TCRA yazindua mfumo ulioboreshwa wa utoaji wa leseni mtandaoni

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
666
835
TCRA YAZINDUA MFUMO ULIOBORESHWA WA UTOAJI WA LESENI MTANDAONI.

Leo 31 Julai,2021.

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imefanya uzinduzi wa Mfumo ulioboreshwa wa Utoaji wa Leseni kwa njia ya Mtandao. Mgeni Rasmi katika uzinduzi huo alikuwa Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt Faustine Ndugulile. Uzinduzi huo uliweza kuhudhuriwa na Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Lugha Bashungwa pamoja na Msemaji Mkuu wa Serikali Ndugu Gerson Msigwa.

Mfumo wa utoaji wa Leseni za Mtandao ulioboreshwa unatarajiwa kutoa Leseni za aina mbili, Leseni Kubwa kama vile za Makampuni ya Simu, Vituo vya Utangazaji na Ujengaji wa Miundombinu ya Mawasiliano pamoja na Huduma za Intaneti. Leseni hii inahitaji uwekezaji mkubwa kwaajili ya kutoa huduma za mawasiliano pamoja na Intaneti. Maombi ya leseni hii yanahitaji kuridhiwa na Mawaziri wenye dhamana ya Mawasiliano na Utangazaji.

Kwa upande wa Leseni ndogo Uwekezaji wake sio mkubwa na muda wake ni miaka 3. Leseni zitakazotolewa hapa ni Maudhui Mtandaoni, Redio za Mtandao, Blogu, Mitandao ya Kijamii, Television za waya, Kuingiza Vifaa vya Mawasiliano pamoja na Kusambaza Vifaa vya Mawasiliano. Mfumo huu utakuwa na ufanisi wa Utoaji wa Huduma za Leseni kwa muda mfupi, kwa Leseni ndogo kwa muda wa siku 5 na Leseni kubwa kwa siku 45.

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt Faustine Ndugulile ametoa pongezi kwa TCRA kwa kutengeneza Mfumo wa utoaji wa Leseni kwa njia ya Mtandao pamoja na kuwatumia Wataalam wa ndani kutengeneza mfumo huo. Dkt Faustine aliendelea kwa kusema,
"Dunia inapita katika mabadiliko makubwa ya TEHAMA, hivyo hatua budi kuboresha mifumo yetu ya upatikanaji wa Leseni kwa wakati na wepesi zaidi kama maelekezo ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ya kuboresha upatikanaji wa huduma Mtandaoni" alisema Dkt Faustine

Aidha Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo Mhe Innocent Bashungwa amempongeza Dkt Faustine Ndugulile kwa Mabadiliko makubwa katika Utendaji wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari. Lakini pia ameiomba TCRA kuharakisha utengenezaji wa mfumo wa ukusanyaji wa Mirahaba ya kazi za Wasanii ili kuboresha pato litokanalo na kazi za Wasanii

IMG-20210731-WA0038.jpg

IMG-20210731-WA0037.jpg

IMG-20210731-WA0036.jpg

IMG_20210731_120208_628.jpg

IMG_20210731_120208_629.jpg
 
Kutoa leseni wanaweza ila kudhibiti uhalifu wa kimtandao hawawezi.
 
Back
Top Bottom