TBS hizi nguo za kichina mnaziona?

TBS hizi nguo za kichina mnaziona?

Basi weka ata maelezo ya bila picha kua ukikuta hivi fanya hivi
Nadhani mchango wangu kwenye uzi huu utawasaidia watakao jali, ni mchango wa jumla, alama ziko nyingi sana, ndio maana nikaomba wewe usaidie ku google images na uzipandishe hapa, watu watachangia tu, nami nikipata taarifa au nikiuona nitajaribu pia. Tusaidie kama unaweza.
 
Kodi kwenye mitumba inavyozidi kuwa kubwa na wafanyabiashara ndio wanaagiza ronya ronya zaidi.
Kwaiyo mnaadhibu wateja wenu kwa kuwa mmeongezewa kodi au sijakuelewa kiongozi?
 
Hili tatizo TBS hawawezi kukwepa, na shida ni kwamba, mizigo inaingia nchini kwa idadi kubwa sana na kila aina. Kudhibiti yote inakuwa ngumu. Na ndipo wafanyabiashara wanapata gepu la kupigia, kwa kutoa sampuli kidogo ya kwenda kukaguliwa ambayo mara nyingi inakua ni og, tofauti na mzigo wanaopitisha kuingiza sokoni.
Kama wanaletewa sampo tu na wao wanaridhika basi kuna shida kubwa. Hao tbs inabidi wajiongeze kwa msako wa kushtukiza hata kama ni mara moja moja
 
Hapa issue ni weledi wa TBS katika kudhibiti viwango vya ubora wa bidhaa na sio kuoneshana ujuaji wa nani ananunua maduka yapi. Naona kuna wenzutu wametufikisha hadi kwenye tshirt ya £60 ambazo ni sawa na Tshs 166,000. Huu mi nauitaga umaarufu kunuka...

TBS wana dhamana ya kudhibiti ubora wa bidhaa, haijalishi hiyo bidhaa ina thamani gani. Masoko yote, yawe ya kwetu ya Mtaa wa Congo au ya kwenu nyie mnaonunua tshirt kwa £60 yanapaswa kulindwa na mamlaka yasivamiwe na bidhaa zisizokidhi viwango
 
Asante mkuu
Nadhani mchango wangu kwenye uzi huu utawasaidia wanatakao jali, ni mchango wa jumla, alam ziko nyingi sana, ndio maana nikaomba wewe usaidie ku google images na uzipandishe hapa, watu watachangia tu, nami nikipata taarifa au nikiuona nitajaribu pia. Tusaidie kama unaweza.
 
Unanunua dukani nguo nzuri kwelikweli inang'aa machoni.

Lakini cha ajabu ukiifua mara moja au mbili tu haitazamiki tena ni kama ulikuwa unanyang'anyana na ngombe.

Wataalam wetu TBS Pale bandarii huwa mnakagua nini?

Haya manguo hamyaoni au hamhusiki na ukaguzi wake?

Mtusaidie tunaibiwa.
Kuna nguo nyingine ukinunua unavaa bira kufua hata miezi 2 siku ukifua ndo kwisha habari yake
 
Mara nyingi bei ya kitu huendana na ubora wake, usitegemee shati ya 2500 ifanane na ya 25000.

Halafu Mtanzania ukimwambia hili shati bei yake 25000 kulingana na ubora wake atakwambia mbona kariakoo yapo mengi tu 2500 hajui kama ni kopi ya mwisho ya mchina.

Yote kwa yote umasikini wetu ndio chanjo, mahitaji mengi kuliko kipato.

Unfortunately Tanzania haiko hivyo ndugu.
 
Mnauziwa kulingana na uwezo wa soko. Mfano dukani kuwe na Levi's jeans OG bei £60 au Lacoste t-shirt £65 au Tims £160 wangapi wataweza kununua kiasi cha duka ku-sustain biashara? Hizo za Kariakoo ndio size za majority na kibiashara ndio zinafaa. Nunua nyingi fua mara moja kwa mwezi zitamudu ila ukitaka kufua kila wiki hamna rangi utaacha ona

Ulichosema ni kweli Rondo, lakini si lazima tununue designer’s stuff ndipo tupate vitu quality, ukishuka hapo tu bondeni kwa mzee madiba ukaingia mall hata stores zisizokuwa na majina utanunua nguo kwa bei ya kawaida kabisa mfano 30-80k ila quality yake ni superb. Sasa nenda stores za hapa kwetu hata zenye majina uone kichekesho chake, nguo unanunua kwa 50-100k ila ukifua unaona inavyochujuka hadi huruma. Maduka yote sinza kino etc bado tu kuna vihoja sijui tunakosea wapi sisi, na si tu kwa wanaofunga mzigo china, hata wanaotoa mzigo turkey bado hakuna kinachoridhisha, kwani hawawezi kuleta nguo za quality bora kwa bei ya kawaida kwa ajili ya watu wa middle income? Hii inatulazimisha mtu kumiliki mirundikano ya nguo utadhani una mnada 😂 wakati ungeweza kuwa na nguo 20 tu na ukapeta.

Hii changamoto huwa inanipa kufikiria labda kuna gharama kubwa sana za uendeshaji wa hizo biashara, zikiwemo kodi za mapango, TRA, Usafirishaji etc, hivyo wananunua nguo kwa dola 5 wanakuja kutuuzia mibei ya ajabu?
 
