasa mfungo ni kujirudi mwenyewe ndani sio kuangalia huko kwingine nje kuna nini?
 
... siku viongozi wa dini watakapoacha lugha za jumla jumla yaani kuzunguka mbuyu wakawa specific; wakawa na ujasiri wa kutamka kama huyo Bwana alivyowahi kutamka maneno hayo hapo chini; kwa hakika utakuwa ukombozi wa pili.

"... Akawaambia, nendeni, mkamwambie yule mbweha, tazama, leo na kesho natoa pepo na kuponya wagonjwa, siku ya tatu nakamilisha kazi yangu."
 
Siku moja watoto walienda mtoni kuchota majio, kufika mtoni wakamuona chura yuko kwenye maji, wakaanza kushindana kumrushia mawe wakitaka kujua nani mwenye shabaha zaidi....kwa huzuni yule chura akapaza sauti ya upole "Mchezo wenu ni mauti yangu".
 
Ujumbe wa Kwaresima ulitakiwa ujikite kwenye imani zaidi mfano badala ya porojo za kisiasa ulitakiwa

1.Ueleze kipindi hiki kuwa cha maungamo kwa kila mtu kibinafsi kuacha mabaya na kutenda mema kama wafanyavyo waislamu kipindi cha mfungo wa ramadhani

2.Usisitize watu kujitoa kwa moyo wote kuhudumia wengine KAma KRISTO alivyojitoa

3.Kuwahurumia wenye shida na mateso kama wagonjwa,yatima ,wahitaji wa chakula nk kama Yesu alivyosaidia wahitaji alipokuwa duniani

4.Kuomba Mungu atuepushe na janga la Corona .Yaani waraka umejaa porojo ina maana kuomba swala la Corona hawajakupa uzito!!!

5.Kuombea uchumi wa nchi na watu wake

Huo waraka umekaa kifarisayo kufunga wafunge wakatoliki halafu washambulie wanasiasa mfungo ni kujirudi mwenyewe ndani sio kuangalia huko kwingine nje kuna nini?
unawafundisha kazi au? usiwapangie cha kufanya. maana naona umekuja na safu yako ya kuwapangia la kufanya.
kama hupendi au unachukiwa waraka pita kimya kimya achana nao.
 
... siku viongozi wa dini watakapoacha lugha za jumla jumla yaani kuzunguka mbuyu wakawa specific; wakawa na ujasiri wa kutamka kama huyo Bwana alivyowahi kutamka maneno hayo hapo chini; kwa hakika utakuwa ukombozi wa pili.

"... Akawaambia, nendeni, mkamwambie yule mbweha, tazama, leo na kesho natoa pepo na kuponya wagonjwa, siku ya tatu nakamilisha kazi yangu."
Ujue kwamba hawa maaskofu wetu hawana vyeti vya kuzaliwa vya babu zao.
 
unawafundisha kazi au? usiwapangie cha kufanya. maana naona umekuja na safu yako ya kuwapangia la kufanya.
kama hupendi au unachukiwa waraka pita kimya kimya achana nao.
Hiki ni kipindi cha kufunga sio cha kuongelea walio nje.Mifungo yote ni internal journey huhangiiki na farisayo yule kuwa sisi katoliki tuko bora kuliko mifarisayo iliyo nje iliyoko kwenye siasa sisi huwa tunafunga kwaresma nk lakini kule nje mifarisayo ya kisiasa haifungi haitendi haki nk. Nooooooooooo!!!! mind your own fast!!! Achana na nje huko

Huo waraka umejaa ufarisayo mtupu
 
Ujumbe wa Kwaresima ulitakiwa ujikite kwenye imani zaidi mfano badala ya porojo za kisiasa ulitakiwa

1.Ueleze kipindi hiki kuwa cha maungamo kwa kila mtu kibinafsi kuacha mabaya na kutenda mema kama wafanyavyo waislamu kipindi cha mfungo wa ramadhani

2.Usisitize watu kujitoa kwa moyo wote kuhudumia wengine KAma KRISTO alivyojitoa

3.Kuwahurumia wenye shida na mateso kama wagonjwa,yatima ,wahitaji wa chakula nk kama Yesu alivyosaidia wahitaji alipokuwa duniani

4.Kuomba Mungu atuepushe na janga la Corona .Yaani waraka umejaa porojo ina maana kuomba swala la Corona hawajakupa uzito!!!

5.Kuombea uchumi wa nchi na watu wake

Huo waraka umekaa kifarisayo kufunga wafunge wakatoliki halafu washambulie wanasiasa mfungo ni kujirudi mwenyewe ndani sio kuangalia huko kwingine nje kuna nini?
MJINGA MMOJA WEWE, USIYEJUA HATA MUNGU NA MAANDIKO MATAKATIFU .

Laiti ungeyajua, Ungeona mchango wa Mungu katika Kukosoa viongozi

Pumbavu mkubwa wewe, Inaana hata habari za Manabii ambao Mungu aliwatuma moja kwa moja wa wafalme.kwenda kuonya, kutoa maono..huzijui???

MPUMBAVU WEWE NA FAMILIA YAKO YOTE.

NMEKUTUKANA.
 
