Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 59,019
- 132,759
Mkuu FP, asante kwa heri ya mwaka mpya heri na wewe!Pasco,
Saa nyingine kaka UNAANDIKA (unaongea) kama hawa watalawa wa sasa wa Tanzania!, Inasikitisha na sijui kama ni wewe yule yule wasiku zote.
Nina maswali Pasco ,
1. Mkuu yule mama anayeuza mama nitilie anayeishi Buguruni malapa na yule msukuma mkokoteni wa Kwa Mtogole waliokuwa na TV yao wakanunua antenna ya mwiba uliotengenezwa kwa tubelights mbovu na waya mbovu wakawa wanashika Local TV kwa sasa ndio basi UNATAKA wasione tena TV au mpaka waende Bar Sinza?. Na je wana uwezo wa kwenda Bar?
2. Yule mzee kule Mwanerumango naye vipi? alipie elfu 10 kila mwezi? akanunue vifaa elf 62 kisha alipie kila mwezi?
3. Mkurugenzi wa TCRA aliwahi kusema kuwa kuna king'amuzi utanunua elf 39 kisha utaona channels ulizokua anaona bure! yaani sio unajiunga na kampuni flani kwa mpango wa subscription flani NO, unanunua basi. Alizungumza hayo Power breakfast ya clouds fm. Imekuaje
Pasco nahisi harufu ya Ufisadi katika wizara ya "RAIS" "wao" mtarajiwa.
Mbongo mpe nafasi ya mabadiliko lazima atavuruga au kunukisha Rushwa.
Hivi nishakwambia, happy nyu year?. basi hepi nyu yiaaa dear Pasco
FP
Mkuu Pasco, point no. 1 unaposema TV havitarusha tena matangazo vitakuwa "content providers only" una maana gani?. Kama ni matangazo ya biashara mbona bado yanarushwa? Pamoja na ku-cut costs hizi TV zinapata vipi faida?
Mkuu Kibanga, asante kunijibia kwa Jembe_Ulaya, kwa kuongezea tuu, Tanzania tumekuwa na vituo vichache vya TV kwa sababu zamani ili kumiliki TV ilikuwa lazima uwe na Studio na Transmiters ambazo ni very expensive!.Jembe kilichofanyika ni kupunguza majukumu, wenye studio sasa ni Content Provider na Kurusha ni jukumu la Multplex ambao kitaifa wapo watatu, ila kwa mikoani wapo multiplex wengi tu na dhani unajua juu ya Cable providers , hawa pia ni Multplex tokea kitambo.
Mkuu Kibanga, siku hizi kupinga kwa nguvu zote kunageuka utamaduni!, unatakiwa upinge kwa nguvu zote kitu unachokijua!, sasa wewe huo mfuko unaujua?, jee unajua umeisha fanya nini?, jee unaujua mpango kazi wake kwa kipindi kifupi, cha kati na kirefu kijachocho?!. Jee ukikuta hizo hoja ulizopendekeza ndicho ambacho mfuko unakiteleza kwa sasa, utaeleza unapinga nini?!.Pasco napinga kwa Nguvu zote kuwepo kwa huo mfuko huu ni ufisadi kwa aina mpya na na jua mfuko huu unapigiwa debe sana J. Makamba tokea akiwa Mbunge na sasa yupo wizara hiyo.
Mimi nilitegemea Funds hiyo ingeenda TTCL na kuwezesha kapuni ya taifa ya simu kufika vijijini ambapo makampuni ya kigeni yameshindwa kufika na ni hivyohivyo kwa TBC huu mradi kwa jinsi ulivyo muhimu kulikuwa hakuna haja ya kuungana na wachina kwani ni Mradi wenye Gharama ndogo sana na faida kubwa, Mpaka leo siamini kwanini wameshinda kufanya wenyewe. Tena huwezi amini techologia wanayotumia ni lowest katika mfumo wa digital at least Star tv naona wanakuja na DVB T2 ambayo ni one of the latest.
Kwanza naomba ku declare mimi
sio mtu wa TCRA, ila nimekuwa nikimsikiliza meneja mawasiliano wa TCRA
Bw. Inocent Mungy, hivyo kujikuta ninauelewa wa kutosha tuu kwa
kuanzia!.
