Tajiri Kichwa
JF-Expert Member
- Apr 2, 2017
- 9,020
- 22,093
Mitumba ukienda Karume unapata kwa bei nzuri haizidi 10000
Kama utaki kwenda karume unakuwa na watu wako ..ikitoka kitu kizuri anakuletea wewe kwanza
Mitumba ukienda Karume unapata kwa bei nzuri haizidi 10000
Hapa kufua kwa petroli naomba nifafanulie zaidi, ufuaji kipimo.TBS hii haikagui ubora inakagua muonekano yaani kama ni shati liwe na sehemu ya kuingiza mikono na kichwa. Nakushauri ukinunua vaa tu bila kufua au fua kwa petroli itabaki na ubora wake.
mitumba ndio balaa kabisa unaikuta ingangaa kweli kweli lakini ukifua mara moja tuu kwisha habari yake. Zingine ukifua mara mbili zinachanika sijui zinakua zimeoza ama yale madawa wanayoweka kuzihifadhi ndio yanazichakaza?Kuepukana na hiyo adha kanunue mtumba au nenda kwenye maduka wanayouza nguo og
Kwa kweli Japo kuna mitumba inadumu sana...mitumba ndio balaa kabisa unaikuta ingangaa kweli kweli lakini ukifua mara moja tuu kwisha habari yake. Zingine ukifua mara mbili zinachanika sijui zinakua zimeoza ama yale madawa wanayoweka kuzihifadhi ndio yanazichakaza?
Hali imebadilika zama hizi mkuu. Magaka yametapakaa kuanzia uswazi mpaka kwa washua. Mchina si wa mchezo mchezoMara nyingi bei ya kitu huendana na ubora wake, usitegemee shati ya 2500 ifanane na ya 25000.
Halafu Mtanzania ukimwambia hili shati bei yake 25000 kulingana na ubora wake atakwambia mbona kariakoo yapo mengi tu 2500 hajui kama ni kopi ya mwisho ya mchina.
Yote kwa yote umasikini wetu ndio chanjo, mahitaji mengi kuliko kipato.
Sie wavaa mitumba ya bei ghali mbona tunapeta tu.... Nguo zimesimama quality mpaka muonekano, na unaweza kuifua mwaka mzima bila matatizo yoyote...
[emoji23][emoji23][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Kuna siku nilijipinda nikanunua viatu kwenye yale maduka ya mtaa wa kongo, baada ya mwezi nilitukana kinoma.
Kiatu unavaa hadi unasikia unyayo unauma kabisa.
Kuna haja ya tbs kuangalia hili.
Nadhani tatizo linaweza kuwa pande zote. Kwa upande wa wanunuzi wanapaswa kuangalia specifications na instruction za nguo, kuna nguo ambazo zinahitaji zifuliwe kwa machine, na zingine ni dry cleaning tu. Sasa nguo inayohitaji dry cleaning ukiifua kwa maji hata uinyoonshe vipi haitokaa sawa. Na hata nguo za kufua kwa nachine pia zina specification za maji unakuta umeambiwa ufue kwa maji baridi tu au moto tu au vuguvugu, sisi tunafua tunavyojua sisi, haiwezi kuwa sawa. Kuna nguo hazi nyooshwi kwa pasi zinanyooshwa kwa mfuke wa moto, sisi tunanyoosha.
Jingine ni maji yetu, huko zitokako maji yana kuwa treated kupunguza mineral contents, hapa kwetu hilo halifanyiki, na kuna wengine hutumia maji ya visima au yakuvuna ya mvua, yoote haya yana athari zake kwenye fabrics.
Sabuni, kuna za unga, vipande, na za maji. Hapa kwetu sabuni nyingi ni kali sana, kwasababu nahisi maji yetu ni hard water na sio soft water hivyo watengenezaji wa sabuni kwa kuzingatia hilo huziongezea kemikali na kuzifanya kali sana, sasa na ufuaji wetu mtu analoweka nguo 24hrs kwenye sabuni kali, anategemea fabrics za hiyo nguo ziwe sawa, hapana.
