TCRA mnachofanya ni sio, mnadumaza nchi

Kilichonipeleka huko ni regional IP address
IP address ni kama plate number ya gari kwamba IP address za africa haziwezi ku operate kwa server iliyoko Europe ama China. Ni sawa na gari lako lenye plate number za tz haliwezi kuliendesha south Africa. Unless hicho kifungu sijakielewa wana maana gani ya kureport regional IP address. Kama wana maana IP address yoyote kutoka huko server iliko kwenye region hiyo hapo sawa.

Hii effectively kama ndivyo, unamwambia mwenye server zake china azihamishie Tanzania eti ku meet demands za TCRA.
Na pia kusajiri domain name kwa .tz ili iwe je? hiyo ni nick name tu haina lolote.
Mkuu mbona wazambia na wakenya wana drive kwetu?

Au mfano wako sio halisi?
 
Mleta mada umechanganya domain name na sever kwenye kila sentensi hadi inaboa.

Pia jaribu kutafiti hiyo dot tz chanzo chaje ni nini. Haipo tanzania pekee. Hao yahoo google na wengine uliotaja wana domain kila nchi. Kuna dot co.uk. kuna dot co.ke. kuna dot co.fr .... .co.cn dot co.za na kadhalika.

Kama kuna tatizo lingine lifafanue lakini si la kusema google na wenzake wana dot. com pekee. Wanazo za kila nchi
 
Rudia tena maada nzima. Sio usome reply moja unajikita kuchangia.
Kwanza uelewe kampuni zote siyo google. Pili google, yahoo wameweka hivyo ili ku localize contents kwamba unapokuwa Tanzania una search kitu google unaletewa resources na server zao zilizo karibu na wewe, hilo unatakiwa kulitambua kwa moyo wako wote. Hiyo ni traffic optimization na traffic cache. Umenipata??

Kampuni kama HUAWEI ama Dangote ama mimi mkamap.com, hawana regional cache umenipata. Nahivyo ni overheads zisizo na maana kumlazimisha mtu huyu kila nchi anunue domain name na anunue IP yake na azimanage manage pia, whatever the case, ama kwa kutumia proxy ama vyovyote vile ni ujuha kuwa na demand ya namna hiyo.

Na chamuhimu zaidi watakapokutaka uwe na IP address kutoka AFRINIC hii maana yake server zako lazima ziwe Africa. Ndiyo tunauliza tukiwapelekea za amazon ili iwe je na wazifanyie nini?

Na mwisho huoni ni ujinga, mimi nime host amazon UK harafu unanilazimisha dotz, ambayo ni aka tu? sasa dotz ili ikusaidie nini? contents ziko uk, IP address za UK, harafu wewe una demand domain lazima iwe dottz?? upuuzi tu huu.

Kutokana na hoja hiyo, ndiyo maana nafikiri na kuamini wanataka ukiwa na kampuni Tanzania na servers zako ziwe Tanzania, kitu ambacho kitachozorotesha maana nzima ya E-economy na kujenga impact hasi kwa Taifa ktk gurudumu la kusonga mbele.
 
Information Ecosystem haitaki masuala ya mipaka ya kisiasa, eti kwamba kampuni zinazooperate Tanzania ziwe na dot tz, halafu zikienda huko duniani Ruksa kuwa na nyingine.
Je leo Trump na Congress wakipitisha sheria ya kijuha kama hii ya kutaka makampuni ya Kimarekani popote pale duniani yawe na dot-us mna ubavu wa kuwakatalia kufanya kazi hapa tz?
TCRA wajiongeze, hii sheria haina maana.
 
Ndiyo mkuu, sheria ni mbovu haina maana na vilevile haina compatibility na reality on the ground. Nothing more nothing less.
 
Hapo ndipo sisi maboya tunahoji ninyi wasomi, watu kutumia mitandao Kutukana, kuzusha uongo, kujenga hofu katika jamii, kunakuzaje Uchumi?

