jjs2017
JF-Expert Member
- May 25, 2019
- 2,023
- 4,213
Habari ndugu zangu..
Mimi sijaenda kwenye nyumba za ibada nipo hapa nawaza sana jinsi viongozi wadini wanavyo changia ndoa nyingi sana kuvunjika kutokana na mafundisho yao ya kila siku.
Kwenye nyumba nyingi sana za ibada wamejaa huko wake zetu na mabinti wengi ambao ndiyo wake zetu watarajiwa.
Ndugu yangu kwanini nasema viongozi wengi wa dini huchangia ndoa nyingi kuvunjika hiii ni kutokana na kauli zao tata ambazo nimeorodhesha hapa chini wanazo kua wanazitoa kwa lengo la kukusanya wanawake wengi ili kujipatia sadaka ( mapato) kwa maslai yao binafsi.
1: WANAWAKE NI JESHI KUBWA
Hii kauli imeleta upinzani sana kwani wanawake wengi walioathiriwa na mpango wa haki sawa wamekua wakiitumia kama silaha ya kumuangamiza mwanaume kinyume na ilivyo tafsiriwa hapo awali enzi za mababu zetu.
2: MAHOBIRI MENGI YANATAJA UCHAWI, KULOGWA NA UWEPO WA MAPEPO WA CHAFU
Mahobiri mengi sana yamekua yakiaminisha kuwa uchawi upo, hali hii upelekea mwanamke aliye ndani ya ndoa kumchukulia mumewe /ndugu wa mume ni mchawi hasa pale kunapotokea changamoto ya kiuchumi na maradhi
3: SITORUDI MISRI NAELEKEA KAANANI
Wanandoa wengi wanaamini misri kwao ni mahusiano waliyo nayo au mapito waliyo pitia kiasi chakukataa kutaka suluhu za kimahusiano wakiamini ni kurudishwa nyuma.
4: " KUTOA MUDA WA KUMTUMIKIA MUNGU
Muda wa kumtumikia Mungu ni jambo zuri sana, ila umetumika kinyume nakufanya wanawake wengi kushinda kwenye nyumba za ibada kwanzia asubuhi mpaka usiku wakifanya usafi, maombi na kujitolea kuombea wengine.
Jambo hili limepelekea sana wanawake wengi kukosa muda na ndoa zao/ wapenzi wao na kutokuthamini watoto wala mume/ mpenzi wake
5: WANAUME TUTAKULA KWA JASHO NA NYIE MTAZAA KWA UCHUNGU
Ni kweli sisi tumeumbiwa kula kwa jasho ila hakuna mahali palipo mkataza mwanamke kufanya kazi kwani imeamriwa "asiye fanya kazi na asile na haikutaja jinsia.
Wamesahau kuwa wao ni wasaidizi wetu na wanaweza kutusaidia katika kufanya kazi na sisi tukiwa kama watawala, ukirejea kwenye sifa za mke mwema kiimani "mwanamke ametajwa kua hali chakula cha uvivu, uliangalia shamba na kulinunua, pia hufanya kazi yake ya mikono kwa moyo" .
Wamesahau kujua hata kazi za nyumbani wakifanya ni thawabu tosha , bali wanaonani utumwa na wanahitaji malipo /kupewa mshahara.
Mahobiri haya yamewafanya wanawake wengi kwaulimbukeni wao kuwageuza wanaume wengi wanao watongoza kuwa ni njia ya kujipatia mapato kwa mgongo wa ndoa / mahusiano
6: MWANAMKE ANAWEZA KUMUOKOA MWANAUME
Hii imepelekea mpasuko ndani ya nyumba na mahusiano kiujumla baina ya mwanamke na mwanamume kiimani,
Unakuta walikua watu wa imani moja , dhehebu moja lakini gafla wanatawanyika kila mtu ana amini katika kile anacho kiamini, huku mwanamke akiamini yeye anaweza kumuokoa mumewe kumbe ndiyo anazidi kumpoteza sana
7: KUTOA SADAKA
Mnapokua mke na mume wote mnakua mwili mmoja na kila kitu mlicho nacho ni kimoja ila msimamizi mkuu ni mwanaume, mwanamke hupaswi kunichukulia tuu hela au mali shambani ukapeleka kwenye nyumba za ibada bila idhini ya mumeo / makubaliano baina yenu. Mahobiri mengi ya kutoa sadaka yamekua yakiwageuza wanawake wengi kuwa waizi wa mali za familia na kuzipeleka zote kwa watumishi.
Wanaume tulipo jaribu kuweka usimamizi kama watawala , wanawake wakafikia mbali zaidi na kuhitaji kujitenga na kua wabinafsi na hata mapato yao hayaonekani ndani ya nyumba bali wanayatumia kulisha watu wengine kwa mgongo wa kutoa sadaka
8: VIKAO VYA WANAWAKE BAADA YA IBADA NA VIONGOZI WA DINI.
kumekuwa na vikao vya mara kwa mara na mikutano ya wanawake , ndani ya hiyo mikutano kumezuka mawaidha yanayo wafanya wanawake waone wanaume siyo kitu mbele ya watumishi wao wa kiimani, kumejenga wanawake kuwa na viburi, jeuri, kutokua watii , kutokua waaminifu, dharau na ubinafsi mkubwa kwa waume zao / wapenzi wao na kupeleka wanaume wengi kuamua kuachana na mpango wa umoja baina ya mwanamke na mwanamume.
9: KUTOA SIRI ZA FAMILIA KWA MGONGO WA KUOMBEWA.
Wanawake wengi wamekua wakutoa siri nyeti za familia kwa watumishi huku wakiamini wataombewa na mwisho wasiku kunikuta kuwa watumwa wa kuombewa na kupeleka kila mapato yao wanayo yapata huko kwenye nyumba zaibada , nayo ni changamoto iliyo haribu ndoa.
10: MAHUBIRI YA MIUJIZA KWA MGONGO WA "AWAHI WALA ACHELEWI"
Mabinti na wamama wengi sana wamekua wakiamini katika miujiza nasiyo kujituma na kuwasikiliza wanaume wao, Wameaminishwa kinyume chakuwa Mungu awahi wala achelewi, hali hii imepelekea wanawake wengi kutosikiliza ushauri wa kiimani na kiuchumi kutoka kwa wanaume wao wakiamini wakati wa Mungu bado haujafika,
Mabinti wengi wamefikia hadi kukataa wanaume waliokua wakijitoa kuwatongoza wakiamini bado wakati haujafika na kusahau kwamba siku zote wakati hauna mwisho, mabinti wamekua wakiringa sana huku wakijiona bado muda wao haujafika,
Vivyo hivyo wanawake wengi walio ndani ya ndoa wamekua wakiongeza muda mwingi sana kushinda kwenye nyumba za ibada huku wakitelekeza majukumu yao ya kifamilia wakiamini bado wakati haujafika na ipo siku utafika tuu.
kiukweli wamesahau maombi ni kutiana moyo sana na kufikia hatua hii kwao ni dalili ya kukata tamaa na kuharibu mahusiano yao
NDUGU ZANGU NIMEFIKIRIA SANA NIMEFIKIA HAPO NAOMBENI KUWASILISHA NA NIPO TEYARI KUKOSOLEWA KWA HOJA ZA MSINGI,..
Nb: ndani ya maandishi haya kuna makosa madogo ya kiuandishi.