Hili la kusema TCRA wamekurupuka sii kweli, matangazo walianza miaka
miwili kabla!. Kingamuzi kimoja, kinaweza kubeba chaneli mpaka 500!,
hivyo hata ingekuwa ni Star Times pekeyake, kingetosha, hivyo ving'amuzi
vingine vyote ni ziada tuu!.
Hapa Tanzania, hatuna hata kituo kimoja kilichokuwa kinarusha Digital
Signal za TV, japo TV zote zinafanya digital production lakini
transmitter zote, zinarusha analogy. Kinachofanyika sasa, TV zote badala
ya kuirusha ile analogy signal free to air hivyo TV kuzinasa bure,
signal hiyo sasa inapelekwa Star Media, na star media ndio wanairusha
kidigitali. Ili uweze kuelewa hii lazima kwanza uwe na DSTV na Star
Times, ukitazama quality ya picha ndipo utanielewa!.
Sasa ITV na Star TV wao wanakuja na kingamuzi cha cha kidigitali na
wanajitapa watarusha signal kwenye HD!, ili walitimize hili, inamaana
wao ITV na Star TV wataachana na zile transmiters za analogia na
watafunga za digitali!. Picha zao zitakuwa kama za DSTV!.
TV za ofisi za serikali, zinatumia king'amuzi chao!.
Pasco.
Wanatakiwa wajipange upya... Ghafla kupata habari Tanzani kunageuka kuwa ni bidhaa adimu......
Kwenye Zuku Clouds wapo kwenye upande wa Radio tu mkuu tena kitambo kwa upande wa TV baado kabsa,na huku Zuku local ni Channel Ten na TBC tu na salio likisha huona hizo channel Ten na TBC,ni tofauti na StarTimes ambao utaona hizo local hata salio likiisha,naona hapa ndio sheria za TZ zinapoangalia sura,kwa,mfano huyo mwenye sura ya Dstv au Zuku hakuna kuona local channels bure lakini huyu mwenye sura ya StarTimes lazima aonyesha local channels buure.Baba mmoja upendeleo kwa watoto kana kwamba wengine ni watoto haramuWakuu dunia ya leo hakuna kitu inaitwa bure tena, huku nchi za dunia ya tatu ndio tunaona mambo haya maajabu na hii inatokana na kulemazwa na mfumo wa kizamani wa bure bure
Labda tuangalie mfumo wa urushaji matangazo kwenye mfumo huu wa dijitali ili tuelewane
Zamani mtu yeyeto anaweza kuanzisha tv station yake labda akaiita miningits tv akawa anafanya vipindi vyake na kwa mfumo wa analojia maana yake alikuwa anaweka dish lake na kurusha na wenye tv zao za analogi wanadaka na kuendelea na maisha
mfumo wa dijitali umekuja kivingine maana sasa meningits tv atahitaji mtambo mkubwa wa kurusha matangazo kwa digitali kitu ambacho ni kigumu kwake
kinachofuatia ni watatokea watu wenye uwezo wa kurusha matangazo kwa dijitali na watakuwa wanakusanya tv station kadhaa za nje na ndani na kuziweka kwenye ving'amuzi vyao kisha kivirusha kidijitali na hii hufanyika kwa makubaliano ya kibiashara zaidi, hapa inabidi meningits tv aende kwa hawa jamaa ajiunge nao wamrushie matangazo yake
Hadi sasa tuna Ting, Startimes, Zuku na Easytv kama sijakosea, hawa ndio wanarusha matangazo kidijitali kupita vingamuzi vya fta na setelaiti
sasa wenye tv stations wanayo haki ya kuchagua kufanya kazi na nani kati ya wenye ving'amuzi hawa kulingana na offer zao, lakini ikaibuka hoja inamaana mtu atalazimika kununua ving'amuzi vingapi kuona local channel mbalimbali?
hapo sasa TCRA ikaja na ubabe kwa manufaa ya mwananchi kwa kuwalazimisha wenye tv stations 5 walizoita za kitaifa kuingia mikataba na wenye ving'amuzi wote.