Munanunua nguo za bei cheap saana mimi sivai mtumba but nguo zangu azichuji na azizeeki haraka na ndio maana sipatani na mtumba labuda gari na baada ya mda kidogo tu ata gari ya mtumba pia sito itaka .

Una shop wapi mwenzetu? Tupeane siri ya mafanikio.
 
Niseme tu ukweli, TBS ni chaka la wala rushwa, kuna vitu vingi feki toka China, tena vinauzwa bei mbaya kuliko hata original vinaingia humu nchini, sasa sijui kazi yao ni nini..
 
Aiseee umeleta mada nzuri sn. Mimi kusema ukweli sipendi kuvaa nguo za mtumba. Lakini kila nikijaribu kununua hizi nguo za dukani hasa mashati na baadhi ya majinzi cha moto huwa nakipata. Nikifua nguo kwishaa habari yake. Inatoa rangi za kufa mtu aaafu inakunjamana hata uinyoooshe vp hainyoosheki.Aafu zinauzwa bei kubwa sn ubora sifuri.TBS kazi yenu ni nini?
Ndio maana tunakimbilia mitumba, nguo mpya za China ni bei mbaya sana madukani, ila ukifua mara moja tu, haina kazi tena..
 
Nadhani tatizo linaweza kuwa pande zote. Kwa upande wa wanunuzi wanapaswa kuangalia specifications na instruction za nguo, kuna nguo ambazo zinahitaji zifuliwe kwa machine, na zingine ni dry cleaning tu. Sasa nguo inayohitaji dry cleaning ukiifua kwa maji hata uinyoonshe vipi haitokaa sawa. Na hata nguo za kufua kwa machine pia zina specification za maji unakuta umeambiwa ufue kwa maji baridi tu au moto tu au vuguvugu, sisi tunafua tunavyojua sisi, haiwezi kuwa sawa. Kuna nguo hazi nyooshwi kwa pasi zinanyooshwa kwa mfuke wa moto, sisi tunanyoosha.
Jingine ni maji yetu, huko zitokako maji yana kuwa treated kupunguza mineral contents, hapa kwetu hilo halifanyiki, na kuna wengine hutumia maji ya visima au yakuvuna ya mvua, yoote haya yana athari zake kwenye fabrics.
Sabuni, kuna za unga, vipande, na za maji. Hapa kwetu sabuni nyingi ni kali sana, kwasababu nahisi maji yetu ni hard water na sio soft water hivyo watengenezaji wa sabuni kwa kuzingatia hilo huziongezea kemikali na kuzifanya kali sana, sasa na ufuaji wetu mtu analoweka nguo 24hrs kwenye sabuni kali, anategemea fabrics za hiyo nguo ziwe sawa, hapana.
Huko wanakozitengeneza, hawalengi soko la Afrika, ila kwasababu za kibiashara wanaleta tu au kuchepusha na hapo ndio sisi tusio treat maji, na kutumia sabuni kiasi maalumu na kwa muda maalumu, na tusio tumia washing machines na kupikicha yanatukuta yote haya.
Na nguo zinazofuliwa kwa dry cleaning sisi tuna fua kwa maji tena mtu anailoweka 24hrs, kwanza haihitaji maji kabisa, lakini umeifua, mbaya zaidi umeiloweka 24 hrs huwezi kutegemea iwe au irudie ubora wake.
Hivyo tujifunze kuangalia label zinasemaje kabla ya kununua, na kama hukuangalia label basi angalia kabla ya kuifua, unaweza kuta haifuliwi ni dry cleaning fabrics, na unapo nyoosha angalia label, inahitaji dry heat, au mvuke, ukifuata masharti ya manufacturer hutojuta, na huto lalamika. Sisi tunajisahau, au hatujali kabisa manufacturer instructions, sio nguo tu, hili liko kwenye vitu vyote. Tukijifunza kutafiti na kuangalia mahitaji ya kitu, kwa case hii nguo, na kujali hatuta juta, lakini ukiangalia mahitaji yako tu bila kujali mahitaji ya nguo uliyoinunua bei ghali hutoisha kulalamika kila siku.
Hata mitumba inazo instructions of care, tuwe waangalifu tusijiumize ki uchumi.
Waswahili tunasema, " cheap is expensive" hahaha, any way mmeelewa nadhani.
Kila la kheri.
Aiseee mzeee umeongea nondo sana hapa!!!!!!!!!!!
 
Unanunua dukani nguo nzuri kwelikweli inang'aa machoni.

Lakini cha ajabu ukiifua mara moja au mbili tu haitazamiki tena ni kama ulikuwa unanyang'anyana na ngombe.

Wataalam wetu TBS Pale bandarii huwa mnakagua nini?

Haya manguo hamyaoni au hamhusiki na ukaguzi wake?

Mtusaidie tunaibiwa.
Unafua wewe au Shemeji?
 
Tatizo la nguo kuchuja na kupauka lilinitesa sana,hususan mimi mpenzi wa cadet na jinsi.Katika kutafuta suluhisho,ikanijia akili ya kusoma label zile ndani ya nguo.Hapo ndo tongotongo likanitoka!!!!!!!!!!!

Mara yako ya mwisho kufuata maelezo ya jinsi ya kuifua/kuitunza nguo ni lini?
5c11fbeffe56dc7e6463b06a262fac3a.jpeg
Clothing-symbol-chart.jpeg
Wash-Care-Symbol-Tips.jpeg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom