TBS hizi nguo za kichina mnaziona?

TBS hizi nguo za kichina mnaziona?

Ndiyo maana mimi nikitaka kununua pamba nakwea pipa kwenda majuu kwa trump, hii ndoto nimeiota leo mchana
 
Ntatoa mfano mzuri Sana wa jersey Kuna authentic na replica. replica inauzwa £65 lakini authentic inauzwa £95 ukiangalia quality ya hizi jersey 2 tofauti nakwambia hivi hutaweza kutofautisha japo ipo namba moja na namba mbili.

Tanzania tunauziwa sio namba mbili Bali totally fake ndio sababu kwetu imekua Kama dumple la bizaa fake. Yani Kuna vitu inakera kwa kweli
Lakini sidhani hata huko nje ulaya kila mtu anaafford kununua t-shirt ya £60,lakini bado wanavaa nguo nzuri zenye quality..sisi tunakwama wapi??

Ni lazima tukubali hawa wachina wanatuletea vitu vya hovyo sana kwenye nguo..
 
Unanunua dukani nguo nzuri kwelikweli inang'aa machoni.

Lakini cha ajabu ukiifua mara moja au mbili tu haitazamiki tena ni kama ulikuwa unanyang'anyana na ngombe.

Wataalam wetu TBS Pale bandarii huwa mnakagua nini?

Haya manguo hamyaoni au hamhusiki na ukaguzi wake?

Mtusaidie tunaibiwa.

Ni kwel ila TBS wakisema wakaze kko utoona mfanyabiashara mtaji utakua umekata kwa hasara na watashindwa kuchukua nguo za bei juu na watakaochukua ujue sio wote watakao kuwa na uwezo wa kununua izo nguo wafanyabiashara mitaji yao midg walio wengi pia ukichukua nguo zote za gharama ujue wachache wataweza kununua sasa wenye kutaka nguo OG ukienda kinondoni kwakina zizzou fashion nguo unashika ununui unaondoka na kwenda kko ubora wa nguo unatofautiana jmn na kuangalia pia na vipato vya watu hata uingereza mbona zipo nguo za kawaida tu na bei nafuu lkn yapo maduka kwa ajili ya kina beckham
 
Lakini sidhani hata huko nje ulaya kila mtu anaafford kununua t-shirt ya £60,lakini bado wanavaa nguo nzuri zenye quality..sisi tunakwama wapi??

Ni lazima tukubali hawa wachina wanatuletea vitu vya hovyo sana kwenye nguo..
mkuu juko nje zipo tshr za 20 000 kibao tena nchu za mgahatibi za high quality hawa wafanyabiashara wetu wanaenda kununua nguo za plastic (nylon na polyster)za dolar 1 wanatyletea huku!
 
Tbs ni shirika la hovyo sana vitu vingi sana vinavyouzwa hapa nchini havina ubora lakini tbs wapo na wanalipwa mishahara kila mwezi
Kuanzia nguo, redio, tv, viatu, mpaka dawa za meno tena hizi wanauza mpaka kwenye mabasi ya mkoani

walicho kosea TBS kupewa mamlaka ya kila idara ikague vitu ndio maana wenzetu utakuta idara fulani ina jitegemea kupitia sehemu fulani na ukaguzi wake si mchezo
 
Mnauziwa kulingana na uwezo wa soko. Mfano dukani kuwe na Levi's jeans OG bei £60 au Lacoste t-shirt £65 au Tims £160 wangapi wataweza kununua kiasi cha duka ku-sustain biashara? Hizo za Kariakoo ndio size za majority na kibiashara ndio zinafaa. Nunua nyingi fua mara moja kwa mwezi zitamudu ila ukitaka kufua kila wiki hamna rangi utaacha ona


Ni kweli mkuu.Lakini, kuna haya maduka makubwa kwenye hizi malls zetu tulitegemea sasa kwa bei zao ziendane na kanuni hii unayoisema, cha ajabu nguo zao nyingi unapigwa bei na bado ni duni.Ninachofahamu, suruali inayoanzia 100,000/= inapaswa kuwa na ubora fulani hivi.Lakini, hali haipo hivyo.

Ninadhani wajasiriamali hawa wamepata mwanya wa kutuibia.Ukizingatia nchi yetu wateja wengi tuwajinga, si wadadisi na pia si watata.Ukichanganya na serikali kulala, kukosa teknolojia , wahusika kuwa wavivu kufanya kazi yao na ukosefu wa uzalendo ndo tunamalizwa kabisa.
 
TBS hii haikagui ubora inakagua muonekano yaani kama ni shati liwe na sehemu ya kuingiza mikono na kichwa. Nakushauri ukinunua vaa tu bila kufua au fua kwa petroli itabaki na ubora wake.

"fua kwa petroli " hahahahah aisee nyie watu mnataka ajali ya moro ihamie gheto kwake, ngoja afikiche nguo cheche ziruke.
 
Mara nyingi bei ya kitu huendana na ubora wake, usitegemee shati ya 2500 ifanane na ya 25000.

Halafu Mtanzania ukimwambia hili shati bei yake 25000 kulingana na ubora wake atakwambia mbona kariakoo yapo mengi tu 2500 hajui kama ni kopi ya mwisho ya mchina.

Yote kwa yote umasikini wetu ndio chanjo, mahitaji mengi kuliko kipato.
Unaweza kununua iyo shati ya 250000 mliman city, then ukaenda kariakoo ukaikuta kwa 20,000.
 
Unaweza kununua iyo shati ya 250000 mliman city, then ukaenda kariakoo ukaikuta kwa 20,000.
Kweli kabisa mkuu.Viatu wanavyolipia laki na nusu kwenda juu,k/koo tunanunua kwa elfu 50 mpaka 70.Hili neno "ORIGINAL" ni fursa kwa baadhi ha wafanyabiashara[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Mm naingia mrp na redtag kununua zile nguo zilizokuwa kwny sale. Umaweza kuingia na elf 60 ukapata nguo hata 5. Tena kwa nguo za kike ndio zinashuka bei hata elf 8 wanapata.
 
Siku niliyosikia mahubiri kuwa kuvaa mtumba ni laana, niliacha kabisa kununua mtumba. Navaa hizi za dukani, ila changamoto ninayoipata ni mateso kwa kweli. Kuna siku nguo ni mpyaaa kabisa nikaamua kufua... uwiii ... rangi yoote ilitoka ikakojoleana ikawa kama batiki la marangirangi.... hovyo kabisaaa nguo za kichina
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom