TBS hizi nguo za kichina mnaziona?

TBS hizi nguo za kichina mnaziona?

Mnauziwa kulingana na uwezo wa soko. Mfano dukani kuwe na Levi's jeans OG bei £60 au Lacoste t-shirt £65 au Tims £160 wangapi wataweza kununua kiasi cha duka ku-sustain biashara? Hizo za Kariakoo ndio size za majority na kibiashara ndio zinafaa. Nunua nyingi fua mara moja kwa mwezi zitamudu ila ukitaka kufua kila wiki hamna rangi utaacha ona

We jamaa unaongea kulingana na top luxiury za ulaya
Ila ata uko jeans nyingi ni za 15 to 30$, na za 30$ ni top quality, kutokana na unaponunua
Ko uko na uku bei sio tofauti kivile
Na miaka ya zaman kariakoo kulikuwa na nguo bei hyohyo zinazodumu sana,
Kikubwa ni wanajua uku hatufatilii na ndo pakupiga biashara kwa kuleta visivyodum ili suply isishuke
 
Tatizo nafikiri ni material wanazo tengenezea nguo ..mfano shati nyingi za maduka ya congo kariakoo inavutia ikiwa dukani jaribu kuivaa na kufua ndio utajua shida iko wapi

Niliwai kwenda kariakoo naambiwa jezi original 35,000 ilikuwa inashangaza sana maana jezi adidas wanauza 180,000 apo lazima upate wasiwasi

Na ata aya maduka ya mlimani city red tag,gsm,Woolworth nako quality sio zile za nguo zenyewe at least streetsoul

Sometimes nguo za mtumba grade 1 zile ni nzuri ila upate muuzaji mzuri ambaye uta afford bei yake ..maana unaweza letewa shati ukaambiwa 30,000 mwisho wa siku unadai ngoja niende kariakoo

Kikubwa bongo kimavazi bado tuendelee kuchanga changa ivyo ivyo ,maana tunavaa kulingana na kipato chetu
 
Hahaha hivyo tatizo sio nguo ni nguo zinazouzwa kariakoo?! Label zipo, I bet hata nguo uliyovaa ina label, ila ni kitu sisi hatukijali kabisa tuna angalia kila kitu lakini siyo label, kwasababu ni kadogo sana au hatujui umuhimu wake, halafu tunalalamika.
Ni nguo za kariakoo tu, vipi za Mwenge, Ubungo, Tegeta, au Tazara?!
Hahaha sisi hatuishiwi malakamiko hata kwa matatizo yetu wenyewe.
Sijui umeamua kubishana au? Unafikiri watu wakisema nguo za Kariakoo wana maana gani? Nguo niliovaa yes ina label, ila sio ya Kariakoo,Mwenge,Tegeta au Mlimani city.
 
We jamaa unaongea kulingana na top luxiury za ulaya
Ila ata uko jeans nyingi ni za 15 to 30$, na za 30$ ni top quality, kutokana na unaponunua
Ko uko na uku bei sio tofauti kivile
Na miaka ya zaman kariakoo kulikuwa na nguo bei hyohyo zinazodumu sana,
Kikubwa ni wanajua uku hatufatilii na ndo pakupiga biashara kwa kuleta visivyodum ili suply isishuke
Soma posts zingine. Nimesema tena hata nguo za Ulaya za £10/15/20 ni nzuri kuliko za 50,000-100,000 za kariakoo
 
Hahaha hatupigwi, hatufuati maelekezo ya jinsi ya ku care hizi nguo. Tatizo siyo bei, tatizo ni kukosa tools, au maarifa ya ku care nguo hizi. Hatuna washing machines, hatufuati kiasi cha sabuni, aina ya sabuni, hatuangalii contents.
Nguo inahitaji dry cleaning tunafua tena tuna pikicha. Nguo inahitaji maji vuguvugu tunatumia baridi, nguo isiyo nyooshwa tunanyoosha.
Lazima tuwalaumu wachina na wazungu, kwa sababu hatufuati maelekezo.

Kwahyo hii inaapply kwenye nguo za sikuizi tu???
Hizi ni minor cases zisizo na mashiko
 
Sasa wachina hawana shida ila ni wanunuaji unaenda dukani unanunua vitu ovyo vinang'aa hadi uonekani.
Hivyo huwa havidumu halafu ni low grade ila ukinunua tshirts shirts na trousers ndio ambazo hazing'ai aifubai tatizo dukani huwezi nunua vitu vyote og inabidi zichanganywe.
Lasivyo huwezi nunua mzigo kabisa dah kazi ipo kwenu kuna wale waliwao ambao ndio nyie hamtuli katika uchaguzi.
 
Sijui umeamua kubishana au? Unafikiri watu wakisema nguo za Kariakoo wana maana gani? Nguo niliovaa yes ina label, ila sio ya Kariakoo,Mwenge,Tegeta au Mlimani city.
Labda nieleweshe, naweza kuwa nimejibu sivyo. Nisamehe "Nguo za kariakoo" wana maanisha nini?!
 
Nguo ni moja ya bidhaa lakini zipo bidhaa nyingi mtaani hazina ubora kabisa mpaka unajiuliza hivi TBS inafanya kazi gani mbali na kupokea mishahara na kubandika sticker zao?
 
Niliacha kuvaa nguo za dukank kwa sababu kama hizo
 
Unanunua nguo miez 2 tu zmepauka,, hili n tatizo kubwa saana
 
Nguo zinazoletwa na wajanja from China. Na wasichokijua wengi huko Mwenge wanachukua Kariakoo halafu wanwapiga bei mara mbili ya Kariakoo. Nguo nyingi za kwenye maduka hapa Dar na mikoani zinanuliwa Kariakoo
Huwa na vaa mitumba, ninapoukuta mtumba nikapendezwa nao, nikiwa na pesa nanunua.
Labda hapo ndio tatizo langu.
 
Nguo ni moja ya bidhaa lakini zipo bidhaa nyingi mtaani hazina ubora kabisa mpaka unajiuliza hivi TBS inafanya kazi gani mbali na kupokea mishahara na kubandika sticker zao?
Hili na kubali, kwa wafanyabiashara kwao ni easy money.
Lakini na sisi tunawezaje kukagua quality ya vitu hata technologia ya kuvitengeneza hatuna na taaluma yake hatuna?!
Hatujui contents zinazohitajika kutengeneza rangi ya nyumba kwa mfano, sasa tunajuaje/tunawezaje kupima ubora wake?!
Mfano tukague gari, kwa specifications zipi?!
 
Umemaliza kabisa kamanda nadhani mada ifungwe[emoji358]
Mara nyingi bei ya kitu huendana na ubora wake, usitegemee shati ya 2500 ifanane na ya 25000.

Halafu Mtanzania ukimwambia hili shati bei yake 25000 kulingana na ubora wake atakwambia mbona kariakoo yapo mengi tu 2500 hajui kama ni kopi ya mwisho ya mchina.

Yote kwa yote umasikini wetu ndio chanjo, mahitaji mengi kuliko kipato.
 
Jana nilikutana na Mshikaji wangu analalamikia zile nguo za vunja bei .. Nimeshangaa Leo nakutana na huu Uzi , asije kuwa ni yeye[emoji1] [emoji1] ...


Poleni jamani karibuni mitumbani.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom