TCRA yawataka Watanzania kutotumia huduma za mawasiliano ambazo hazijaidhinishwa na mamlaka hiyo

The Sheriff

JF-Expert Member
Oct 10, 2019
617
1,801
Tamko linasema hivi:

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inapenda kuutaarifu Umma kuwa utoaji wa huduma za mawasiliano, zikiwemo huduma za usalama mtandaoni (cybersecurity services), intaneti, na vituo vya kutunzia data (data centres), katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bila kuwa na leseni iliyotolewa na TCRA ni kinyume na Kifungu cha 14 cha Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta ya mwaka 2010 (EPOCA) ambacho kinakataza mtu, taasisi au kampuni yoyote kutoa huduma hizo bila kuwa na leseni.

Aidha, tunapenda kuukumbusha Umma kuepuka kutumia huduma za mawasiliano, zikiwemo huduma za usalama mtandaoni, intaneti, na vituo vya kutunzia data, zinazotolewa na mtu, taasisi au kampuni zisizo na leseni zilizotolewa na TCRA.

TCRA inaendelea kusimamia huduma za mawasiliano nchini na haitasita kuchukua hatua kisheria dhidi ya mtu, taasisi au kampuni itakayobainika kujihusisha na utoaji wa huduma za mawasiliano, zikiwemo huduma za usalama mtandaoni, intaneti na vituo vya kutunzia data, ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bila kuwa na leseni iliyotolewa na TCRA.

TCRA.jpg

=============For English Audience Only==============
The Tanzania Communications Regulatory Authority (TCRA) has issued a public statement warning against the use of communication services that have not been authorized by the regulatory body. According to the statement, providing communication services, including cybersecurity services, internet, and data centers, within the United Republic of Tanzania without a valid license from TCRA is in violation of Section 14 of the Electronic and Postal Communications Act of 2010 (EPOCA).

The public is urged to avoid using communication services, including online security services, internet, and data storage centers, offered by individuals, institutions, or companies that do not possess a valid TCRA license. TCRA reaffirms its commitment to overseeing communication services in the country and emphasizes that legal action will be taken against any individual or entity found to be providing such services without the required TCRA license.
 
Kazi yao ni kudidimiza na siku kutafuta mbinu mpya mmekaa kimaslai na kisiasa sana,,, kwahy hamuna tija ndani ya hili taifa na ningekuwa waziri usika ningewafutilia mbali na kuweka watu wenye uelewa
 
Kazi yao ni kudidimiza na siku kutafuta mbinu mpya mmekaa kimaslai na kisiasa sana,,, kwahy hamuna tija ndani ya hili taifa na ningekuwa waziri usika ningewafutilia mbali na kuweka watu wenye uelewa
leseni muhimu mkuu tcra wapo kumlinda mtumiaji na kuweka fair play ground kwa service providers assume wewe unalipia lesen na umekamilisha vigezo kibao kupata hio lesen halaf kuna wagaigai hawana lesen na hawatambuliki wanatoa huduma kama yako haitokua sawa hio
 
leseni muhimu mkuu tcra wapo kumlinda mtumiaji na kuweka fair play ground kwa service providers assume wewe unalipia lesen na umekamilisha vigezo kibao kupata hio lesen halaf kuna wagaigai hawana lesen na hawatambuliki wanatoa huduma kama yako haitokua sawa hio
uzuri wake inatumia siasa kujibu maswali ya msingi, pale wanapojibu kisiasa unaweza hisi watu makin lakin kiuhalisia hakuna kitu unachosema ni sawa kwa mtazamo wao lakin kimatendo ni wapo tofaut na unachosema
 
Upo Umuhimu mkubwa sanaa wa kila "Mtanzania" mkubwa kwa mdogo kuyaelewa masuala ya Usalama wa mtandaoni...
 
Back
Top Bottom