TBC1 yakatiza mahubiri ya Pengo kwa kuongelea habari za TZ

MVUMBUZI

JF-Expert Member
Jan 8, 2011
5,183
2,304
Mahubiri ya Pengo yaliyokuwa yanarushwa na TBC1 yalikatizwa ghafla saa 6:45 mchana leo Jumapili na kuweka muziki wenye theme ya amani kuondoa makali ya mahubiri hayo yaliyokuwa yanarushwa ktk ibada moja ya jumapili leo. Pengo alikuwa anazungumzia unabii wa kitabu cha ufunuo kuna verse inazungumzia habari za joka kubwa jekundu lililoshuka duniani na kushuka na moja ya tatu ya nyota zote. Ndipo alipoanza kuutafsiri kwa context ya Tanzania kama kawaida ya mahubiri na alipoanza kusema " kwa Tanzania unabii huu............."
,TBC1 ikakatiza ghafla na kuweka miziki ya bongo fleva kuhusu amani ya TZ mpaka saa 7 mchana then wakaendelea na vipindi vingine.

Jambo hili limenishangaza kwani najiuliza ni kwa nini TBC1 haitaki kuweka vipindi vinavyowafungua waTZ macho? Ni kwa nini wakatize kipindi kwa stahili ya kihuni namna ile kisa mahubiri yanaigusa nchi?
Kuimba nyimbo za amani baada ya kukatiza yale mahubiri ni kutaka kuwadanganya waTZ kwamba mahubiri ya Kadinali Pengo yalikuwa yanavuruga amani ya nchi.

Kama TBC1 itaendelea na huu unafiki wa kuwanyima waTZ habari za kweli ili wao wapime wenyewe kuna uwezekano wengi tukaachana nayo na kuhamia TV ambazo siyo biased. TBC1 inachuja habari wanazotaka waTZ wazijue na kuondoa habari zinazowafanya waTZ waerevuke na kufanya maamuzi positive kwa mustakabali wa nchi yao. Hizi juhudi za TBC1 zina lengo la kujenga taifa la mandondocha ambao sio informed kufanya mambo tofauti na kile wanachoonyesha.
Hii ni aibu na kuwanyima waTZ haki ya habari kutoka chombo ambacho kinaendeshwa kwa kodi zao.
 
Ndiyo Sera za magamba hizo kuwa na raia mambumbumbu ili watumie umbumbumbu wao kuwatawala daima.
 
Wanatimiza maagizo walizo pewa. Unamkumbuka tido mhando, umahiri wake ulimwondo tbc1.

Ukweli ni kwamba TBC1 sasa inaelekea kubaya kwani inaonyesha mkurugenzi anayejulikana na boya tu kwani kuna mtu very influential anayesimamia kila operasheni day and night na ku command kuondolewa kipindi chochote ambacho kinaongea negativism kuhusu JK na serikali yake. Hata hivyo hii ni sawa na kuficha uchafu chini ya kapeti kwani uchafu ni uchafu tu na unakera popote ulipo na dawa ya uchafu ni kuutupa panapostahili na siyo kuuficha chini ya kapeti
 
umefika sasa wakati wa TBC kumilikiwa na umma na sio serikali tena,kwa mtakaolewa namaanisha nn mfano BBC,KBC,KENYA AIRWAYS NK mashirika yanayomilikiwa na umma yanakuwa huru na kukua zaidi na hata kuiumbua serikali, waajiriwa na tbc wapo kwa maslahi ya serikali ya CCM na sii kwaa ajili ya wananchi. tunapotoa maoni ya katiba mpya na hili likumbukwe kuichukua airtanzania na tbc kuwa mali ya umma.
 
mim hiyo channel siangalii kabisa!!!!tv za kibongo chuki binafs zimetawala!ngoja aljazeera swahili ianze kazi!wataangalia tv station zao wenyew!sie wajanja tunajirusha aljazeera
 
Acha masikhara mvumbuzi,yaani unataka wan JF waamini kuwa hujui yaliyompata Tido, wanahofia vibarua na ubaya ni kuwa wao hawapo competent kama Tido alivyokuwa
 
Mlipiga kura mkawachagua na kuwarudisha madarakani, muwe tayari kuishi na matokeo ya uchaguzi huo.

Nashukuru Mungu wanafamilia walinielewa 2010 nilipopiga kampeni kama baba na kauli mbiu ya CCM NO CDM YES for change. Ila ningepata dawa ambayo mtu akinywa kama soda fahamu zinafunguka ningechangia hiyo dawa ili waTZ wote wanywe waone full picture ya udhalimu wa CCM. Nasema hivi kwa sababu supporters wengi wa CCM ni the poorest of the poor wa Tanzania ambao bila kuona kofia, shati au kanga ya kijani hawapigi kura na hawa wanahitaji elimu kubwa ili wabadilike. CCM inatumia ignorance yao kutwaa uongozi kila mara.
 
Acha masikhara mvumbuzi,yaani unataka wan JF waamini kuwa hujui yaliyompata Tido, wanahofia vibarua na ubaya ni kuwa wao hawapo competent kama Tido alivyokuwa

Najua kilichompata Tido ni kukataa kuwa mnafiki na badala yake akatumia professional yake inavyotakiwa bila upendeleo na akina Makamba wakamletea za kuleta kwani walihisi ndiye mchawi wa CCM while wachawi walikuwa waTZ waliochoshwa na usanii wa Magamba.
 
Msiwalaumu sana hawa jamaa, ni amri wanazopewa na wakuu wao. Iko siku watajiunga nasi tu!
 
TEC na CCT inabidi waihoji TBC ni kwanini wamekatisha mahubiri ikiwa muda ulikuwa unaruhusu na hapakuwa na jambo lolote la dharura kwa maslahi ya nchi. Pili, inabidi TBC waeleze namna watakavyo
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom