Ninachojua Tbc ni ccm damudamu kama wameipendelea cdm leo yawezekana kuna tatizo. Maybe wamecheleweshewa salary wakamind si nasikia siku hz every 23rd salary out.
Mimi nishamwambia mke cku nikikuta umeweka tbc nakupa talaka mara1
Jana saa mbili usiku nilikuwa nikiangalia taarifa ya habari ya TBC1 na habari kuu jana ilikuwa ni kutua kwa mahelkopita huko Igunga kwa ajili ya kutumika katika mikutano ya kampeni. TBC1 walionyesha helkopita ya CCM ikitua na Makamba akapokelewa na Mwigulu na watu wengine. Kisha ikaonyeshwa kwa UFUPI SANA Mwigulu akihutubia na kisha makamba akasikika akisema maneno mawili matatu tu basi. Pia TBC1 haikuonyesha UMATI wa watu ambao hao viongozi wa CCM walikuwa wakihutubia!! Kwa kifupi coverage kwa CCM ilikuwa kidogo sana.
Kisha nikashuhudia coverage ya CHADEMA. Walianza kuonyesha helkopita ikiwa angani na maneno CHADEMA yakionekana, kisha wakaionyesha helkopita ikiwa eneo fulani ambalo naamini ni kituo cha mafuta ikiwa inakunywa mafuta. Baada ya hapo helkopita ya CHADEMA ikaonyeshwa ikitua huko Nkinga na Mwenyekiti wao akashuka na kuhutubia. Kinyume na walivyo cover hotuba ya CCM, hapa Mbowe alipewa muda mreeefu akihutubia kuhusu mambo ya siasa na dini na wakati huohuo TBC1 ikionyesha umati wa watu ambao Mbowe alikuwa akihutubia. Baada ya hotuba TBC1 walionyesha helkpita ya CHADEMA ikituka kuondoka eneo la mkutano.
Kwangu mimi naona TBC1 hawakuitendea haki CCM kwa kuipa coverage kidogo sana hasa juu ya helkopita ambayo imegeuka kuwa ni kete ya kisiasa huko Igunga. Pia TBC1 hawakumuonyesha mpambanaji Magufuli wakati akiunguruma huko Igunga.
siyo kwamba wamefanya hivyo kwa bahati mbaya bali wana malengo yao lengo kuu nikuwapa nafasi ccm siku ya mwisho ya kampeni ilikuongeza mhemko..pili alicho kuwa anakiongea mbowe ni swala la kitaifa ambalo kila mtanzania angependa kulisikia kutoka kwa kiongozi wa juu hasa xhama tawala akiliongelea kwa hisia kali tofauti na wanavyofanya magamba wanalifanya mtaji wa kujiatia kura bila kujari madhara yatokanayo na kampeni zao hizo chafu..
Kimbunga you know what?
TBC1 walionyesha uhalisia wa mambo yalivyokuwa jana kule Igunga. Camera zao zilimwonyesha Nnape cjui na Januari wakiteremka kwenye Chopa lakini hawakuonyesha umati wa watu waliohudhuria pale MAANA HAUKUWEPO!! Wewe ulitegemea waelekeza camera kwenye miti na uwanja mtupu?Waliona aibu maana hakukuwa na watu.
Lakini Mbowe alipotua na Chopa ule UMATI ULIKUWA NI WA KUFA MTU. Nilifurahia sana taarifa ya TBC1 jana jioni maana walionyesha HALI HALISI BILA KUCHAKACHUA. Tunataka coverage ya namna hii mpaka siku ya kupiga na kuhesabu kura.
Big up TBC1!
Mara ya kwanza niliposoma heading nikafikiri mtoa mada amekosea heading.