TCRA naombeni majibu haya kabla ya kuhitaji alama za vidole za kila mmiliki line, je technology ya kisasa imewashinda?

Finger print ni kwa ajili ya kumtambua na kumthibitisha mtumiaji wa line

Sent using Jamii Forums mobile app
Ukimjua what value will add, kama security issues na wahusika wawe wabunifu sasa kidigital sio huu usumbufu ambao utaishia kupotezea watu muda na pesa.

Watakuja watawala ambao sio waoga kama hawa wa sasa wataona huu ujazz band na kushangaA kama sie.
 
Nikikipata TU kitambulisho haraka sana napeleka fp lakini siku NIKIPOKEA SMS ZA KITAP ELI HAKI YANANI TUTAKUTANA UPILATONI HUKOOO! Sitaki ujinga kabisa
 
Finger print ni kwa ajili ya kumtambua na kumthibitisha mtumiaji wa line

Sent using Jamii Forums mobile app
Kitambulisho cha Taifa kuna kuweka alama za vidole. Kuna haja gani tena kuweka alama hizo wakati tayari zipo kwenye database ya NIDA? Hawa TCRA watuambie ukweli tu. Yaelekea wanatafutwa wale walioandikisha majina yasiyokuwa yao. Lakini kama ni hivyo mbona rahisi sana, pitisha majina kwenye hiyo database, yatajitokeza yenyewe. Hili la vitambulisho vya NIDA ni usumbufu kwa mamilioni ya wananchi ambao huu ni mwaka wa tatu sasa wanasubiri bila mafanikio kuvipata.
 
Niliweka fingerprint wakati naprocess passport

Niliweka fingerprint wakati najiandikisha kupiga kura(kitambulisho cha kupiga kura nnacho)

Nikiweka fingerprint wakati wa kitambulisho cha taifa (Japo sijakipata mpaka Leo)

LEO NASAJILI LINE KWA KUTUMIA KITAMBULISHO CHA KUPIGA KURA AMBACHO NILIKIPATA KWA KUWEKA FINGERPRINT, Halafu unaniambia niweke tena fingerprint eti kwa ajili ya kutambuliwa? Kutambuliwa kwa namna gani tena?

Nonsense with high level of stupidity!!!
Mkuu nakushauri uache kwenda kusajiri ili usiwe "Nonsense with high level of stupidity"!!
 
JE KUMEFANYIKA TATHIMINI YA KUTOSHA AU MATAMKO YA MVUA
NAJUA KUNA FAIDA LAKINI TUANGALIE HASARA ZIFUATAZO
1.MAPATO KUSHUKA –hapa ni kwamba sasa hakutakuwa na wageni kutumia mawasiliano ya simu za mkononi,awali passport hasa pale airport zilitumika sasa ununuzi wa vocha kushuka
2.MAWAKALA KUKOSA KAZI –hili zoezi linafanyika kwa simu maalumu na mawakala wote hawana hizi simu unategemea hao mawakala watakula nini,BOMU la MAJOBLESS linaibuka .
3. ZOEZI LIMEKUJA KAMA MVUA YA VULI- hapa nakumbuka maamuzi ya mwakyembe kutaka ndoa zifungwe kwa kutumia cheti cha kuzaliwa wakati hata yeye hakuwa nacho kwa wakati huo.
4. HAKUNA ANALYSIS YA KUTOSHA KWA NINI WATU HAWANA VITAMBULISHO-hapa nashanga kwa nini hivi vitambulisho mtu asiletewe mtaani kwake ofisi za serikali za mitaa itarahisisha mpaka vijijini kule kwenye nyumba za tope.
5.WATEJA KUTOELEWA NINI NI NINI-hapa tutegemee queue ya nguvu katika callcentre za makampuni ya simu ,wateja wengi watapiga simu kuuliza maswali
:rolleyes::rolleyes::rolleyes::rolleyes::rolleyes::rolleyes:
6.SIM CARD KUUZWA BEI ZA JUU-hapa itatokea watu kusajiri sim card na kuuza kwa bei kubwa kwa sababu demand yaani soko litakuwa kubwa na kitakacho tokea ni yaleyale watu kutumia simcard siyo yake
7.HUDUMA ZA MPESA,TIGOPEA KUPUNGUA-hapa wateja wataanza kutoa fedha zao kwenye simu kwa kuhofia kufungiwa simcard zao, huduma za simBanking zitapungua na serikali kukosa kodi zinazotokana na miamala ya electronic money transfer na pay bill mbalimbali .
Unafikiri kuna mtu atashindwa kusajili laini kwa kukosa kitambulisho?
Ni rahis kupata kitambulisho kuliko kukaa bila simu
 
Cha ajabu kwenye requirement za ID wanataka tutumie national ID ambako tayari kuna fingerprints zetu. Why wasifanye integration ya hizo systems mbili. Why kuwe na duplicate fingerprints TCRA na NIDA?

