TCRA yatoa onyo kwa waagizaji na wasambazaji wa vifaa vya mawasiliano ya simu ambavyo havijaidhinishwa

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,016
9,885
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ni taasisi ya Serikali iliyoanzishwa kwa Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Na. 12 ya 2003, na kupewa jukumu Ia kusimamia Sekta ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta nchini Tanzania.

TCRA imebaini kuwa yapo baadhi ya Makampuni au wafanyabiashara wanaoingiza, kusambaza na kuuza nchini Tanzania vifaa vya mawasiliano zikiwemo simu, ambavyo hazijaidhinishwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania.

Aidha, TCRA imebaini pia, kuna baadhi ya Makampuni au wafanyabiashara wanaoingiza au kusambaza nchini Tanzania vifaa vya mawasiliano na simu bila kuwa na leseni kutoka TCRA kwa ajili ya kuingiza au kusambaza vifaa vya mawasiliano ya kielektroniki.

Kwa mujibu wa Kifungu cha 23 (1) (b) na (c) cha Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta iliyofanyiwa marejeo mwaka 2022, wasambazaji wa vifaa vya kieletroniki wanatakiwa kuwa na leseni halali toka TCRA. Vilevile kifungu cha 83(1) cha Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta kinaelezea umuhimu wa vifaa vya kieletroniki vinavyoingia nchini kuidhinishwa na TCRA.

Vivyohivyo, Kanuni ya 27 (1) ya Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (Viwango vya Vifaa vya Mawasiliano ya Kielektroniki na Usimamizi wa Taka za Kielektroniki) 2020 inaainisha adhabu kwa mtu yeyote atakayebainika kuuza, kuingiza au kusambaza nchini bidhaa au vifaa vya mawasiliano ikiwemo simu ambazo hazijaidhinishwa na TCRA.

HIVYO BASI, TCRA, inautaarifu Umma na wafanyabiashara wote wa vifaa vya mawasiliano ikiwemo simu ambazo hazijaidhinishwa na TCRA, kuhakikisha wanatuma maombi TCRA ya kuidhinisha Simu au vifaa hivyo maramoja na wale wasiokuwa na leseni stahiki za kuingiza nchini na kusambaza simu au vifaa vya mawasiliano kuacha mara moja kufanya biashara hizo mpaka pale watakapo pata leseni husika kutoka TCRA.

Kwa ambaye atashindwa kutekeleza ilani hii, TCRA haitasita kuchukua hatua za kiudhibiti na kisheria bila kutoa taarifa nyingine.
 
Mimi kama machinga nitajuaje kuwa chaja ya simu ninayouza haihitajiki nchini mwangu?
 
Back
Top Bottom