Wakatoa agizo kwamba lazima ITV, EAT, STARTV, TBC na CHANNEL10 ziingie mikataba na wenye ving'amuzi wote na pia ikatoa amri wenye ving'amuzi warushe chaneli hizo tano bure hata kama muda wa package ya kawaida ukiisha basi chaneli hizi ziendelee kuonekana
Hadi hivi sasa kampuni zote zinarusha chaneli hizo tano lakini bado hawajaafikiana vizuri kibiashara kwasababu ya ulazima waliopewa na TCRA
Sasa hizi tv station zingine kama DTV, clouds nk wanalazimika kutafuta kampuni moja ya kufanya nayo kazi au kama wakiweza basi wataingia mkataba hata na kampuni zaidi ya moja, kwataarifa nilizo nazo Clouds tv wameshindwana na Startimes na wamekwenda Zuku
Kama hutaki usumbufu wa kulipia kwa mwezi walau kwa muda huu wakati bado tupo ugenini kwa dijitali basi unaweza kufunga dish la free chanel na utaweza kuona baadhi ya stations zinazorusha matangazo kwa setelaiti....na hii ni kwa muda tu maana biashara ikichanganya watazitoa na utalazimika kuziangalia kupitia ving'amuzi
.
Alichosema Mkurugenzi wa TCRA ni sahihi kabisa!, baada ya kukinunua hicho king'amuzi kwa hiyo elfu 39, utapata zile stesheni 5 za bure bila hata kufanya subscription!. Hiyo ndio basic!, sasa ukiamua kulipia ile subscription fee ya elfu 10 kwa mwezi ndio unapata kila kitu, sasa .
Mkuu Kibanga, siku hizi kupinga kwa nguvu zote kunageuka utamaduni!, unatakiwa upinge kwa nguvu zote kitu unachokijua!, sasa wewe huo mfuko unaujua?, jee unajua umeisha fanya nini?, jee unaujua mpango kazi wake kwa kipindi kifupi, cha kati na kirefu kijachocho?!. Jee ukikuta hizo hoja ulizopendekeza ndicho ambacho mfuko unakiteleza kwa sasa, utaeleza unapinga nini?!.
Juzi wakazi wa Mtwara, wameandamanishwa kupinga gesi isisafirishwe kuja Dar es Salaam, wengi ni masikini wa watu hata hawajui kuwa kumbe gesi ya Mtwara ni 14% tuu!, 86% iko high seas na sio mali ya Mtwara, wao wanapelekwa pelekwa tuu kama ling'ombe!.
Sipingi kupinga, get your facts right, then pinga according to the facts ay hand!, sio kupinga tuu ilimradi kupinga!.
Pasco.
Kwenye Zuku Clouds wapo kwenye upande wa Radio tu mkuu tena kitambo kwa upande wa TV baado kabsa,na huku Zuku local ni Channel Ten na TBC tu na salio likisha huona hizo channel Ten na TBC,ni tofauti na StarTimes ambao utaona hizo local hata salio likiisha,naona hapa ndio sheria za TZ zinapoangalia sura,kwa,mfano huyo mwenye sura ya Dstv au Zuku hakuna kuona local channels bure lakini huyu mwenye sura ya StarTimes lazima aonyesha local channels buure.Baba mmoja upendeleo kwa watoto kana kwamba wengine ni watoto haramu
Pamoja Sana!.Pasco,
Aisee tumeelewana.
kama unanunua tu once then free to air. Sina neno nimekubali; nilifikiri imebadilika.
Dah sijui kwanini sikuwahi hii dili ya DECODER dadeki!!
Mnyak-atari, acha hatari!, mimi sio mtu wa TCRA usiniletee hatari!.Mkuu clouds tv ipo zuku ila kubwa ni hilo kwa nini local channel za zuku sio bure na hao TCRA(akina Pasco) wala hawakusema hilo kwenye kampeni zao.Wao walisisitiza tu tununue ving'amuzi sio ving'amuzi gani,linchi letu bana!
