TCRA: Wenye akaunti ‘feki’ kukiona

TCRA: Wenye akaunti ‘feki’ kukiona

TCRA wamekosa kazi! Wameambiwa wakusanye zile bil 400 toka makampuni ya simu....mnahangaika na account fake!! Mtaweza kudhibiti? Huyo James Kilaba jina sio lake! Sasa nani fake zaidi hapo??? Aache umbulula!! Wakusanye kodi aachee mambo yasiyo na faid kwa Taifa!!!
MAMLAKA ya Udhibiti wa Mawasiliano hapa Nchini (TCRA) imewaonya watumiaji wa mitandao ya kijamii wanaojisajili katika mitandao hiyo kwa kutumia majina na taarifa za uongo, anaandika Charles William.

James Kilaba Kaimu Mkurugenzi wa TCRA amesema, vitendo vya watu kujisajili katika mitandao ya kijamii kwa kutumia majina na taarifa zisizo sahihi, ni kosa kisheria na kwamba wanaofanya hivyo watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Kilaba ameyasema hayo leo, wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuongeza ufahamu kuhusu matumizi sahihi na salama ya mitandao ambayo inasimamiwa na Kitengo cha dharura cha kuitikia matukio ya usalama kwenye mitandao hapa nchini (TZ-CERT).

“Tumeamua kuzindua kampeni hii ili kuwasaidia wananchi kuepuka makosa ya kimtandao na kuepuka kufanyiwa utapeli au wizi mitandaoni kwa sababu matukio mengi ambayo yamekuwa yakiripotiwa au kulalamikiwa yanazuilika kwa watu kupewa elimu ya matumizi sahihi ya mitandao,” amesema Kilaba.

Kampeni hiyo ya kuongeza ufahamu kuhusu matumizi sahihi na salama ya mitandao, itafanyika kupitia matangazo ya redio, televisheni, magazeti pamoja na mitandao ya kijamii ambapo katika mitandao ya kijamii itajulikana kama, “Darasa mtandao”.

“Miongoni mwa mambo ambayo tutawafundisha wananchi ni kutoweka wazi taarifa zao binafsi zote katika mitandao, kubadili na kutunza neon la siri (password), kutojibu ujumbe unaosema umeshinda bahati nasibu na mengineyo mengi,” amesisitiza Kilaba.
 
Hilo linaweza kabisa kuwa kweli, lakini pia inategemea ni namna gani JF itakavyoamua kupambana na hii Serikali dhalimu inayotaka kuua freedom of speech hivyo mwenye haki ya kuongea nchini abaki kuwa dikteta uchwara tu SKA Mungu wa Ikulu.

muda wetu hapa jf unahesabika...
 
Utabiri wa Shaban Robert ndani ya riwaya za KUSADIKIKA , KUFIKIRIKA na MFALME J.U.H.A .ndo unatimia sasa....
Kumbe mtunzi aliona mbali...!!!!
 
Mmeshindwa tu kuyasimamia Makampuni ya simu kwenye usajili wa line tu, ije kwenye mitandao? Facebook wenyewe wameshindwa hayo Ndio maana kuna account fake, sasa tuambieni Sheria ya JF inaruhusu watu kutumia majina fake, nyinyi mmasema ni kosa kisheria, ina maana mnampango Jf ikate roho?
Siku mkianza kukamata fake account basi ndio itakuwa mwisho wangu kutumia mitandao
Kwanza waanze na Makonda ambaye ana akaunti fake za kujibizana na wabaya wake
 
Kuna jambo moja hapo, aidha huyo mtu wa TCRA ni mjinga tu kama walivyo wengi kipindi hiki au ujumbe sahihi wa kilichozungumziwa haukueleweka na chanzo cha hii habari.
Inawezekana pia yote mawili yakawa possible.
 
Jpm aliwatumbua watumishi wa NIDA kwa kutumia mabilion ya fedha ilhari wananchi bado hawajapata vitambulisho, sasa aanza na huyu mkurugenzi wa TCRA James kilaba kazima kimeo changu kesho yake wajanja wakakifungua na nakitumia mpk leo
 
Tunae bwana Vincent Mungi humu JF, ni vizuri akafafanua hii habari.

Maana naona habari imejichanganya.
 
Mmeshindwa tu kuyasimamia Makampuni ya simu kwenye usajili wa line tu, ije kwenye mitandao? Facebook wenyewe wameshindwa hayo Ndio maana kuna account fake, sasa tuambieni Sheria ya JF inaruhusu watu kutumia majina fake, nyinyi mmasema ni kosa kisheria, ina maana mnampango Jf ikate roho?
Siku mkianza kukamata fake account basi ndio itakuwa mwisho wangu kutumia mitandao
Daaa mr Hero umetema cheche na sumu ya kweli kabisa
 
Back
Top Bottom