Nadhani tatizo linaweza kuwa pande zote. Kwa upande wa wanunuzi wanapaswa kuangalia specifications na instruction za nguo, kuna nguo ambazo zinahitaji zifuliwe kwa machine, na zingine ni dry cleaning tu. Sasa nguo inayohitaji dry cleaning ukiifua kwa maji hata uinyoonshe vipi haitokaa sawa. Na hata nguo za kufua kwa machine pia zina specification za maji unakuta umeambiwa ufue kwa maji baridi tu au moto tu au vuguvugu, sisi tunafua tunavyojua sisi, haiwezi kuwa sawa. Kuna nguo hazi nyooshwi kwa pasi zinanyooshwa kwa mfuke wa moto, sisi tunanyoosha.
Jingine ni maji yetu, huko zitokako maji yana kuwa treated kupunguza mineral contents, hapa kwetu hilo halifanyiki, na kuna wengine hutumia maji ya visima au yakuvuna ya mvua, yoote haya yana athari zake kwenye fabrics.
Sabuni, kuna za unga, vipande, na za maji. Hapa kwetu sabuni nyingi ni kali sana, kwasababu nahisi maji yetu ni hard water na sio soft water hivyo watengenezaji wa sabuni kwa kuzingatia hilo huziongezea kemikali na kuzifanya kali sana, sasa na ufuaji wetu mtu analoweka nguo 24hrs kwenye sabuni kali, anategemea fabrics za hiyo nguo ziwe sawa, hapana.
Huko wanakozitengeneza, hawalengi soko la Afrika, ila kwasababu za kibiashara wanaleta tu au kuchepusha na hapo ndio sisi tusio treat maji, na kutumia sabuni kiasi maalumu na kwa muda maalumu, na tusio tumia washing machines na kupikicha yanatukuta yote haya.
Na nguo zinazofuliwa kwa dry cleaning sisi tuna fua kwa maji tena mtu anailoweka 24hrs, kwanza haihitaji maji kabisa, lakini umeifua, mbaya zaidi umeiloweka 24 hrs huwezi kutegemea iwe au irudie ubora wake.
Hivyo tujifunze kuangalia label zinasemaje kabla ya kununua, na kama hukuangalia label basi angalia kabla ya kuifua, unaweza kuta haifuliwi ni dry cleaning fabrics, na unapo nyoosha angalia label, inahitaji dry heat, au mvuke, ukifuata masharti ya manufacturer hutojuta, na huto lalamika. Sisi tunajisahau, au hatujali kabisa manufacturer instructions, sio nguo tu, hili liko kwenye vitu vyote. Tukijifunza kutafiti na kuangalia mahitaji ya kitu, kwa case hii nguo, na kujali hatuta juta, lakini ukiangalia mahitaji yako tu bila kujali mahitaji ya nguo uliyoinunua bei ghali hutoisha kulalamika kila siku.
Hata mitumba inazo instructions of care, tuwe waangalifu tusijiumize ki uchumi.
Waswahili tunasema, " cheap is expensive" hahaha, any way mmeelewa nadhani.
Kila la kheri.