TCRA, Tunaomba ufafanuzi

TCRA, Tunaomba ufafanuzi

meningitis

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2010
Posts
8,464
Reaction score
4,828
Naona usanii unaendelea kulitafuna taifa!kwa waelewa wa mambo tumeshanusa harufu chafu ya ufisadi ndani ya TCRA.nisiseme mengi bali nijikite kwenye swali langu au letu!

Ili niweze kuona local channels zote ninunue king'amuzi kipi?

This is a very serious question from the common mwananchi.
 
Swali zuri kwa january makamba kwakuwa vingine tunaona tatu,vingine nne, vingine mbili na kuna kipya kimeingia ni moja tu.

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Swali zuri kwa january makamba kwakuwa vingine tunaona tatu,vingine nne, vingine mbili na kuna kipya kimeingia ni moja tu.

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
tuliambiwa local channels zote zitakuwa bure ,tunachohitaji ni king'amuzi tu!au mimi nilielewa vibaya?
 
Weka dish mambo yote kwisha hamna kulipia kila mwezi wala kukosekana kwa chanel unazotaka. Tanzania ya leo wiziwizi,uongouongo,ufisadi
 
Weka dish mambo yote kwisha hamna kulipia kila mwezi wala kukosekana kwa chanel unazotaka. Tanzania ya leo wiziwizi,uongouongo,ufisadi

kaka unaponiambia 'dish' nakumbuka nilivyokuwa naogeshwa na mama enzi hizo.fafanua kama wewe ni mtumishi wa TCRA.
Dish lipi?mbona mlituambia king'amuzi ?tuwe serious katika hili!
 
Kwa mwendo huu wa hawa TCRA tutajikuta tuna ving'amuzi zaidi ya viwili kupata local Channels..... Gharama zaidi kwa mwananchi....
 
Kwa mwendo huu wa hawa TCRA tutajikuta tuna ving'amuzi zaidi ya viwili kupata local Channels..... Gharama zaidi kwa mwananchi....

ni zaidi ya viwili mkuu.
Star tv
itv
clouds
tbc
channel ten
mlimani tv
 
Aksante sana kwa swali zuri sana, mimi pia nilikuwa nasubiri kujua ni king'amzi kipi kinaonyesha channel zote tano maana nilisikia kuna mgogoro kati ya makampuni yanayouza ving'amuzi.
 
Hawawezi kujibu chochote, wanatekeleza matakwa ya mafisadi.

TCRA hawana maandalizi yoyote mbali ya kutoa discriminative policies kwa kampuni zinazotoa TV services.

Wanadhani ( hata serikali yenyewe inafikiria hivyo) kwamba TCRA wakishatangaza deadline ya analogy basi ndio kuwaandaa wananchi!

Ni Aibu kwa serikali.

Kama serikali inawajali wananchi inabidi waahirishe hadi 2015, serikali iandae wananchi wake, Na makampuni yanayorusha matangazo yajiandae kufikisha matangazo katika hali ya ubora
 
Wanatakiwa wajipange upya... Ghafla kupata habari Tanzani kunageuka kuwa ni bidhaa adimu......
habari inauzwa ?wakati sisi ndio wazalishaji wa habari hizo?
TCRA wamecopy na kupaste!shame!
 
Aksante sana kwa swali zuri sana, mimi pia nilikuwa nasubiri kujua ni king'amzi kipi kinaonyesha channel zote tano maana nilisikia kuna mgogoro kati ya makampuni yanayouza ving'amuzi.

me mbona nina cha startimes na local chaneli zote tano nazipata though bado nasubiri vingine nihame.elfu kumi na nane then chaneli zenyewe za kizushi tu.kwa anayetumia zuku anaweza tupa data zake?
 
Dstv naona local channel moja tu yaani TBC, zingine sioni na wala sijawahi ona hata siku moja, please anayejua namna ya kufanya hata nione Star TV tu. Msaada please
 
me mbona nina cha startimes na local chaneli zote tano nazipata though bado nasubiri vingine nihame.elfu kumi na nane then chaneli zenyewe za kizushi tu.kwa anayetumia zuku anaweza tupa data zake?
ITV na Star tv unazipata?
 
Naangalia ITV na EATV zooote hazina sauti SHAME ON THEM sijui ni hujuma kwa IPPMEDIA kutoka kwa hawa TBC??? Maana Startime ni wadau wao?
 
