Nchi ya maziwa na asali

Mkandara

JF-Expert Member
Mar 3, 2006
15,772
8,958
Majuzi nimelisikia Bunge letu tukufu wakijadili hoja ya URAIA PACHA na HADHI MAALUM kwa kina sana lakini yaonyesha wazi viongozi wetu hawajui maana wala tofauti ya mifumo hii miwili japokuwa ni wasomi wazuri.

Kwa sababu hizi inanilazimu kuufahamisha Umma, viongozi na Wabunge wanaojadili hoja ya Hadhi Maalum pasipo kutambua Sheria hizi zinatumikaje Kimataifa maana yaonekana wazi Bunge limejadili Muswada huu kwa Dhana ya Kisasa zaidi ya Uhalisia.

1. HADHI MAALUM

Hii ni kibali cha Sheria hutolewa kwa Wageni wahamiaji nchini ambao wana uraia wa nje (Permanent Resident au Green card) ili kuwawezesha wahamiaji hao kuishi nchi husika, huingizwa katika.mfumo wa kodi ili kuchangia katika mfuko wa Taifa pasipo kuomba work permit kila mwaka.

The all point ni kumwezesha mwajiriwa au mwekezaji aishi bila kuomba work permit kila mwaka kama hatua ya kwanza kabla hajaomba na kupewa Uraia wa nchi hiyo. na atapewa huduma zote za kuishi nchini kisheria, wakati bado anatambuliwa kama raia wa nchi alikotoka. Serikali haimpi Hadhi Maalum raia wake anayeishi nje ya nchi isipokuwa mhamiaji anayetaka kuishi ndani ya nchi.

2. URAIA PACHA

Asili yake ni baada ya kuundwa Umoja wa Mataifa UN nakupitisha sheria ya kutambua Mataifa yote duniani na HAKI za Utaifa wao (Sovereign). Hivyo, Wakoloni walokuwa wakiishi katika Makoloni yao, walilazimika kuunda Sheria ya Uraia Pacha ili waweze kuwa na HAKI miliki ama kuhodhi haki zote za Uraia wa makoloni hayo bila kupoteza Uraia wa nchi walizotoka.

Waingereza, Makaburu, Majarumani, Wafaransa, Wareno na kadhalika ndivyo walivyopata Uraia wa nchi zetu pasipo kupoteza Uraia wa makwao na serikali zao kupitia taasisi za fedha na Uwekezaji ziliwawezesha mikopo, zana na vifaa ili kuwekeza katika miradi mbali mbali nchini mwetu ikiwa ni pamoja na Kilimo, viwanda na Biashara nyinginezo.

Hivyo iliwasaidia raia wakoloni kuweza kuwekeza nchini wakachuma bidhaa toka nchi zetu na kuzipeleka kwao bila kuvunja Sheria za UN. Iweje sisi tunataka kufanya kinyume, badala ya kufikiria mikakati ya kumwezesha Mtanzania achume Ulaya na kuzirudisha Tanzania kama walivyofanya Wakoloni, leo hii karne ya 21 tunafikiria kuombana hati za Uraia wa makazi, urithi na sijui visa ya muda mrefu badala ya kutumia vijana wetu waishio nje kuwa mawakala wa kuuza mali zetu wenyewe nchi za nje.

Tunataka kupitisha sheria ya kumtambua raia wetu aishie nje kwa HADHI MAALUM ambayo haimpi haki ya kisheria kwenda kuishi na kuchuma nje akapeleka utajiri huo Tanzania. Maana Kisheria atakuwa anafanya utakasaji wa fedha (Money Laundry) ama ataonekana anasaidia Magaidi (funding Terrorist group). Ndio maana Mtanzania anayeishi nje hawezi kusafirisha fedha nyingi pasipo maelezo ya kina juu ya fedha hizo.

Kwa hiyo, Sheria hii tumefanya Kinyume kabisa. Anayetakiwa kupewa Hadhi Maalum ni mgeni mhamiaji Tanzania kama hatua ya kwanza kabla hajapewa Uraia wa Tanzania. Na Uraia Pacha ni hatua ya Kisheria kuhakikisha Raia wako anatambuliwa huko nje kama ni mgeni wa nchi fulani na anaweza kuchuma na kurudisha mapato yake kwao kama walivyotufanya Wakoloni.

Nipo tayari kupokea hoja au maswali yoyote yanayohusiana na maswala ya Hadhi Maalum au Uraia Pacha..

Karibuni
 
Umeeleza vizuri karne ya 21 watu/wanasiasa bado wanawaza kijima kabsa sijui wanachoogopa ni kitu gani au wanaona tishio kwa utawala wao na sio kwa maslahi mapana ya nchi.
 
Umeeleza vizuri karne ya 21 watu/wanasiasa bado wanawaza kijima kabsa sijui wanachoogopa ni kitu gani au wanaona tishio kwa utawala wao na sio kwa maslahi mapana ya nchi.
Yashangaza wanaogopa nini? Hata zile nchi zilokataa Uraia Pacha ni kwa sababu kuna Wanasiasa mahasimu walokimbia Utawala wa nchi zao kwenda kuomba ukimbizi nje na wamekuwa mwiba wa Serikali hizo.

Mfano mzuri ni India ambayo nawasikia Viongozi wengi wakiizungumzia. Sisi kina Lissu, Lema, Heche wote wanerudi na wanafanya Siasa ndani. Kwa hiyo hii sio sababu, Bila shaka wanaogopa vivuli vyao wenyewe ama kuna viongozi au Wabunge wamerithi mali na Utajiri ambao ndugu zao wanaishi nje?
 
Yashangaza wanaogopa nini? Hata zile nchi zilokataa Uraia Pacha ni kwa sababu kuna Wanasiasa mahasimu walokimbia Utawala wa nchi zao kwenda kuomba ukimbizi nje na wamekuwa mwiba wa Serikali hizo.

Mfano mzuri ni India ambayo nawasikia Viongozi wengi wakiizungumzia. Sisi kina Lissu, Lema, Heche wote wanerudi na wanafanya Siasa ndani. Kwa hiyo hii sio sababu, Bila shaka wanaogopa vivuli vyao wenyewe ama kuna viongozi au Wabunge wamerithi mali na Utajiri ambao ndugu zao wanaishi nje?
Nafikiri wanaogopa mwamko watakao uleta diaspora kwa nchi yao na juu ya haki za msingi za raia kikubwa wanaangalia maslahi yao na familia zao kwanza hata sio nchi
 
Back
Top Bottom