MVUMBUZI
JF-Expert Member
- Jan 8, 2011
- 5,182
- 2,304
Mahubiri ya Pengo yaliyokuwa yanarushwa na TBC1 yalikatizwa ghafla saa 6:45 mchana leo Jumapili na kuweka muziki wenye theme ya amani kuondoa makali ya mahubiri hayo yaliyokuwa yanarushwa ktk ibada moja ya jumapili leo. Pengo alikuwa anazungumzia unabii wa kitabu cha ufunuo kuna verse inazungumzia habari za joka kubwa jekundu lililoshuka duniani na kushuka na moja ya tatu ya nyota zote. Ndipo alipoanza kuutafsiri kwa context ya Tanzania kama kawaida ya mahubiri na alipoanza kusema " kwa Tanzania unabii huu............."
,TBC1 ikakatiza ghafla na kuweka miziki ya bongo fleva kuhusu amani ya TZ mpaka saa 7 mchana then wakaendelea na vipindi vingine.
Jambo hili limenishangaza kwani najiuliza ni kwa nini TBC1 haitaki kuweka vipindi vinavyowafungua waTZ macho? Ni kwa nini wakatize kipindi kwa stahili ya kihuni namna ile kisa mahubiri yanaigusa nchi?
Kuimba nyimbo za amani baada ya kukatiza yale mahubiri ni kutaka kuwadanganya waTZ kwamba mahubiri ya Kadinali Pengo yalikuwa yanavuruga amani ya nchi.
Kama TBC1 itaendelea na huu unafiki wa kuwanyima waTZ habari za kweli ili wao wapime wenyewe kuna uwezekano wengi tukaachana nayo na kuhamia TV ambazo siyo biased. TBC1 inachuja habari wanazotaka waTZ wazijue na kuondoa habari zinazowafanya waTZ waerevuke na kufanya maamuzi positive kwa mustakabali wa nchi yao. Hizi juhudi za TBC1 zina lengo la kujenga taifa la mandondocha ambao sio informed kufanya mambo tofauti na kile wanachoonyesha.
Hii ni aibu na kuwanyima waTZ haki ya habari kutoka chombo ambacho kinaendeshwa kwa kodi zao.