Jamii ya kimaasai yakataa mambo ya kimila kunajisiwa kisiasa

Irene Darton

Member
Feb 25, 2024
18
21
Wakazi wa Ngorongoro wamefurahishwa na tukio la kuzuiwa kwa Mwanaharakati Joseph Moses Oleshangay anaeishi jijini Arusha aliyeanzisha harakati za kujitawaza kuwa Laigwanan wa jamii ya kimasai katika mitandao ya kijamii na baadaye kupanga tukio hilo kufanyika ndani ya hifadhi ya Ngorongoro.

Kwa kipindi cha wiki moja nyuma yalisikika Malaamiko ya wamaasai wa Ngorongoro mbakaji huyo wa mila anayeishi jijini Arusha ambaye ni mdogo wa Mbunge wa Jimbo la Ngorongoro alikuwa na nia ya Kujitawaza kuwa Laigwanan ikiwa ni wiki moja tu tokea kaka yake huyo kutawazwa kuwa Laigwanan wa Jamii ya kimasai . Kwasasa cheo hichohicho kinawindwa kwa hali yoyote ikiwezekana ata kwa kumwaga damu za wamasai wasio na hatia na mdogo mtu Joseph Oleshangay.

Kufuatia malalamiko hayo yaliyoihusu Famiali hiyo ya Shangay kuwa walikuwa wamepanga kunajisi utaratibu wa mila ya kimasai kwa lengo la kujiimarisha kisiasa ulifanyika ufuatiliaji ili kuona kama jamii ya Kimasai inazitambua harakati hizo na kama zinabaraka za wazee, au ni suala ambalo lilikuwa limepangwa na wanaharakati na wanasiasa kwa masllahi yao wenyewe ilibainika kuwa ni kweli suala hilo lilikuwa la kisiasa na lilikuwa linaufadhili wa wanaharakati na asasi za kiraia kama PIBGO’s Forum, Pastoral Women Council (PWC), Ujamaa Resources Community Team (UCRT), Legal and Human Rights Centre (LHRC), Tanzania Human Rights Defenders Coalition (THRDC), Tanganyika Law Society (TLS), Haki Ardhi na Lawyers Environmental Action Team (LEAT).

Kulingana na barua ya jeshi la polisi ambayo ilimtaka Joseph Oleshangay kusitisha kuitisha kusanyiko hilo ambalo lilikuwa ni kinyume cha Sheria na kulikuwa na viashiria vya uvunjifu wa amani kutokana na hata waaapishaji kugawanyika na wengine kuinamisha vichwa kama ishara ya mila kuingiliwa. Sambamba na amri ya polisi pia taratibu za mamlaka zinaelekeza kuomba kibali cha kufanya kusanyiko ili apewe ulinzi. Lakini sherehe hizi za mila ni wazi zimekuwa na madoido zaidi ya sherehe za kufunda wanawake “kitchen party “ inayoleta wafundaji kutoka ndani na nje ya ukoo.

Hata hivyo Joseph Oleshangay alikadi agizo hilo halali la kuomba kibali na kulazimisha kuandaa sherehe hiyo kwa lengo la kujipatia umaarufu wa kisiasa na kiharakati endapo Jeshi la Polisi litamzuia, akiamini kuwa wanaharakati waliopo nyuma yake ambao ndio waliopo katika mitandao ya kijamii watapaza sauti na kulihusisha tukio hilo na shughuli za kimila huku wakijua kabisa kuwa shughuli ya Joseph Oleshangay haikuwa na chembe ya tukio la kimila.

Baada ya Polisi kumzuia wanaharakati na wanasiasa walishindwa kujificha kuwa walikuwa nyuma ya mpango huo ovu, baada ya kuona Serikali ipo makini wakaanza kumtetea kwa kudai kuwa Mamlaka ya Ngorongoro imetumia nguvu kuzuia masuala ya kimila kufanyika.

Aidha asasi za kiraia zimeshindwa kutekeleza wajibu wao kwa mujibu wa vibali vyao kama walivyoomba na sasa wameingia katika Siasa, Mwanaharakati Joseph Moses Oleshangay ameamua kuwalaghai wamasai na kuwafanya mtaji wa kujipatia fedha za wazungu na kuwatumia Kama ngazi ya kupanda na Kuwa maarufu zaidi . “ MAAASAI COMMUNITY IS NOT A POLITICAL LADDER”. Jamii ya kimaasai inaheshimika kwa kutunza mila na desturi Iła uwepo wa wabakaji wa mila huenda ukafifisha ndoto za wa Maasai nyingi.

Hii ni ishara kuwa tuna wasomi walafi wa madaraka na miamvuli ya upotoshaji.
 
Back
Top Bottom