TCRA: Utoaji wa Leseni za Maudhui Mtandaoni umesitishwa hadi Juni 30, 2021

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,014
9,883
Mkuu wa TCRA Kanda ya Ziwa, Mhandisi Mihayo akizungumza kwenye Usiku wa Waandishi wa Habari na Wadau wa Habari Kanda ya Ziwa katika ukumbi wa Gold Crest Hotel Jijini Mwanza.

Mamlaka ya Mawasiliano ya Tanzania (TCRA) imetangaza kusitisha utoaji wa leseni za Maudhui Mtandaoni kwa muda kuanzia Januari 28,2021 hadi Juni 30,2021.

Akizungumza leo Jumatatu Februari 1,2021 kwenye Usiku wa Waandishi wa Habari na Wadau wa Habari Kanda ya Ziwa katika ukumbi wa Gold Crest Hotel Jijini Mwanza, Mkuu wa TCRA Kanda ya Ziwa, Mhandisi Mihayo amesema hatua ya kusitisha utoaji leseni kwa Blogs na Online Tv inatokana na kuendelea kuwepo kwa ukiukwaji mkubwa wa matumizi sahihi ya mtandao.

“Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuanzia tarehe 28 Januari, 2021 imesitisha utoaji leseni za maudhui mtandaoni kwa muda hadi tarehe 30 Juni 2021 ili kutoa fursa kwa TCRA kufanya tathmini na kuja na hatua muhimu za kurekebisha dosari nyingi zilizojitokeza”,amesema Mhandisi Mihayo.

Mhandisi Mihayo pia amewataka watoa huduma wa sekta ya utangazaji kutekeleza matakwa ya kanuni ya uendeshaji ikiwemo kuwalipa mishahara watumishi wao.

Aidha amewasihi waandishi wa habari kupendana na kushirikiana na kuhakikisha wanajiendeleza kielimu kuanzia ngazi ya Diploma ili kukidhi vigezo vinavyotakiwa.

Itapendeza sana ikiwa TCRA wataondoa leseni, Nchi zote Duniani hadi zilizoendelea hawajawawekea masharti ya kulipia leseni kwa gharama kubwa watu wao, wanamiliki blogs na youtube channel kwa UHURU MKUBWA, Kuna Kijana mmoja wa Kimarekani ana Blog zaidi ya 10 na yupo huru kuongeza. Serikali zao wanawaacha ili watumie fursa ya mtandao kukuza uchumi.

Kwa sababu wanaamini kodi wanayolipa inatosha. Naomba na serikali yetu ilione hili kwani kuna vikwazo vikubwa kwa vijana wanaotaka kujiajiri.

Mfano mtu una wazo zuri unataka kulifanyia kazi kwa kufungua Youtube Channel lakini unakutana na kikwazo cha Leseni Tsh Milioni 1. Pesa hiyo kwa makampuni na wanahabari wakubwa inaweza kuwa ni ya kawaida ila kwa kijana ambaye anamiliki simu tu au laptop milioni moja ni pesa nyingi sana.

Kama itakuwa wanaona haiwezekani kuondoa leseni basi waweke gharama nafuu ambazo hata mtu wa kipato cha chini aweze kumudu. Kwa mfano wakisema Leseni Tsh 100,000 au 200,000 angalau mtu anaweza kujitutumua na kuipata, ila milioni ni kubwa kwa kweli, Tunaomba serikali yetu iliangalie hili ili vijana waweze kujikwamua kiuchumi kupitia fursa mbalimbali zinazopatikana mtandaoni.

Mimi nina wazo la kuanzisha YOUTUBE CHANNEL lakini huu mwaka wa pili bado sijafanikiwa kupata hiyo ada ya leseni, naona kabisa hata idea yenyewe inaenda kuishia hewani.
 
Nipe iyo idea.
 
KAZI IPO KWA KWELI, KAMA YOUTUBE NDIO KUNA UTOPOLO MWINGI, VICHANNEL VYA AJABU AJABU TU VINAANZISHWA
 
Ni mimi sijaelewa au ni nini? Inamaana hakuna blog wala online tv itafunguliwa kwa miezi sita?
 
Wana bodi,

Hivi karibuni, mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) ilifanya maamuzi ya kusitisha kutoa leseni mpya kwa online TVs na Blogs zote nchini. Inasemekana kwamba maamuzi haya yalifanywa kutatua tatizo la ukiukwaji wa maadili na kanuni. Kama mtumiaji wa huduma zinazo tolewa na vyombo hivi vya habari ninajiuliza kama maamuzi yenyewe yalifanywa kwa kufata kanuni zilizopo au ni maamuzi holela yaliyo fanywa na watu wachache.

Mfano mkubwa wa sehemu ambayo ni blog ila sio blog rasmi ni Jamii Forum yenyewe. Nina fikiri kwamba kwa kawaida kwenye kitengo chochote, lazima adhabu nyingi ziwepo (kama vile faini na suspensions kwa vyombo husika) kabla ya maamuzi ya mwisho ya kuamua kufungia chombo chochote cha habari. Vile vile ni muhimu kwa TCRA kuwa na kanuni kwa ajili ya vyombo hivi vya habari kabla ya kuchukua maamuzi yoyote.
.
 
Jakaya ndio katufikisha hapa.

Yaan Nchi alikabidhiwa mungu wa mingu, mungu wa mababu namababu, anayependa kila Chombo cha habari kimsifiee.

Alafu kuna Mbwa wa kijani wa Lumumba wanaowaza kwa matako, utasikia " Vijana Jiajirini kwenye kilimo na ufugaji".....

Kwa kilimo kipi? Kwa ufugaji upi? Mimi saizi hata uwe ndugu yangu, Ukiniomba hata Mia, HUPATI NG'OOO ili mradi tu niwe najua ni wa CCM.

Huo U-CCM na ufedhuli wake, upeleke hukohuko kmmmake.
 
Wana bodi,

Hivi karibuni, mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) ilifanya maamuzi ya kusitisha kutoa leseni mpya kwa online TVs na Blogs zote nchini. Inasemekana kwamba maamuzi haya yalifanywa kutatua tatizo la ukiukwaji wa maadili na kanuni. Kama mtumiaji wa huduma zinazo tolewa na vyombo hivi vya habari ninajiuliza kama maamuzi yenyewe yalifanywa kwa kufata kanuni zilizopo au ni maamuzi holela yaliyo fanywa na watu wachache.

Mfano mkubwa wa sehemu ambayo ni blog ila sio blog rasmi ni Jamii Forum yenyewe. Nina fikiri kwamba kwa kawaida kwenye kitengo chochote, lazima adhabu nyingi ziwepo (kama vile faini na suspensions kwa vyombo husika) kabla ya maamuzi ya mwisho ya kuamua kufungia chombo chochote cha habari. Vile vile ni muhimu kwa TCRA kuwa na kanuni kwa ajili ya vyombo hivi vya habari kabla ya kuchukua maamuzi yoyote.
.
chanzo cha taarifa yako ni kipi
 
chanzo cha taarifa yako ni kipi
TBC online
Screenshot_20210216-051022_Instagram.jpg
 
Back
Top Bottom