Sheria iliyoundwa na Bunge la JMT ikaundiwa chombo (TCRA) cha kusimamia utekelezaji wa sheria hiyo, itaitwaje eti sheria ya chombo hicho? Na chombo hicho kina ubavu gani wa kuzibadilisha hiyo sheria? Hii ni sawa na kusema TRA wasisimamie sheria ya ukusanyaji Kodi sababu ni sheria ambazo watu fulani wawazipendi.

Hatua ya kwanza muhimu kwa binadamu kutatua tatizo linalokukabili, ni kujua na kukubali kuwa una tatizo. Usipoanza na hili itakuwa vigumu kuondokana na tatizo. Jamii forums wakitambua hawaendani na sheria za sasa za nchi ni kuangalia jinsi ya kujipanga ili waendane nazo si kutaka kupambana kwa kujifanya hawazikubali kanuni za mchezo hawatalimaliza tatizo.

TCRA pamoja na kusimamia ukuaji wa secta ya mawasiliano lakini pia inasimamia maudhui kwa ajili ya USALAMA wa taifa hili Kiuchumi na Utamaduni kwa sheria zilizotungwa na BUNGE sio TCRA
Dr. Martin Luther King Jr. nampenda sana huyu mtu alisema njia pekee ya kutii sheria ya kidhalimu na ya hovyo ni KUPINGA HIYO SHERIA KWA GHARAMA YOYOTE ILE, na hata Mungu anapenda hivyo.
 
Na
Ningeweza ningeomba Wenye Internet WAIZIMIE kabisa Tanzania isiwe na huduma za Internet tuone hayo mabenki na kampuni za simu na vitengo vingine km havijafa! Wao si wanajifanya kibri? Nazima tu tap, kwishneyi!
ngoja mpango wa trump, alisema waafrica mnamtusi kuwa kutumia internet ambayo wao ndio wametengeneza na wanaweza kuamua tu wakazima toka huko kwao tukarudi kwenye ukinga wetu wa kuandika barua na zile sijui za maneno 50.
 
Nadhani hili tayari limeanza kuathiri biashara.
Wale jamaa wachimba dhahabu wakubwa hapa tz wamemaliza kufanya migration kubwa ya mtandao wao december hii.
Nadhani haya ndio matokeo ya bugudha hizi. Server zao zote wamekimbizia SA. Labda wataalamu wa IT wanipe maelezo kidogo kuhusu migration nini nini na inasaidia nini kampuni kufanya haya iliofanya??
Naota kama ni
 
TCRA wanaharibu uchumi, sheria inatakiwa ziwe friendly kwa mjasilia mali na mwekezaji, ili wa generate uchumi kakamavu zaidi. Na hisi hizi sheria zilitungwa na mafisadi ili kuwalinda. Serikali inabidi waliangalie hilo.

Ushauri kwa serikali.
Wa outsource hiyo kazi, waipe kampuni ya nje mbali kabisa huko hata mashariki ya mbali, wazili review hizo sheria za TCRA kama zina compatibility na hali halisi na kama kweli zinaujenga uchumi wa Tanzania ama zinaubomoa.
 
MkamaP
Google wanatumia .co.tz na server zao haziko Tanzania, so kwa maoni yangu inawezekana pia kwa JF kutumia .co.tz na server kubaki huko ziliko.
Google Tanzania: Google
 
Yaani inauma sana. Hadi najiuliza hivi ni woga? ni kujipendekeza? Ujuha? Hivi hawa watu walisoma elimu gani iliyowajaza upumbavu mwing kias hiki?
 
Tumieni lugha ya staha...mnaposhauri ama kukosoa. Hata kama tuna hasira za kujaza gunia la debe sita. Huwezi kupewa majibu ama ushauri wako kutiliwa maanani kama unatanguliza lugha za kuudhi. Jifunze kushinda hisia za lugha chafu unapokwazika wakati unajiandaa kutoa maoni, ushauri, ama kuuliza swali.
-----------------
Mbona kama TCRA wamekanusha habari ya huyo Mwanasheria, tena kupitia verified user yao ya JF?
Weka link ya uzi hapa
 
Back
Top Bottom