TCRA yasomesha watatu kwa Sh 2.2 bilioni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TCRA yasomesha watatu kwa Sh 2.2 bilioni

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by BAK, Nov 3, 2011.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Nov 3, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,804
  Likes Received: 83,180
  Trophy Points: 280
  Raymond Kaminyoge
  Mwananchi


  KAMATI ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), imegoma kupitisha hesabu za Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA), kutokana na ubadhirifu wa fedha za umma.

  Ubadhirifu huo uliobainika mbele ya kamati hiyo ni pamoja na mamlaka hiyo kutumia Sh2.2bilioni kuwasomesha wafanyakazi wake watatu nje ya nchi mwaka 2009/10.

  Jumla ya Sh4.1bilioni zilitumika katika kipindi hicho kugharamia mafunzo. Hayo yalibainika Dar es Salaam jana wakati Mwenyekiti wa Bodi ya TCRA, Jaji Mstaafu Buxton Chipeta na menejimenti yake walipofika mbele ya kamati hiyo kuhojiwa kuhusu hesabu zao.

  "Tumezikataa hesabu hizi kuna matumizi makubwa ya fedha za umma yasiyozingatia kanuni za fedha," alisema Makamu Mwenyekiti wa POAC, Deo Filikunjombe. Alisema TCRA imekuwa ikimlipa mwenyekiti wa bodi na wajumbe wake Dola za Marekani 350 kila mmoja kwa mwezi, sawa na Sh600,000 hivyo kutumia jumla ya Dola 2,000 sawa na Sh3.4milioni kwa ajili ya mawasiliano, wakati wao si watendaji wa shughuli za kila siku za mamlaka hiyo.

  Aidha, alisema wajumbe hao walinunuliwa katika mwaka huo wa fedha, simu za mkononi zenye thamani ya Dola za Marekani 600, sawa na Sh1 milioni kila mmoja.

  "Wajumbe wa bodi hawastahili posho hizi na kuanzia sasa wasilipwe kwa sababu siyo watendaji wa shughuli za kila siku. Pia kwa nini wanalipwa kwa kutumia Dola badala ya Shilingi ya Tanzania?" alihoji Filikunjombe. Makamu Mwenyekiti wa POAC aliongeza kuwa mamlaka hiyo imetumia Sh36 milioni kuwalipa posho wafanyakazi saba wa idara ya uhasibu wanaofanya kazi katika muda wa ziada, huku wakifanya kazi za kawaida wanazopaswa kufanya katika muda wa kawaida.

  "Hawa wanalipana mamilioni ya fedha kwa kufanya kazi ambazo waliajiriwa kuzifanya na wanalipwa mshahara! Huu ni ubadhirifu," alisema Filikunjombe.

  Kamati hiyo pia ilibaini matumizi makubwa ya fedha katika ujenzi wa Jengo la Makao Makuu ya Mamlaka hiyo, Barabara ya Sam Nujoma, Dar es Salaam. Alisema licha ya mshauri wa mamlaka hiyo kukadiria gharama za jengo hilo kuwa Sh27 bilioni, hadi sasa kiasi kilicholipwa ni Sh45bilioni. Kamati pia imebaini matumizi ya Sh600milioni ambayo hayakufuata taratibu za zabuni ya ununuzi wa umma.
  "Kiasi hicho kimetumika kununulia vifaa mbalimbali vya ofisi bila zabuni ya ununuzi kutangazwa jambo ambalo ni kinyume na sheria," alisema Filikunjombe.

  Alisema sheria inaruhusu mkurugenzi mkuu wa mamlaka hiyo, kuidhinisha kiasi kisichozidi Sh50 milioni tu kwa mwaka.Akijibu hoja hizo, Mwanasheria wa TCRA, Elizabeth Nzagi alisema fedha za mawasiliano zimekuwa zikitolewa kwa wajumbe wa bodi ili kuwarahisishia mawasiliano baina yao na menejimenti.

  Nzagi alisema mafunzo katika sekta ya mawasiliano ni gharama kubwa na hiyo ndiyo iliyofanya itumie Sh4.1 bilioni kwa mwaka. Hata hivyo, alisema si kweli kwamba Sh2.2 bilioni zilitumika kusomesha wafanyakazi watatu tu nje ya nchi, bali hayo ni makosa ya kihasibu.


  Alisema katika kipindi cha mwaka wa fedha uliopita, wafanyakazi wa idara ya uhasibu walilipwa Sh36 milioni za posho ya kufanya kazi katika muda wa ziada kutokana na uchache wa wafanyakazi.

  "Tunatarajia kuajiri wafanyakazi wengine ili kazi hizo ziweze kufanywa katika muda wa kawaida," alisema Nzagi.

  Kuhusu gharama za ujenzi wa jengo la TCRA, Meneja Mawasiliano na Uhusiano, Innocent Mungy alisema inaweza kuwa juu kuliko makadirio kutokana na kushuka kwa thamani ya shilingi.

  "Hakuna ubadhirifu katika ujenzi wa jengo lile hata uchunguzi ukifanywa kila kitu kiko wazi," alisema.
  Pia, Jaji Chipeta alisema hakuna ubadhirifu katika mamlaka hiyo akisema kilichojitokeza mbele ya kamati hiyo ni makosa ya kibinadamu katika utayarishaji wa hesabu zilizowasilishwa.
   
 2. M-pesa

  M-pesa JF-Expert Member

  #2
  Nov 3, 2011
  Joined: Sep 4, 2011
  Messages: 605
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Haya mashirika ndio maana hayana ufanisi, mawazo ya wafanyakazi ni jinsi gani waibe.
   
