TCRA: Wenye akaunti ‘feki’ kukiona

TCRA: Wenye akaunti ‘feki’ kukiona

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2015
Posts
14,242
Reaction score
34,917
MAMLAKA ya Udhibiti wa Mawasiliano hapa Nchini (TCRA) imewaonya watumiaji wa mitandao ya kijamii wanaojisajili katika mitandao hiyo kwa kutumia majina na taarifa za uongo, anaandika Charles William.

James Kilaba Kaimu Mkurugenzi wa TCRA amesema, vitendo vya watu kujisajili katika mitandao ya kijamii kwa kutumia majina na taarifa zisizo sahihi, ni kosa kisheria na kwamba wanaofanya hivyo watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Kilaba ameyasema hayo leo, wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuongeza ufahamu kuhusu matumizi sahihi na salama ya mitandao ambayo inasimamiwa na Kitengo cha dharura cha kuitikia matukio ya usalama kwenye mitandao hapa nchini (TZ-CERT).

“Tumeamua kuzindua kampeni hii ili kuwasaidia wananchi kuepuka makosa ya kimtandao na kuepuka kufanyiwa utapeli au wizi mitandaoni kwa sababu matukio mengi ambayo yamekuwa yakiripotiwa au kulalamikiwa yanazuilika kwa watu kupewa elimu ya matumizi sahihi ya mitandao,” amesema Kilaba.

Kampeni hiyo ya kuongeza ufahamu kuhusu matumizi sahihi na salama ya mitandao, itafanyika kupitia matangazo ya redio, televisheni, magazeti pamoja na mitandao ya kijamii ambapo katika mitandao ya kijamii itajulikana kama, “Darasa mtandao”.

“Miongoni mwa mambo ambayo tutawafundisha wananchi ni kutoweka wazi taarifa zao binafsi zote katika mitandao, kubadili na kutunza neon la siri (password), kutojibu ujumbe unaosema umeshinda bahati nasibu na mengineyo mengi,” amesisitiza Kilaba.
 
Mmeshindwa tu kuyasimamia Makampuni ya simu kwenye usajili wa line tu, ije kwenye mitandao? Facebook wenyewe wameshindwa hayo Ndio maana kuna account fake, sasa tuambieni Sheria ya JF inaruhusu watu kutumia majina fake, nyinyi mmasema ni kosa kisheria, ina maana mnampango Jf ikate roho?
Siku mkianza kukamata fake account basi ndio itakuwa mwisho wangu kutumia mitandao
 
waambie watueleze kupanda kwa bei ya vifurushi wao pia wanahusika ama LA.. kama hawahusiki ina maana hawaoni? na kodi pia imepanda katika miamala ya simu..
 
Msituzingue na mkitaka mzifunge ila suala la jina halisi la mtu nyinyi mnajuaje ili mradi mtu havunji sheria tatueni kero zetu acheni kufuatilia vitu kama ivo
 
Imeshakua Nchi ya matamko kila mtu na lake anavyojisikia mara wamachinga waondolewe mwingine wamachinga wasibugudhiwe, mara uniform za polisi, yaani ili mradi vululuvululu
 
Back
Top Bottom