MPUNGA MMOJA
JF-Expert Member
- May 30, 2015
- 304
- 401
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeondoa zuio la kampuni za simu nchini kuwatumia mawakala kusajili laini za simu mitaani.
Akizungumza Jumatano Aprili 14, 2021 mkurugenzi wa mamlaka hiyo, Dk Jabir Bakari amesema mamlaka hiyo imeondoa zuio hilo na sasa kampuni za simu zitaendelea kuwatumia mawakala kufanya usajili.
Zuio hilo lilitolewa Februari 16, 2021 na utekelezaji wake ulitakiwa kuanza Mei mosi, 2021 ambapo usajili wa laini ulitakiwa kufanyika kwenye maduka ya kampuni husika.
“Kampuni za simu zinaweza kuendelea kuwatumia mawakala bila kuathiri usajili sahihi wa laini kwa mfumo wa kibayometria.”
“Hili litafanyika wakati tunaendelea kufanya tathmini upya ya namna bora inayoweza kutumiwa na watoa huduma kuwasimamia mawakala,” amesema akiwataka mawakala kutumia weledi katika utendaji wao wa kazi.
Chanzo: Mwananchi