TBS hizi nguo za kichina mnaziona?

TBS hizi nguo za kichina mnaziona?

Vitu kama hivyo vinaingiziwa kwa magendo... zinapelekwa sample quality kwa ajili ya ukaguzi... mzigo ukipita zilizobaki zote low quality...

Kuna mambo yanasikitisha sana...


Cc: mahondaw
 
unataka TBS wawe wanazifua kwanza ili wajue kuwa hazichuji?
watafua nguo ngapi?
 
Hili tatizo TBS hawawezi kukwepa, na shida ni kwamba, mizigo inaingia nchini kwa idadi kubwa sana na kila aina. Kudhibiti yote inakuwa ngumu. Na ndipo wafanyabiashara wanapata gepu la kupigia, kwa kutoa sampuli kidogo ya kwenda kukaguliwa ambayo mara nyingi inakua ni og, tofauti na mzigo wanaopitisha kuingiza sokoni.
 
Acha kuongea ww, ata ayo ya 25k matatizo yake ni yaleyale
Infact mashati mengi congo ni 18 mpaka 27k
Apo ni kuibiwa tu otherwise uwe mtaalam sana
Mengi mazuri ni ya ovyo ukikaa nayo mwezi
Nipo kwenye sekta hii kitambo naongea kulingana na uzoefu wangu.

Na hii sio kwenye nguo tu hadi kwenye vifaa vya kielektroniki ni hivyo hivyo.
 
Unanunua dukani nguo nzuri kwelikweli inang'aa machoni.

Lakini cha ajabu ukiifua mara moja au mbili tu haitazamiki tena ni kama ulikuwa unanyang'anyana na ngombe.

Wataalam wetu TBS Pale bandarii huwa mnakagua nini?

Haya manguo hamyaoni au hamhusiki na ukaguzi wake?

Mtusaidie tunaibiwa.
Hapa bana pagumu sana kwa kweli. Sababu kuna nguo zingine zinauzwa zikiwa zimeshanika au kupauka kabisa na watu still wanazinunua.
 
huwa napenda sana kujiburudisha kwa kusikiliza mziki.

katika bidhaa ambayo wachina wamekuwa wananitesa ni earphones.

honestly sijawahi kununua earphone ya kichina halafu nikakaa nayo mwezi mmoja au zaidi bila kuharibika.

asilimia 98 ya bidhaa za earphone za kichina zinazoingizwa nchini zina ubora duni mno.

huwa kila mara nalizimika kununua earphone mpya. tbs mpo wapi?
 
Kweli kabisa. Mimi nimeachana na hizo special za kizushi nagonga used.Sema Tz tunakosea,tumediscourage mitumba kwa kuweka kodi kubwa, wenzetu Kenya biashara imeshamiri balaa.Sasa hivi vitu vikali vinatoka NBI, bei zake ni moto.
Kodi kwenye mitumba inavyozidi kuwa kubwa na wafanyabiashara ndio wanaagiza ronya ronya zaidi.
 
Mitumba ukienda Karume unapata kwa bei nzuri haizidi 10000
Tatizo nafikiri ni material wanazo tengenezea nguo ..mfano shati nyingi za maduka ya congo kariakoo inavutia ikiwa dukani jaribu kuivaa na kufua ndio utajua shida iko wapi

Niliwai kwenda kariakoo naambiwa jezi original 35,000 ilikuwa inashangaza sana maana jezi adidas wanauza 180,000 apo lazima upate wasiwasi

Na ata aya maduka ya mlimani city red tag,gsm,Woolworth nako quality sio zile za nguo zenyewe at least streetsoul

Sometimes nguo za mtumba grade 1 zile ni nzuri ila upate muuzaji mzuri ambaye uta afford bei yake ..maana unaweza letewa shati ukaambiwa 30,000 mwisho wa siku unadai ngoja niende kariakoo

Kikubwa bongo kimavazi bado tuendelee kuchanga changa ivyo ivyo ,maana tunavaa kulingana na kipato chetu
 
Mi nimehamia huko maana hizi za dukani hatari sana.
Kuna siku nimenunua splash cardet 70K nikaifua ikapauka nikasema sinunui tena
Mtumbani ukienda 70K unapata nguo 7 Grade 1
Mitumba mingi inatoka US na Europe ni nguo za kiwango cha juu. Ukipata grade 1 kama mpya
 
Mi nimehamia huko maana hizi za dukani hatari sana.
Kuna siku nimenunua splash cardet 70K nikaifua ikapauka nikasema sinunui tena
Mtumbani ukienda 70K unapata nguo 7 Grade 1
Na wauzaji washawajulia Wabongo. Wanajua wakiweka bei juu mtaani ni OG
 
Kuepukana na hiyo adha kanunue mtumba au nenda kwenye maduka wanayouza nguo og
dada
maduka ya kawaida yanayouza nguo OG kwa bongo ni machache sana, na ukizipata ni ghali kwa mtu mwenye kipato cha kati/chini.

nguo nyingi mpya za madukani ni "midosho" inayotengenezwa china. baadhi ya wabongo wanaomiliki maduka maeneo ya kinondoni wanaziingiza ili kuwapiga wabongo wenzao.

kwa mfano ili kupata OG polo t-shirt au OG lacoste sneakers inabidi uende kwenye maduka makubwa yanayopatikana ndani ya malls.

na hapo budget yako inabidi iwe vizuri. la sivyo utaishia tu kufanya window shopping na kugeuza.
 
Tatizo watu mnapenda manguo yanayong'aa kimuonekano kama kiatu kilichotoka kupigwa kiwi..lazima zichuje tu
 
Mi nimehamia huko maana hizi za dukani hatari sana.
Kuna siku nimenunua splash cardet 70K nikaifua ikapauka nikasema sinunui tena
Mtumbani ukienda 70K unapata nguo 7 Grade 1

Aya maduka jina tuu ni nguo za kawaida tuu ..ukipata mtu mzuri anakuwa anakuchukulia vitu vizuri vya mtumba au kikitoka kitu kizuri anajua anaanza kukufikiria wewe kwanza utavaa vitu safi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom