TCRA naombeni majibu haya kabla ya kuhitaji alama za vidole za kila mmiliki line, je technology ya kisasa imewashinda?

Tabu yote ni vile hakuna national database...

Passport lazima uache finger prints, kwa national ID zoezi ni hilo hilo, sasa imehamia usajili wa simu, si ajabu ikaenda kwa mabenki na kwingineko...

Lets have kitu kama social security number, unatambuliwa na serikali pindi tu unazaliwa na vitu vingine vyote vina centralize hapo...

Sent using Jamii Forums mobile app
Hao wanapotezea muda watu
 
Nimeenda kusajiri line wakachukua saini yangu, wakapiga picha yangu passport size, copies za IDs zangu

Alafu naona sms kuwa niende tena kusajiri upya
Kiukweli SITAENDA wacha wafunge tu line

NIDA walichukua alama za vidole
NEC walichukua alama za vidole
bado TCRA nao tena?

Kwani alama za vidole huwa zina tabia ya kubadilika baada ya muda?

Hawawezi kuchua kutoka kwa wenzao NEC, NIDA?

Alama za vidole ni unique
kila mtu na zake dunia nzima!

sasa zimewachanganya?
Hapa kwa kweli kila mtu ana mwisho wa uvumilivu wake


Sent from my iPhone using JamiiForums
Mkuu mi na tiara eyii walichukua Sasa Tena na huku
 
Watu wanaweza tumia kitambulisho chako cha NIDA kusajili line na hiyo laini akatumia mtu ambaye sio wewe. Sasa endapo wakitumia fingerprint za NIDA bila kukuchukua alama za vidole upya kama unavoshauri huoni kuwa utakuwa linked kwenye tukio la uhalifu ingawa wewe mwenyewe si muhusika bali kimetumika kitambulisho chako tu kusajilia laini ambayo imehusishwa na uhalifu?

Fingerprint lazima zichukuliwe ili kuhakikisha kuwa fingerprint zako zinakuwa linked directly na simkadi yako na picha yako bila ya shaka yoyote.

Sent using Jamii Forums mobile app
Iko kitambulisho changu cha nida atakipata wapi ? Pia anayesajili si anapigwa picha yake halisi , ukiibiwa iko kitambulisho si unatoa taarifa polisi mkuu
 
Ni vyema ungetuambia vitambulisho vya taifa mmefikia wapi, sio kusumbua watu kama watoto wakati hamna jipya.
Subirini KWANZA tupate Vitambulisho vya taifa .siyo tutumie namba Kama magari.sisi hatuna haraka.
Halafu TV zipo radio zipo, toeni "DEMONSTRATION "JINSI MTAKAVYOTUMIA. HIZO FPS.
MIMI NINGEAMBIWA @ SIM CARD ITAFUNGUKA KWA FINGERPRINTS NINGEKUWA WA KWANZA.
NI USUMBUFU.
 
JE KUMEFANYIKA TATHIMINI YA KUTOSHA AU MATAMKO YA MVUA

NAJUA KUNA FAIDA LAKINI TUANGALIE HASARA ZIFUATAZO

1.MAPATO KUSHUKA –hapa ni kwamba sasa hakutakuwa na wageni kutumia mawasiliano ya simu za mkononi,awali passport hasa pale airport zilitumika sasa ununuzi wa vocha kushuka

2.MAWAKALA KUKOSA KAZI –hili zoezi linafanyika kwa simu maalumu na mawakala wote hawana hizi simu unategemea hao mawakala watakula nini,BOMU la MAJOBLESS linaibuka .

3. ZOEZI LIMEKUJA KAMA MVUA YA VULI- hapa nakumbuka maamuzi ya mwakyembe kutaka ndoa zifungwe kwa kutumia cheti cha kuzaliwa wakati hata yeye hakuwa nacho kwa wakati huo.

4. HAKUNA ANALYSIS YA KUTOSHA KWA NINI WATU HAWANA VITAMBULISHO-hapa nashanga kwa nini hivi vitambulisho mtu asiletewe mtaani kwake ofisi za serikali za mitaa itarahisisha mpaka vijijini kule kwenye nyumba za tope.

5.WATEJA KUTOELEWA NINI NI NINI-hapa tutegemee queue ya nguvu katika callcentre za makampuni ya simu ,wateja wengi watapiga simu kuuliza maswali

:rolleyes::rolleyes::rolleyes::rolleyes::rolleyes::rolleyes:

6.SIM CARD KUUZWA BEI ZA JUU-hapa itatokea watu kusajiri sim card na kuuza kwa bei kubwa kwa sababu demand yaani soko litakuwa kubwa na kitakacho tokea ni yaleyale watu kutumia simcard siyo yake

7.HUDUMA ZA MPESA,TIGOPEA KUPUNGUA-hapa wateja wataanza kutoa fedha zao kwenye simu kwa kuhofia kufungiwa simcard zao, huduma za simBanking zitapungua na serikali kukosa kodi zinazotokana na miamala ya electronic money transfer na pay bill mbalimbali .
Iyo no 2 na no 6 nakazia
 
Mkuu hutaki kutambuliwa? Fingerprints ni kwa ajili ya kukutambua in relation to that Simcard. Bado fingerprints zinatumika nchini mwetu kumtambua mtu hata huko ulaya bado wanawatambua raia wao kwa njia ya fingerprints na DNA. Acha waanze kwanza kututambua kwa fingerprints. We need to start from somewhere mkuu!
Je hivyo vitambulisho vya NIDA. WAMESHATOA KWA WANANCHI?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza niwapongeze NIDA kwa kuja na online copy ambayo inapatika katika website yao so wasio na ID itahitaji namba tu amabyo utaipata ofisi za NIDA then utaingia kwa web yao utajibu maswali machache utadowload Id yako safii....

Niseme Mim Nina mwaka na nusu sasa sijaipata Id yangu line yangu ya VODA ishafungwa mwezi Wa saba sasa.... Tigo ndo hivyo napumulia machine hii inanipa woga hata Wa kufanya transactions.

SASA BASI:

LEO nimeenda ofisi za tigo baada ya kupata namba ya id na copy.

MAJIBU

SYSTEM zetu hazikubali copy wala namba labda ujaribu mwezi Wa tano kuanzia tarehe moja.

Nilichokaa kinyongee nkaondoka SMS mnitumie nyie nakuja kutii wito mnanletea mapicha picha.
 
Kwanza niwapongeze NIDA kwa kuja na online copy ambayo inapatika katika website yao so wasio na ID itahitaji namba tu amabyo utaipata ofisi za NIDA then utaingia kwa web yao utajibu maswali machache utadowload Id yako safii....

Niseme Mim Nina mwaka na nusu sasa sijaipata Id yangu line yangu ya VODA ishafungwa mwezi Wa saba sasa.... Tigo ndo hivyo napumulia machine hii inanipa woga hata Wa kufanya transactions.

SASA BASI:

LEO nimeenda ofisi za tigo baada ya kupata namba ya id na copy.

MAJIBU

SYSTEM zetu hazikubali copy wala namba labda ujaribu mwezi Wa tano kuanzia tarehe moja.

Nilichokaa kinyongee nkaondoka SMS mnitumie nyie nakuja kutii wito mnanletea mapicha picha.


Duh, nafahamu kabisa, hili zoezi litakuwa gumu mno kwa miaka na miaka, na huenda wangemaliza tu kwa teknolojia kirahisi sana na kwa usahihi mkubwa, kuliko hii ya finger prints..!!
 
Kwa upande wangu naona bado waafrika tutaendelea kuwakilishwa na rangi nyeusi, sio ya ngozi bali weusi wa fikra, kwa nini?
1. Utzrztibu tu wa kupata vitambulisho ni kama unatafuta msaada wa figo, blunders tupu.
2. Kusema twende katika Shops za mitandao kwa ajili ya kusajiri fingerprint najiuliza kwa yule wa matombo msalabani ambako hata laini ya simu alipanda basi ndo akampata wakala, huyu naamini kufika Tigoshop au Vodashop bado ni ndoto.
3.
TCRA wanakurupuka kwa kuiga taratibu za mataifa, leo ukifika marekani wanajiweza kiteknolojia na mifumo yao mi miongo na miongo na hawakuanza tu kama tunavyoanza sisi.
4.Anyway wazifunge tu, siku hizi hata hatupigi simu tunachati wasap, tutahamia email.
 
Hellow watu wa Mungu, salam..