 3. jamii01

  jamii01 JF-Expert Member

  #3
  Nov 3, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 1,836
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  kila mtu anasoma ili haibe..
   
 4. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #4
  Nov 3, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,804
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Kusomesha wafanyakazi watatu kwa mwaka kwa sh 2.2bn ni "makosa ya ki-uhasibu"! Kweli Mi-Afrika ndivyo tulivyo!
   
 5. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #5
  Nov 3, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,517
  Likes Received: 2,259
  Trophy Points: 280
  kwani walikua wanasoma kitu gani cha bei ghali namna hiyo? mjini mipango,kijijini kazi,kha!
   
 6. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #6
  Nov 3, 2011
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Who is this guy on red bolded?

  Haiwezekani kila mtu anapoonekana ana makosa aseme ni makosa ya kibinadamu wakati hiyo ni sekta nyeti na inapaswa iendeshwe kitaalamu zaidi, sasa unapofanya makosa kama hayo wakati kuna wataalamu wa kufanya hiyo tena kabla hata mjengo haujaanza kujengwa pamoja na makadirio yooote gharama haiwezi kuzidi kwa kiasi kikubwa hivyo. Bilion 27 to Bilion 45 na bado hela inalipwa? Bado Consultant hajaletewa vurugu za kufukuzwa?

  Aggggrrrrrrrrrrrr!! Watu wanadhalilisha taaluma zao kipuuzi sababu ya pesa.
   
 7. Mtumiabusara

  Mtumiabusara JF-Expert Member

  #7
  Nov 3, 2011
  Joined: Nov 18, 2009
  Messages: 473
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  kwa hiyo walisomesha wafanyakazi wangapi kama siyo 3? Na watueleze walikuwa wanasomea kozi gani
   
 8. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #8
  Nov 3, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  huyu jaji alokua anasoma hyo taarifa ni KILAZA
   
 9. H

  Haika JF-Expert Member

  #9
  Nov 3, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,318
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Sasa kama mahela yako mengi wafanyeje?
   
 10. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #10
  Nov 3, 2011
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,757
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  Naipenda JF
   
 11. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #11
  Nov 3, 2011
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Mitanzania mingine bana. Unapelekaje hesabu zinazoonyesha watu watatu wamesomeshwa kwa 2.1 billion!

  Halafu wazungu wakija kuchukua kazi zetu tunalalamika
   
 12. Kabembe

  Kabembe JF-Expert Member

  #12
  Nov 3, 2011
  Joined: Feb 11, 2009
  Messages: 2,238
  Likes Received: 931
  Trophy Points: 280
  Hizi kamati za Bunge zikishabaini kuna ubadhirifu au upotevu wa pesa za umma then what next? Am tired of this trend of business as usual.
   
 13. k

  kapuchi Senior Member

  #13
  Nov 3, 2011
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 167
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  TCRA mbona ni wabadhirifu siku nyingi tu, hata huo ukaguzi umefanywa kijuu juu sana.napendekeza an independent auditor aende akague mtakuja kuniambia, masafari na maposho wanayojilipaga kiukweli yanakiuka kabisa taratibu za malipo kama alivyosema makamu mwenyekiti wa kamati. hawa jamaa bwana wanaiba sana tena bila huruma kodi za walalahoi!
   
 14. Tangawizi

  Tangawizi JF-Expert Member

  #14
  Nov 3, 2011
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 2,835
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280
  Ile nafasi ya ukurugenzi wa TCRA ni nzuri. Na allowance zao pia ni nono sana. Tatizo hawakujua kama bunge litakuja kukagua hizo hesabu.
  Bottomline, hii nchi haina displine toka juu kabisa mpaka huku chini. Ndio maana watu wanafanya haya tunayoyasikia na kuyaona.
   
 15. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #15
  Nov 3, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  wamesomea jinsi ya kusajiri line za simu si unajua huu mfumo umeanza hivi karibuni.
   
 16. F

  FJM JF-Expert Member

  #16
  Nov 3, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  2.2billion kusomesha watu watatu? Ina maana hao watu wemesomeshwa kuanzia chekechea au? Maana haingiii akilini ni course ya aina gani inatayogharimu kiasi hicho! Hivi hakuna watanzania wenye ujuzi badala ya kujiri watu wasio na ujuzi halafu wanaishia kuwa wanafunzi badala ya kufanya kazi? Lakini kubwa ni hili, kama wanatumia hela zote hizo kusomesha wafanyakazi wake inakuwaje tena wakosee hata kutayarisha vitabu vya mahesabu?
   
 17. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #17
  Nov 3, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,015
  Likes Received: 743
  Trophy Points: 280
  Tz hiyo bana.
   
 18. Zanta

  Zanta JF-Expert Member

  #18
  Nov 3, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 2,017
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Hivi upungufu wa madawati nchi nzima gharama yake sh. ngapi?
  Mtoto anakaa chini wengine wanasomeshwa ka 2.2 bilioni? manina walai!
   
 19. Zanta

  Zanta JF-Expert Member

  #19
  Nov 3, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 2,017
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Halafu lijitu linasimama bungeni na kusema "kutokana na ufinyu wa bajet" blah blah ..............................
  **********zao!
   
 20. M

  Makupa JF-Expert Member

  #20
  Nov 3, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Jamani acheni kulalamika,kozi za mambo ya mawasiliano ni aghali sana
   
Loading...