Huko wanakozitengeneza, hawalengi soko la Afrika, ila kwasababu za kibiashara wanaleta tu au kuchepusha na hapo ndio sisi tusio treat maji, na kutumia sabuni kiasi maalumu na kwa muda maalumu, na tusio tumia washing machines na kupikicha yanatukuta yote haya.
Na nguo zinazofuliwa kwa dry cleaning sisi tuna fua kwa maji tena mtu anailoweka 24hrs, kwanza haihitaji maji kabisa, lakini umeifua, mbaya zaidi umeiloweka 24 hrs huwezi kutegemea iwe au irudie ubora wake.
Hivyo tujifunze kuangalia label zinasemaje kabla ya kununua, na kama hukuangalia label basi angalia kabla ya kuifua, unaweza kuta haifuliwi ni dry cleaning fabrics, na unapo nyoosha angalia label, inahitaji dry heat, au mvuke, ukifuata masharti ya manufacturer hutojuta, na huto lalamika. Sisi tunajisahau, au hatujali kabisa manufacturer instructions, sio nguo tu, hili liko kwenye vitu vyote. Tukijifunza kutafiti na kuangalia mahitaji ya kitu, kwa case hii nguo, na kujali hatuta juta, lakini ukiangalia mahitaji yako tu bila kujali mahitaji ya nguo uliyoinunua bei ghali hutoisha kulalamika kila siku.
Hata mitumba inazo instructions of care, tuwe waangalifu tusijiumize ki uchumi.
Waswahili tunasrma, " cheap is expensive" hahaha, any way mmeelewa nadhani.
Kila la kheri.
huwa napenda sana kujiburudisha kwa kusikiliza mziki.
katika bidhaa ambayo wachina wamekuwa wananitesa ni earphones.
honestly sijawahi kununua earphone ya kichina halafu nikakaa nayo mwezi mmoja au zaidi bila kuharibika.
asilimia 98 ya bidhaa za earphone za kichina zinazoingizwa nchini zina ubora duni mno.
huwa kila mara nalizimika kununua earphone mpya. tbs mpo wapi?
hata Mtumba una grades pia, ukipata Ile grade ya 1 ndo mkataba kabisa....mitumba ndio balaa kabisa unaikuta ingangaa kweli kweli lakini ukifua mara moja tuu kwisha habari yake. Zingine ukifua mara mbili zinachanika sijui zinakua zimeoza ama yale madawa wanayoweka kuzihifadhi ndio yanazichakaza?
machimbo yapo kila mkoa Brother, mfano nilikua daslam mwaka juzi nilipita sehemu moja hivi jirani na TBL pale, nliona trousers Kali sana za Mtumba aina ya Dickies, ukiwa Mwanza unasogea pale Lango Lango wanaita, Moshi tuko na Maimoria(Memorial), Yani kiufupi kila mji wako watu ambao wanakua na frame za kuuza iwe ni mashati, suruali, sandals mpaka viatu vya Mtumba ambavyo ni quality mara mia ya vinavyoitwa Vipya vya madukani...😁😁Tupeane machaka mazuri bouy nami nafeel sana mtumba aisee bouy
Nunua headphone brand ya Xiaomi mkuu usahau kero na shida zote pitia uzi wangu hapo jukwaa la sayansi na teknolojia ili ujionee utofauti na maajabu https://www.jamiiforums.com/threads...omi-tukutane-hapa-ili-kupeana-ujanja.1331956/
Hahaha hili la kutafuta picha nizielezee naomba niseme, sita liweza ndugu, kama unaweza saidia.Mkuu asante kwa maelezo yako mazuri .Naomba tuanze basi kupeana uzoefu au ujuzi kwa faida za watu wengi pia mfano nguo ukikuta imeandikwaje ndio inakua inahitaji nini?
Namaanisha pengine lugha ikawa changamoto .Naomba utuwekee zile rebo na ufafanuzi wake kwa lugha yetu pendwa itasaidia sana ila binafsi yangu dukani siendi tena
Hahaha hili la kutafuta picha nizielezee naomba niseme, sita liweza ndugu, kama unaweza saidia.