TCRA wamenishangaza sana, wanataka alama za vidole kwa kila mmiliki wa line ya simu.. Nimejiuliza maswali mengi mno sijapata jibu sababu sioni sababu yoyote ya msingi kufanya hivyo ukilinganisha na technology ya kisasa iliyopo.. Let's get down to details kwanini nawashangaa

1: Ukimiliki simu, TCRA wanajua line yako, simu yako, na IMEI ya simu yako..

2. Hata ukibadili line katika simu nyingine, ukawasha, still wanajua, unatumia simu gani, IMEI ipi, uko wapi at present position etc

3. Ukiamua, utumie mtandao kwa line yako, still TCRA wanajua IP address yako, uko wapi and a precise location.

4: Simu unazopiga, kuingia, sms, data usage, etc etc wanazo, hata utumie line mpya lakini haina jina still watapata details zote hizo..

5: Utaratibu wa sasa wa kusajili line mpya, unapigwa picha iliyo clear kabisa na ku upload ktk system, kisha kitambulisho ulichosajilia line kinapigwa picha na inaingizwa ktk system ya kampuni ya simu husika, na majibu yanarudi instantly, kuwa picha na kitambulisho vimekubalika, je picha ya passport size ya mmiliki wa line si zaidi ya finger print.

Swali rahisi kabisa, je alama ya vidole ndio security sign kubwa zaidi kuliko hizo correct digital details kama ni security mnahitaji? The answer is BIG NO definitely..

Je, alama ya vidole nchi nzima, let's say only 40% wenye line wamejiweza wakaenda, 60% hawajaweza, na mkawafungia tuseme, Serikali hawaoni watapoteza matrilioni ya shilingi kwa kuwapoteza hawa ambao hawajaenda kutoa alama ya vidole..?

Swali la mwisho na kubwa kabisa lenye kikwazo haswa, ukisema mwananchi aende na IDs za NIDA wengi hawana, IDs za Mpiga kura wengi hawana na wenye umri wa 18 and below hawana, ID za shule labda sekondari hapo wanazo ila akimaliza tu shule wanaacha so hizo hazifai, hili tu la IDs watapoteza wateja mamilioni, hii ina maana serikali itapoteza matrilioni ya shilingi kwa kupoteza wateja wengi mnooooo

Kama issue ni security, finger print sio realible these days, njia za kisasa za kidigitali nilizotaja hapo juu ndio very correct one and world wide are using..!!

Sijaelewa TCRA wamekaa na kujadili hasara kubwa itakayojitokeza sbb tu ya kutafuta finger prints za watu... Nimeshangaa sana. Siku hizi kumkamata mhalifu finger prints is nothing, just unatakiwa kujua line yake tu, basii. TCRA, msaidieni mh Rais wetu, apate mapato ya kutosha, hizi ideas zenu za kuja kuleta hasara kubwa unreasonably acheni. TCRA tayari mna TTMS, inawapatia kila kitu at your finger tips. Ukianzisha project hasa kama hii ya finger print nchi nzima lazima ufikiri mara elfu na elfu, big question is, DOES IT REALLY WORTH THE INVESTMENT? You can rethink again, mtapoteza trillions kwa maamuzi yasiyo na umuhimu mkubwa..!! Ni ushauri tu
Acha usome namba tu ili uache ufala wa kusifia sifia ujinga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hutaki kutambuliwa? Fingerprints ni kwa ajili ya kukutambua in relation to that Simcard. Bado fingerprints zinatumika nchini mwetu kumtambua mtu hata huko ulaya bado wanawatambua raia wao kwa njia ya fingerprints na DNA. Acha waanze kwanza kututambua kwa fingerprints. We need to start from somewhere mkuu!
Niliweka fingerprint wakati naprocess passport

Niliweka fingerprint wakati najiandikisha kupiga kura(kitambulisho cha kupiga kura nnacho)

Nikiweka fingerprint wakati wa kitambulisho cha taifa (Japo sijakipata mpaka Leo)

LEO NASAJILI LINE KWA KUTUMIA KITAMBULISHO CHA KUPIGA KURA AMBACHO NILIKIPATA KWA KUWEKA FINGERPRINT, Halafu unaniambia niweke tena fingerprint eti kwa ajili ya kutambuliwa? Kutambuliwa kwa namna gani tena?

Nonsense with high level of stupidity!!!
 
Back
Top Bottom