Mfuko huo unawezesha kwa utaratibu wa "mwenye nacho ataongezewe!". TTCL sio ndio waliokuwa wa kwanza na wameshika mpini sasa kwenye mobile operators TTCL ndio wa mwisho!. TBC vivyo hiyo, ndio TV ya kwanza kuleta Digital Cameras hapa nchini na kutumia DV tapes mwaka 2000, wakati wengine wote wanatumia VHS!, sasa hivi 12 years later, TBC wako vile vile na zile zile DV zao, Star TV saa hizi wako kwenye HD tena wameshaachana na DV tapes, wao wako kwenye SD Card!, sasa uiwezeshe TBC ifanye nini?. Kama mfuko una nia ya dhati ya kuwawezesha vijijni kufikiwa na matangazo ya digital kweli, then wawawezeshe wenye Digitek!.Pasco naujua na ndio maana nikamtaja na Pioneer wa huo mpango kuanzia bungeni hadi wizarani hali ni hiyo kuwa makampuni kama voda, tigo, Airtel wapate ruzuku kwa kwenda vijijini kitu ambacho sio sawa na ushahuri ni huo kuiwezesha TTCL Mobile kufika huko.
Hilo la gesi naona ni walewale tena unakosea zaidi Baharini ni 78% 7% Lindi, 1% Pwani.
Hivi hiyo bahari ni Jamuhuri ya CCM au?
Wanacho hoji wana mtwara ni kuwa mnawaachacha vipi wao?
Je Mkoa, Wilaya, Kata, Kijiji wanafaidika vipi? Hat akwa huduma muhimu? Zahanati, shule, uborereshaji wa Uvuvi na Kilimo.
Pia unaweza kuwajibia ni vipi barabara miaka 51 haijakamilika lakini bomba la gesi miezi 18 ?
Mkuu Mnyaka, kwanza nikurekebishe, hawa TCRA sio wa kwangu, hii TCRA ni yetu wote!, kama alivyo JK ndiye rais wetu wote, waliomchagua na wasiomchagua, wanaompenda na wasiompenda ndiye rais wetu na TCRA ni mamlaka yetu!.PASCO,Huyo mkurugenzi ni bora angekuwa alisema hivyo.Walichokuwa wanasema na kusisitiza ni wananchi wahakikishe wananunua ving'amuzi ili mitambo ya analogy itakapozimwa waendelee kupata televisheni za nyumbani bure na za ziada za kulipia.Hawakuweka msisitizo unaotakiwa kuelezea utofauti uliopo kati ya hizo leseni ya ving'amuzi mbalimbali.
Wananchi hao wakawa wananunua bora king'amuzi kama walivyoshauriwa na hao TCRA wako.Usiwatetee kwamba wametoa elimu kuhusu utofauti huu unaousema wewe wa ving'amuzi.Wao walikomaa zaidi na kuwapa elimu wananchi wasitupe tv za migongo,jambo ambalo ni rahisi sana kueleweka wakaacha yale tatanishi kama hili la makampuni.
Sasa wale waliofuata maneno ya hilo li TCRA lako wakanunua ving'amuzi walivyovichagua(sio startimes,ting wala hiyo ambayo umesema ya star tv na ITV,ambayo bado haipo sokoni na tayari wana leseni!) wakitegemea kuwa wataona free local channel kumbe hawakuambiwa kuwa hayo makampuni hayana mandate ya kurusha free channel waende wapi sasa?
Ni serikali ipi ilipaswa kutoa elimu hii kuhusu huu utofauti wa makampuni?Kuwalaumu tu kuwa wabongo ni wazito sio kuwatendea haki kwani watu wengi sana wamenunua ving'amuzi vyao kabla hata ya tangazo lenu rasmi TCRA.Wasiliana na huyo ndugu yako Mungi mwambie aje huku kujibu kwanini watu waendelee kulipia local channel kisa hawakununua ving'amuzi tajwa na wao(TCRA) wala hawakuwaambia wasinunue hivyo ving'amuzi.Kwa nini wanasema sasa ambapo watu wameshanunua ving'amuzi hivyo visivyotakiwa.Huoni kama huku ni kuibiana na kunyanyasana?
Wanatumia decoda ya PVR kama ile ya DSTV!.Pasco umeijuaje Digitek kiasi cha kuipigia debe hivi? Tupe dondoo japo kiduchu basi!