Sent using Jamii Forums mobile app

Nimeliwaza sana hilo, ingekua rahisi zaidi wenye vitambulisho vya taifa vikatumika na kusiwepo ulazima wa kuchukuliwa tena alama za vidole.

Lakini unawezakushangaa alama za kule NIDA au NEC mifumo haifanyi kazi kama ilivyokusudiwa.

Pia haya mambo kuna sheria zake zinazoongoza kuchukua, kuhifadhi na kutumia taarifa za watu, sijajua upande huo umeangaliwa kiasi gani kutengenezewa sera au sheria.
 
Kwa upande wangu naona bado waafrika tutaendelea kuwakilishwa na rangi nyeusi, sio ya ngozi bali weusi wa fikra, kwa nini?
1. Utzrztibu tu wa kupata vitambulisho ni kama unatafuta msaada wa figo, blunders tupu.
2. Kusema twende katika Shops za mitandao kwa ajili ya kusajiri fingerprint najiuliza kwa yule wa matombo msalabani ambako hata laini ya simu alipanda basi ndo akampata wakala, huyu naamini kufika Tigoshop au Vodashop bado ni ndoto.
3.
TCRA wanakurupuka kwa kuiga taratibu za mataifa, leo ukifika marekani wanajiweza kiteknolojia na mifumo yao mi miongo na miongo na hawakuanza tu kama tunavyoanza sisi.
4.Anyway wazifunge tu, siku hizi hata hatupigi simu tunachati wasap, tutahamia email.
Kweli kabisa uweusi ni wa fikra sio ngozi
 
Fikiria kama TCRA pia.
Hili zoezi ni endelevu na hawajatangaza ukomo bali mwanzo.
Hakuna kampuni itakayopoteza wateja maadam ukamilishapo vigezo ikiwa ni pamoja na kupatiwa kitambulisho cha TAIFA nenda kakamilishe usajili.
Kwa wenye vitambulisho hivyo waanze kusajili upya laini zao.
Sent using Jamii Forums mobile app
Kama ni ivo hamna shda mi nlijua tar1 ndo mwisho coz hata hko nida sijawah kwenda nna alergy na maofisi ya serikali
 
Mkuu hutaki kutambuliwa? Fingerprints ni kwa ajili ya kukutambua in relation to that Simcard. Bado fingerprints zinatumika nchini mwetu kumtambua mtu hata huko ulaya bado wanawatambua raia wao kwa njia ya fingerprints na DNA. Acha waanze kwanza kututambua kwa fingerprints. We need to start from somewhere mkuu!
Wachana na hivyo viingereza vyako vya kipumbavu!! Hauwafikirii mawakala zaidi ya milioni tano watakaopoteza ajira zao unabwabwaja hovyo kwa kuwa umeshiba ugali!

Halafu wewe haujui kabisa Kiingereza! Next time andika kwa Kiswahili, usitutapishe hapa!
 
TCRA wako sahihi kabisa tatizo lenu ni kupinga kila kitu kama sera yenu kuu.

Kinachotakiwa ni uharaka wa kuwapata waharifu kama nyie mnaotukana ovyo hasa cdm siyo kuwa mnaropokaropoka tu kwenye mitandao bila ushahidi.

Mwisho siyo lazima kufanya hivyo acheni.
 
Mkuu hutaki kutambuliwa? Fingerprints ni kwa ajili ya kukutambua in relation to that Simcard. Bado fingerprints zinatumika nchini mwetu kumtambua mtu hata huko ulaya bado wanawatambua raia wao kwa njia ya fingerprints na DNA. Acha waanze kwanza kututambua kwa fingerprints. We need to start from somewhere mkuu!
Kazi ya Finger print na DNA ni ya NIDA, TCRA ni regulatory wa mawasiliano
 
Back
Top Bottom