TCRA: Kipindi cha Shule ya Uongozi cha Humphrey Polepole kinatolewa pasipo kuzingatia misingi, sheria na kanuni za huduma ya utangazaji

Kana siri nyingi za ushindi wa uchaguzi 2020
Wakiamua hakuna cha kuwazuia, hana kwa kuropokea labda huko nchi za mbali...

Ni ngumu kutofautisha maamuzi ya CCM na maamuzi ya serikali.

Hivyo kutoa siri za CCM sawa na kutoa siri za serikali, vivyo hivyo kutoa siri za serikali sawa na kutoa siri za CCM...
 
"Tutafundisha watu adabu awamu hii, adabu." Napenda haki ila polepole acha anyooshwe alijiona mungu-mtu kipindi fulani.

There is a rule of a finishing return.
 

Polepole ni ccm na ni sehemu ya serikali pia;
 
2015-2021 inetoa somo kubwa sana kwa vijana kuacha uchawa. Huyu si polepole ambae PS wote walitakiwa kushika simu zao ziwe standby maana haijulikani PS yupi atapigiwa simu kwenye kipindi hicho mubashara. Leo TCRA iliyo chini ya PS inamvimbia. Vijana tupunguze uchawa na kuheshimu watu, sponsor hufa
 
Wahuni walibaki wengi sana serikalini magufuli alitakiwa kuitawala tz kwa miaka 30 ili kuwamaliza na kizazi chao
 
⁶. Wahuni walianza na ghetto lake. Sasa kwenye vipindi. Watakuja kusema halipi kodi. Wataenda kusema gaidi. Baada ya hapo panya chali…
Mwana kulitafuta,mwana kulipata,Polepole amefanya wrong timing.Nahisi amepata fundisho maishani.
 
Ccm hawapendi ukweli ndio ajifunze kua jambo la leo kesho linaweza kua kwako.

Wamfute na uanachama wampe kesi ya kuhujumu uchumi
Tulio nyuma yake ni jeshi kubwa na kuu kabisa wahuni wanamtegemea mkuu wa majeshi msaliti kudumu kwao ila nguvu ya uzarendo hakuna wa kuizuia hata siku moja
 
Kwa kifupi, Polepole amepoteza uwezo wa kupambanua mambo ya msingi. Sikutegemea awe hamnazo kiasi hiki. Kwenye masuala ya kanuni, kuna mstari mwekundu (red line) ambao ukiuvuka huwezi kugeuka na kurudi nyuma yake tena. Ni kama kufa kwa nadhiri.

Akitumikia awamu ya tano alishiriki kupindisha misingi mikuu ya demokrasia. Kama akili yake inafanya kazi, leo hii hawezi tena kutarajia ile misingi irejee (kimiujiza) kulinda haki yake ya kujieleza (freedom of speech). Katika utawala wa jiwe hilo ilikuwa hatari kubwa sana sawa na kujitafutia kifo.

Conventional wisdom (busara ya kawaida) inamtaka akae kimya kabisa; aachane na siasa hata na uanaharakati. Hana tena moral credibility. Natumaini Bashiru analitambua hilo ndio maana katulia.
 
Unafikiri yanafanyika kwa bahati mbaya?

Unaamini Polepole “aliokotwa tu” kwa kipaji chake cha kubwabwaja na kupewa uKatibu Mwenezi wa chama dola?
 
Binafsi nakubaliana na shule ya polepole kwa asilimia kubwa, kwenye kuwanyoosha wahuni.

Ila TCRA wanavihoja uchwara ambavyo lazima ukubaliane nazo for the sake of social interest. Pole kwenye maswala ya COVID amepotoka ni ujinga kwenda against medical advice. Magufuli alikuwa na mitazamo yake ya ovyo pia.

Swala la bandari ambalo TCRA awajaligusua mtazamo wa polepole ni nonsense pia. Bandari ya Bagamoyo lazima ijengwe kwa sababu za kibiashara in the long run because is Dar heading towards a saturation point (ili swala ata Kakoko kalitolea ufafanuzi).

Issue ya Bagamoyo ni economic benefits kwa Tanzania wajenge TPA au wachina. Tatizo la wachina wana investment zingine ambazo TPA awazitaki na wachina awataki kujenga bila ya hizo investment za unyonyaji ambazo hazina maslahi kwa TPA.

Mie nadhani polepole aangaike na wahuni tunamuelewa sana kwenye hiyo agenda na kuachana na agenda zote za Magufuli he wasn’t perfect.

Hipo siku tutainamisha chungu watoke wahuni tukate vichwa; not otherwise kama wanavyofikiria wao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…