Ujumbe wa Kwaresima ulitakiwa ujikite kwenye imani zaidi mfano badala ya porojo za kisiasa ulitakiwa

1.Ueleze kipindi hiki kuwa cha maungamo kwa kila mtu kibinafsi kuacha mabaya na kutenda mema kama wafanyavyo waislamu kipindi cha mfungo wa ramadhani

2.Usisitize watu kujitoa kwa moyo wote kuhudumia wengine KAma KRISTO alivyojitoa

3.Kuwahurumia wenye shida na mateso kama wagonjwa,yatima ,wahitaji wa chakula nk kama Yesu alivyosaidia wahitaji alipokuwa duniani

4.Kuomba Mungu atuepushe na janga la Corona .Yaani waraka umejaa porojo ina maana kuomba swala la Corona hawajakupa uzito!!!

5.Kuombea uchumi wa nchi na watu wake

Huo waraka umekaa kifarisayo kufunga wafunge wakatoliki halafu washambulie wanasiasa mfungo ni kujirudi mwenyewe ndani sio kuangalia huko kwingine nje kuna nini?

Jiwe ndio kuharibu ustaarabu wa hii nchi, hilo baraza la maaskofu limeongea ukweli, ila kwa njia ya mafumbo kwa kuogopa lile kundi lake la watu wasiojulikana. Hakuna asiyejua ukweli huo.
 
Laiti ungeyajua, Ungeona mchango wa Mungu katika Kukosoa viongozi
Sio kipindi cha mfungo kipindi cha mfungo ni cha kuombea sio kukosoa .Mtu anasimama mbele za Mungu kuomba ya kwake na kuombea adui zake sio kukosoa adui zake!! Mfungo batili huo kabla ya kuanza!! Mfungo gani ambao badala yakuombea adui zako unauanza kwa kukosoa adui zako???

Yesu aliposema waombeeni adui zenu hiki ndicho kipindi chake sio cha porojo za kukosoa !!!
 
Ujumbe wa Kwaresima ulitakiwa ujikite kwenye imani zaidi mfano badala ya porojo za kisiasa ulitakiwa

1.Ueleze kipindi hiki kuwa cha maungamo kwa kila mtu kibinafsi kuacha mabaya na kutenda mema kama wafanyavyo waislamu kipindi cha mfungo wa ramadhani

2.Usisitize watu kujitoa kwa moyo wote kuhudumia wengine KAma KRISTO alivyojitoa

3.Kuwahurumia wenye shida na mateso kama wagonjwa,yatima ,wahitaji wa chakula nk kama Yesu alivyosaidia wahitaji alipokuwa duniani

4.Kuomba Mungu atuepushe na janga la Corona .Yaani waraka umejaa porojo ina maana kuomba swala la Corona hawajakupa uzito!!!

5.Kuombea uchumi wa nchi na watu wake

Huo waraka umekaa kifarisayo kufunga wafunge wakatoliki halafu washambulie wanasiasa mfungo ni kujirudi mwenyewe ndani sio kuangalia huko kwingine nje kuna nini?
Ila wangesifia serikali ya awamu ya tano ungewapongeza.
 
Na kwamba, kikundi hicho wakati mwingine kujiona kiko juu ya Katiba na Sheria mbalimbali za nchi na hivyo kuzivunja pasi na kujali.
Wanzungumzia jumla, hawazungumzii hali ya waTanzania.

Hapa kwetu hakuna "Kikundi" kama hiki:
kikundi cha watu fulani kujiona ni wa daraja la juu na bora kuliko kingine.
Hapa kuna Kiongozi anayesema anakikundi cha "wanyonge", hao wanyonge hawajulikani ni akina nani hasa.

Ni wale wasiohoji maamuzi yake?

Bahati nzuri kwa watawala wanaowazungumzia ndani ya waraka huo, ni kwamba "Liberation theology," ilianzia na kufia Amerika ya Kusini.
 
Hiki ni kipindi cha kufunga sio cha kuongelea walio nje.Mifungo yote ni internal journey huhangiiki na farisayo yule kuwa sisi katoliki tuko bora kuliko mifarisayo iliyo nje iliyoko kwenye siasa sisi huwa tunafunga kwaresma nk lakini kule nje mifarisayo ya kisiasa haifungi haitendi haki nk!!!!! nooooooooooo!!!! mind your own fast!!! Achana na nje huko

Huo waraka umejaa ufarisayo mtupu

We leta vijitafsiri vyako uchwara maana unafaidika na huu utawala wa kikatili, lakini Maaskofu wamenyoosha maelezo. Yule askofu mwingine mmemkamata jana kwa suala la katiba, lakini ukweli ni kuwa ukiacha Bakwata, taasisi nyingine zote za dini zimeshajua na kuweka wazi kuwa kwa sasa tuna kiongozi mlevi wa madaraka.
 
Pumbavu mkubwa wewe, Inaana hata habari za Manabii ambao Mungu aliwatuma moja kwa moja wa wafalme.kwenda kuonya, kutoa maono..huzijui???
Hakuna nabii alienda kumkosoa mfalme kipindi cha mfungo .Kipindi cha mfungo walikitumia kwa kuwa mbele za MUngu tu Kuomba yao na kuombea taifa hawakwenda kukosoa.Huo mfungo batili baraza lifute huo waraka umekaa kifarisayo sio wa mfungo wa Kikristo!!
 
Back
Top Bottom