TCRA naombeni majibu haya kabla ya kuhitaji alama za vidole za kila mmiliki line, je technology ya kisasa imewashinda?

Kazi lazima iwe haraka na ifuate taratibu zake za kusajiriwa,hamuwezi acheni.

Fingerprint ni muhimu kote duniani
Tatizo ni kwamba wanashindwaje kuchukua details tulizotoa kwenye kupatikana kwa National ID maana system n moja kwa nini wasi integrate hzo system zao......
 
Hivyo vitambulisho vya NiDa tiyari vinafinga print sasa inakuwaje tuchukuliwe finga plint tena.... ?
 
CHANGAMOTO KUBWA NINAYOIONA KATIKA ZOEZI HILI NI KUWA VIAMBULISHO VINGI AMBAVYO TAYARI NIDA WAMEVITOA VINA ERRORS..SASA KWA ZOEZI HILI ITAKUWAJE
KUNA ERRORS ZA .....MIAKA YA KUZALIWA
MAJINA AMBAYO YAMEKOSEWA
MAJINA YALIYOBADILISHWA BAADA YA MTU KUPEWA KITAMBULISHO MIAKA KADHAA ILIYOPITA

NIDA MNAHITAJI KUSHUGHULIKIA TATIZO HILI .

PILI CHANGAMOTO ZA WAZEE WALIOKO VIJIJINI ..HAWA MNAWEZA WASAIDIAJE KUJA KUHAKIKI FINGEPRINTS KWENYE MADUKA YA SIMU.
 
Hellow watu wa Mungu, salam..

TCRA wamenishangaza sana, wanataka alama za vidole kwa kila mmiliki wa line ya simu.. Nimejiuliza maswali mengi mno sijapata jibu sababu sioni sababu yoyote ya msingi kufanya hivyo ukilinganisha na technology ya kisasa iliyopo.. Let's get down to details kwanini nawashangaa

1: Ukimiliki simu, TCRA wanajua line yako, simu yako, na IMEI ya simu yako..

2. Hata ukibadili line katika simu nyingine, ukawasha, still wanajua, unatumia simu gani, IMEI ipi, uko wapi at present position etc

3. Ukiamua, utumie mtandao kwa line yako, still TCRA wanajua IP address yako, uko wapi and a precise location.

4: Simu unazopiga, kuingia, sms, data usage, etc etc wanazo, hata utumie line mpya lakini haina jina still watapata details zote hizo..

5: Utaratibu wa sasa wa kusajili line mpya, unapigwa picha iliyo clear kabisa na ku upload ktk system, kisha kitambulisho ulichosajilia line kinapigwa picha na inaingizwa ktk system ya kampuni ya simu husika, na majibu yanarudi instantly, kuwa picha na kitambulisho vimekubalika, je picha ya passport size ya mmiliki wa line si zaidi ya finger print.

Swali rahisi kabisa, je alama ya vidole ndio security sign kubwa zaidi kuliko hizo correct digital details kama ni security mnahitaji? The answer is BIG NO definitely..

Je, alama ya vidole nchi nzima, let's say only 40% wenye line wamejiweza wakaenda, 60% hawajaweza, na mkawafungia tuseme, Serikali hawaoni watapoteza matrilioni ya shilingi kwa kuwapoteza hawa ambao hawajaenda kutoa alama ya vidole..?

Swali la mwisho na kubwa kabisa lenye kikwazo haswa, ukisema mwananchi aende na IDs za NIDA wengi hawana, IDs za Mpiga kura wengi hawana na wenye umri wa 18 and below hawana, ID za shule labda sekondari hapo wanazo ila akimaliza tu shule wanaacha so hizo hazifai, hili tu la IDs watapoteza wateja mamilioni, hii ina maana serikali itapoteza matrilioni ya shilingi kwa kupoteza wateja wengi mnooooo

Kama issue ni security, finger print sio realible these days, njia za kisasa za kidigitali nilizotaja hapo juu ndio very correct one and world wide are using..!!

Sijaelewa TCRA wamekaa na kujadili hasara kubwa itakayojitokeza sbb tu ya kutafuta finger prints za watu... Nimeshangaa sana. Siku hizi kumkamata mhalifu finger prints is nothing, just unatakiwa kujua line yake tu, basii. TCRA, msaidieni mh Rais wetu, apate mapato ya kutosha, hizi ideas zenu za kuja kuleta hasara kubwa unreasonably acheni. TCRA tayari mna TTMS, inawapatia kila kitu at your finger tips. Ukianzisha project hasa kama hii ya finger print nchi nzima lazima ufikiri mara elfu na elfu, big question is, DOES IT REALLY WORTH THE INVESTMENT? You can rethink again, mtapoteza trillions kwa maamuzi yasiyo na umuhimu mkubwa..!! Ni ushauri tu
Controling state does things to scare and intimidate people. The good news is that it is a matter of time that the controls get lost
 
TCRA wako sahihi kabisa tatizo lenu ni kupinga kila kitu kama sera yenu kuu.

Kinachotakiwa ni uharaka wa kuwapata waharifu kama nyie mnaotukana ovyo hasa cdm siyo kuwa mnaropokaropoka tu kwenye mitandao bila ushahidi.

Mwisho siyo lazima kufanya hivyo acheni.
Acha upumbavu wewe! Umekula maharage umevimbiwa sasa unajamba tu na kuamrisha watu kama tarishi!

Umefikiri kuhusu ajira za vijana zitakazoyeyuka?

Umefikiria kuhusu idadi ya watu wenye vitambulisho vya hiyo NIDA?

Haujafikiri kitu maana humo ndani ya kichwa chako hicho kikubwa pamejaa maboflo tu!!
 
waweze kupata wezi vizuri ukihiiba tu wanacheki finger print
Sent using Jamii Forums mobile app
Kutumia finger print siyo njia ya kukamata wezi sbb hii ni njia ya kuthibitisha kuwa mtumiaji wa laini ya simu ndiyo yeye. Simu zitaibiwa kama kawaida na watu wahack simu kama kawaida.
TCRA ilifungia baadhi ya simu imei kwa lengo la kupunguza wimbi za simu fake kuwepo mtaani lkn watu wamechange imei na kutumia kama kawaida na hawajakamatwa
Kuna simu zenye finger print kama TECNO na zingine lakn watu wanabypass finger print na wanatumia kama kawaida
Kuna issue ya Factory reset protection (FRP) lakn watu wanabypass na kutumia kama kawaida
Kuna simu zenye mfumo wa secure boot lkn watu wametengeneza DA FILE na wanabypass na issue inapiga kazi kama kawaida.
N.B
Issue ya finger print italinda usalama wa sim card yako na siyo simu. Mfano umeibiwa simu halafu mtu akatumia laini yako kumtukana kiongozi yyte au kusambaza taarifa za uongo, atakuja kukamatwa huyo mwizi au ww?
 
Back
Top Bottom