CHAMVIGA
JF-Expert Member
- Oct 5, 2012
- 7,687
- 2,240
Naomba msaada wenu wa ushauri na maelekezo ni nini nifanye,Nimemaliza chuo Motco ngazi ya Diploma ktk fani ya Ualimu ila pasi kuwa na bahati nimefeli somo la Saikolojia kwa miaka 2 mfululizo kila niliporudia.Imenifanya nisipate cheti cha kuhitimu mafunzo ya Diploma na mwisho wake nimeishia kuwepo nyumbani bila kazi.Msaada wenu wa ushauri unahitajika kwangu kwani maisha yanazidi kuwa magumu,kama kuna sehemu inayojulikana kupatikana kwa nafasi ili nifundishe kipindi najipanga naomba niunganishwe.Nawasilisha kwenu kwa hatua na ushauri
Aisee pole sana. Inaonekana hilo somo unabifu na mwalimu wake haiwezekani ipige chini mara 2. Sitaki kuamini kuwa wewe ni mbovu kiasi hicho mpaka unafeli psychology kila unaporudia. Jaribu tena ndugu bila hvyo katafute temporarly work for teaching somewhere else ili upate kusogeza maisha.