TBS, TCRA na TRA washindwa kuisaidia Serikali kuondoa spea feki za Simu. Mafundi simu waishia lockup wasijue lakufanya

mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
13,767
7,115
Wana Jf

Serilikali kupitia ajent zake za kitaifa kwa pamoja wanaungana kuikosesha mapata serikali na kuleta mtafaruku mkubwa kati ya mafundi simu na wateja wao.

TBS, TCRA na TRA zilivyoshindwa Nazi zao kila moja nitaelezea makosa yao

TBS wameshindwa kuajiri vijana wenye weledi kutambua vitu feki , kuna chinese copy nyingi za spea za simu na vitu vingine ambavyo ni bdublicated, refabrished vinavyoingiza nchini. Kuna kuna wafanyabiashara wauni kwa kutambua kuwa ni feki wananua na wanaimport kupitia ajency za serikali. Sio kwamba hawajui kabisa pengine rushwa inatembea.

TCRA hiki chombo kimeshindwa kusimamia uingizwaji wa simu feki na refurbished. Simu feki zimejaa mitaani, copy original mfano; techno, Itel, ambazo ni feature phone, ndizo feki zilizojaa sana kwani muundo wa chip zinazotumika kwenye mother board ni rahisi sana hivyo viwanda feki vinachukua sample ya tecno, itel na kuziduplicate sana. IMEI kwao sio issue kuitengeneza kwa sababu kuna kikokotoo ambacho utumia tangia wanapopata simu ya kwanza wanaingiza IMEI moja inazalisha nyingine, kwenye mtambo wa simu/ TCRA inaonekana ni genuine phone.

Hata hizi simu feki android wanafanya hivyo. TCRA wameruhusu simu nyingi za iPhone zilizoisha muda wake kuuzwa nchini kama simu mpya. Simu hizi zimejaa makumbusho na kinondoni na kariakoo.

Jinsi ya kuzitambua. Chukua IMEI yake nenda kwenye site. Www.iunlocker.net itakuja page inakwambia weka IMEI itakupa full info. Ukikuta warranty expired hiyo ni used au refurbished. Ukienda kwa mafundi, utakuta kesi nyingi simu za iPhone zimezima, huko ndani ya simu vichesho , simu zimeoza. TCRA msiwe wachoyo tafteni mafundi wabobezi mliowaingineer wasome muwajiri kwa kazi ya kutambua vitu feki nyie peke yenu hamuwezi kujua kwa kuwa sekta hiyo bado wachanga.

TRA; imefeli vibaya sana kushindwa kufanya ukaguzi wa mizigo inayopitishwa viwanja vya ndege, meli hivi, Mzigo unapoingia una register yake, simu feki zinapita wapi ? Simu feki uingizwa kwa njia ya maji kupitia bandari bubu. Jinsi ya kuwqkamata walaghai waliojificha. Nenda posta mpya maeneo ya IPS building, Benk ya Posta mtaa wa azikiwe, utakuta aina kumi za simu zinauzwa kama original na vijana wanaojua machimbo kwa wahuni wa kichina na watanzania. Tumia njia zenu za ushushu mtajua wanaozileta mtaokoa pesa za kitanzania kwa simu zinazoingizwa nchini bila ushuru.

Kwa upande wa kujua spea feki, katika kundi lenu tafta wataalum waliosoma masomo ya simu kupitia DIT na VETA watawasaidia kujua spea feki kwani wao ni wabobezi na wanazitambua.
 
Hizi ofisi zenyewe watendaji wengi wao mambo ya kamlete unafikir watalamu wanatoka wapi mara kamlete mtoto wa mjomba, kibongobongo bado sana.
 
Back
Top Bottom