Kama hupati sauti chukua remote yako bonyeza track, nenda kwenye audio track, shift yellow to stereo, shusha chungwa left or right utapata sauti mkuu.
 
Mimi nazipata zoote zinazorushwa kwa sattelite tena vizuri bila chenga. Nunua sattelite dish utapata channel mpaka utakimbia halafu asilimia kubwa kama sio zote za sattelite ni Digital. Mimi nnakauelewa ka kuyarekebisha hayo madish kwa msaada tuwasiliane kwa namba 0767-387560
 
Naona usanii unaendelea kulitafuna taifa!kwa waelewa wa mambo tumeshanusa harufu chafu ya ufisadi ndani ya TCRA.nisiseme mengi bali nijikite kwenye swali langu au letu!

Ili niweze kuona local channels zote ninunue king'amuzi kipi?

This is a very serious question from the common mwananchi.

nunua satelite dish
 
Wakuu dunia ya leo hakuna kitu inaitwa bure tena, huku nchi za dunia ya tatu ndio tunaona mambo haya maajabu na hii inatokana na kulemazwa na mfumo wa kizamani wa bure bure
Labda tuangalie mfumo wa urushaji matangazo kwenye mfumo huu wa dijitali ili tuelewane
Zamani mtu yeyeto anaweza kuanzisha tv station yake labda akaiita miningits tv akawa anafanya vipindi vyake na kwa mfumo wa analojia maana yake alikuwa anaweka dish lake na kurusha na wenye tv zao za analogi wanadaka na kuendelea na maisha
mfumo wa dijitali umekuja kivingine maana sasa meningits tv atahitaji mtambo mkubwa wa kurusha matangazo kwa digitali kitu ambacho ni kigumu kwake
kinachofuatia ni watatokea watu wenye uwezo wa kurusha matangazo kwa dijitali na watakuwa wanakusanya tv station kadhaa za nje na ndani na kuziweka kwenye ving'amuzi vyao kisha kivirusha kidijitali na hii hufanyika kwa makubaliano ya kibiashara zaidi, hapa inabidi meningits tv aende kwa hawa jamaa ajiunge nao wamrushie matangazo yake

Hadi sasa tuna Ting, Startimes, Zuku na Easytv kama sijakosea, hawa ndio wanarusha matangazo kidijitali kupita vingamuzi vya fta na setelaiti

sasa wenye tv stations wanayo haki ya kuchagua kufanya kazi na nani kati ya wenye ving'amuzi hawa kulingana na offer zao, lakini ikaibuka hoja inamaana mtu atalazimika kununua ving'amuzi vingapi kuona local channel mbalimbali?
hapo sasa TCRA ikaja na ubabe kwa manufaa ya mwananchi kwa kuwalazimisha wenye tv stations 5 walizoita za kitaifa kuingia mikataba na wenye ving'amuzi wote.
Wakatoa agizo kwamba lazima ITV, EAT, STARTV, TBC na CHANNEL10 ziingie mikataba na wenye ving'amuzi wote na pia ikatoa amri wenye ving'amuzi warushe chaneli hizo tano bure hata kama muda wa package ya kawaida ukiisha basi chaneli hizi ziendelee kuonekana

Hadi hivi sasa kampuni zote zinarusha chaneli hizo tano lakini bado hawajaafikiana vizuri kibiashara kwasababu ya ulazima waliopewa na TCRA
Sasa hizi tv station zingine kama DTV, clouds nk wanalazimika kutafuta kampuni moja ya kufanya nayo kazi au kama wakiweza basi wataingia mkataba hata na kampuni zaidi ya moja, kwataarifa nilizo nazo Clouds tv wameshindwana na Startimes na wamekwenda Zuku

Kama hutaki usumbufu wa kulipia kwa mwezi walau kwa muda huu wakati bado tupo ugenini kwa dijitali basi unaweza kufunga dish la free chanel na utaweza kuona baadhi ya stations zinazorusha matangazo kwa setelaiti....na hii ni kwa muda tu maana biashara ikichanganya watazitoa na utalazimika kuziangalia kupitia ving'amuzi
 
nunua satelite dish

Wale wasio na uwezo wa kununua satelite dish unawashauri nini?

Btw, mimi kwa upande wangu tbc na channel ten ziko poa lakini itv, eatv na startv ndio mzozo. Matangazo yake yalikuwa yanastuck mara kwa mara lakini baadae yakakata kabisa (no service). Nimejaribu kupiga customer care hakuna msaada wowote.
 
Back
Top Bottom